Thursday, May 5, 2016

Wazazi Mtwara watakiwa kupiga vita watoto wao kuishia la saba.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya hoteli, Amina Mussa, katika maafali ya kuhitimu mafunzo hayo katika ukumbi wa hoteli ya Old Boma.



Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiongea katika maafali ya kuhitimu mafunzo ya hoteli katika hoteli ya Old Boma, Mtwara.



Wahitimu wa mafunzo ya hoteli 



Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya hoteli mmoja wa wahitimu hao.



Na Juma Mohamed, Mtwara.

WAZAZI na walezi mkoani hapa wametakiwa kuwaendeleza kielimu watoto wao walioishia katika elimu msingi ili waweze kunufaika na uwekezaji unaofanyika kupitia kampuni mbalimbali.
Akizungumza katika maafali ya kuhitimu mafunzo ya hoteli yaliyofanyika katika hoteli ya Old Boma, Mikindani, mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, alisema vijana wengi wanahangaika kutafuta ajira kutokana na kukosa elimu kwasababu wengi wao wana elimu ya msingi ambayo haiwezi kuwapatia ajira itakayokidhi mahitaji yao.
Alisema, kwa namna ambavyo kasi ya uwekezaji inavyoongezeka mkoani hapa ndivyo ambavyo mahitaji ya ajira kwa vijana yanavyozidi kukuwa, hivyo ni jukumu la wazazi kuona umuhimu wa kuwaendeleza vijana wao kwasababu kuna vyuo mbalimbali vinavyotoa fani zitakazowasaidia kupata ajira.

Fatma Ally


“Kwahiyo mwanao ambaye ameishia darasa la saba hebu jitahidi ufanye mpango baada ya miaka miwili hijayo afanye mtihani wa ‘form four’..na yule ambaye amemaliza ‘form four’ asitegemee tu JKT, mfano mimi JKT pale nina nafasi sita za darasa la saba ambazo inabidi nizigawanye katika halmashauri Tatu..” alisema.
Aliwataka wananchi wa Mtwara kutokubali kuwa mashuhuda wa maendeleo kwa wenzao kutoka maeneo mbalimbali kwa kuacha fursa ambazo zinaweza kuwanufaisha zikiwanufaisha wengine kutokana na kuwa nyuma kielimu.
Aidha, alilipongeza shirika la Trade Aid ambalo ndio wanaondesha mafunzo hayo kwa wahitimu katika Hoteli Hiyo ya kitalii iliyopo katika mji wa Mikindani, kwa kushirikiana na wakazi wa mji huo na kuweza kuendeleza miradi mbalimbali ikiwamo kuendesha Hoteli hiyo.

Kwaito nayo ilihusika kwenye mahali 


Naye, meneja mradi wa Shirika hilo Emmanuel Mwambe, alisema shirika lilianza ukarabati wa jengo la Old Boma mwaka 1999 ambapo lilipata kibali kutoka katika serikali ya wilaya na miaka mitano baadaye ikafunguliwa hoteli kwa malengo ya kuisaidia jamii ya wakazi wa Mikindani na Mtwara kwa ujumla.
“Lakini Trade Aid tukafikiria tukasema hapana tutasaidia vipi, sio biashara ya hoteli, ngoja tuangalie tunafundishaje vijana amabao wataenda kujiajiri, na kweli Trade Aid imeanza kutoa mafunzo yake kwa miaka mingi katika fani mbalimbali na mimi nilikuwepo hapa miaka ya nyuma kama mwanafunzi..” alisema.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya hoteli, Amina Mussa, katika maafali ya kuhitimu mafunzo hayo katika ukumbi wa hoteli ya Old Boma.


Amina Mussa, ambaye ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo, alisema amefurahishwa na hatua kuhitimu kwani baada ya hapo anatarajia kupata ajira kupitia ujuzi wa masuala ya hoteli ambao ameupata katika kipindi chote cha mafunzo, huku akiwataka vijana wengine kuchangamkia kujiunga na mafunzo hayo yanayotolewa bila malipo.


Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa hoteli ya Old Boma na wahitimu wa mafunzo ya hoteli.


No comments: