Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati)akitembezwa ndani ya kiwanda cha Urafiki Textile mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho. |
Na Evelyn Mkokoi, Dar es Salaam.
Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Nida Textile Industries kilichopo Tabata Jijini Dar es Salaam kimetozwa
faini ya sh. Milioni 30 kwa kosa la uchafuzi wa mazingira kwa kutiririsha maji
taka na yenye sumu katika mto kibangu na kuhatarisha maisha ya viumbe hai na wafanyakazi kiwandani hapo.
Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku saba kwa Baraza
la Taifa na Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC imetokana na ziara ya Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ya
kukagua viwanda na mazingira nchini ambapo sambamba na adhabu hiyo kiwanda
hicho kimetakiwa kufanya usafi mara moja katika mazingira kiwandani hapo.
Aidha, kimetakiwa kupeleka ripoti ya upimaji wa moshi na
vumbi litokanalo na makaa ya mawe na maji yanayotoka kiwandani hapo ili
serikali kujiridhisha kama si hatarishi kwa mazingira.
‘’Ili kujiridhisha NEMC waje nao wachukue vipimo vya maji
haya yanayotiririka ili tuone kama ni salama kwa mazingira na viumbe hai, na
kiwanda kiwasilishe cheti cha utirishaji maji kwa Baraza.” Alisisitiza Naibu
Waziri Mpina.
Kwa upande wake Meneja wa kiwanda hicho Mohamed Rajabu
alipoulizwa kama ameikubali adhabu hiyo, alitupia lawama kwa NEMC na kusema
kuwa wao ndo walitoa kibali cha athari ya tathimini ya mazingira kwa kiwanda
hicho na ndiyo maana kinaendelea kufanya kazi na kuwa wangekuwa wanapita kwanza
na kutoa onyo kwa wenye viwanda kabla ya kutoa adhabu kali ya mamilioni ya
fedha.
Aliongeza kuwa
kukabiliana na faini kubwa hivyo kwa kiwanda hicho kunaweza kupelekea wafanyaki
kupoteza ajira zao kwa kupunguzwa kazini.
Akihitimisha katika zoezi hilo Naibu waziri Mpina aliwataka
wawekezaji na wenye viwanda nchini kutii sheria na kuthamini maisha ya
wafanyakazi kwa kuyaweka mazingira safi na salama.
No comments:
Post a Comment