Tuesday, July 19, 2016

NDANDA FC kuanza VPL kwa kuwafuata SIMBA SC Taifa.


Kikosi cha Ndanda FC msimu wa 2015/2016



Na Juma Mohamed, Mtwara

TIMU ya soka ya Ndanda FC ya mkoani hapa imepangwa kuanza ugenini na wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club, katika michuano ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inaonesha ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu, huku ‘Wanakuchele’ Ndanda FC wakianzia ugenini dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar kabla ya kurejea Nangwanda kuvaana na Yanga.
Akizungumza na Juma News, afisa habari wa Ndanda, Idrissa Bandari amesema wao wameipokea vyema ratiba hiyo na kwamba kwa sasa wanakiandaa vyema kikosi chao ili kiwe imara kwa ajili ya kuimili mikimikiki ya ligi hiyo.

Kikosi cha Simba SC msimu wa 2015/2016



“Vyovyote ingekuja, tungechukulia uzito kama ratiba zingine kama ambavyo zinakuja kwetu kuwa na uzito mkubwa, kwahiyo tunaimani kwa ratiba hii pia ni ngumu lakini tunakwenda nae hivyohivyo kama ilivyo..sio mechi rahisi ni mechi ngumu tunazoanza nazo lakini hakuna mechi yeyote kwenye ligi inayokuwa ya kwanza, katikati au yamwisho ikawa rahisi..” alisema Bandari.
Katika hatua nyingine, Bandari alisema wamekuwa wakizisikia taarifa za kocha wao Malale Hamsini kujiunga na klabu ya JKT Ruvu ya Pwani na kwamba leo jioni uongozi unakaa kikao ambacho kitajadili juu ya suala hilo, huku Malale mwenyewe akidai kuwa mustakabali wake utatokana na maamuzi ya klabu ya JKU ya Zanzibar ambayo ndio mwajiri wake.


1 comment:

Unknown said...

Duh kazi kazi....