Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmad akiteta jambo na Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Mtwara Mikindani, Geofrey Mwanichisye katika ukumbi wa
Mikutano wa chuo cha sanaa-Bagamoyo.
Juma Mohamed, Bagamoyo
Licha ya
wakulima wa baadhi ya wilaya katika mkoa wa Ruvuma kukataa kuuza korosho zao
kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, serikali imesema mfumo huo utaendelea
kutumika na maeneo yote nchini yanayolima zao hilo yanapaswa kutekeleza mfumo
huo.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa tasnia ya korosho nchini uliofanyika
katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, waiziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dokta Charles Tizeba, amesema bila mfumo huo wakulima wataendelea kutonufaika
na zao hilo.
 |
Dkt. Charles Tizeba
 |
Mwenyekiti
wa Bodi ya Korosho Tanzania-CBT, Anna Abdallah, akiongea na wadau wa
korosho katika mkutano unaowakutanisha wadau wa zao hilo kutoka mikoa
yote inayolima korosho nchini.
|
|
Baadhi ya
wabunge kutoka mkoani Mtwara wameunga mkono agizo hilo la serikali licha
kuendelea kusisitiza usimamizi bora, huku wakulima kutoka wilayani Tunduru
wakiahidi kuanza kuuza mazo yao kupitia mfumo huo katika msimu ujao wa korosho
ambao unatarajiwa kuzinduliwa katika mkutano huo.
Mkutano huo
uliowakutanisha wadau wa tasnia ya korosho nchini, pamoja na mambo mengine
unatarajia kupanga bei dira ya zao hilo kwa msimu mpya wa 2016/2017.
|
No comments:
Post a Comment