Thursday, May 12, 2016

Serikali kuwafilisi na kuwafunga mawakala wababaishaji wa pembejeo za korosho..>>>>> www.jumanews.blogspot.com



Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akizungumza na wadau wa korosho katika uzinduzi wa Ugawaji na Uhamasishaji wa Pembejeo za Ruzuku za Zao la Korosho msimu wa 2016/2017, uliofanyika katika maghala ya TANECU wilayani Tandahimba, Mtwara.



Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, katika ziara fupi za kuangalia pembejeo za ruzuku za zao la korosho


Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Mfaume Juma, akizungumza katika uzinduzi wa Ugawaji na Uhamasishaji wa Pembejeo za Ruzuku za Zao la Korosho msimu wa 2016/2017, uliofanyika katika maghala ya TANECU wilayani Tandahimba, Mtwara.


Kaimu katibu mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Zao la Korosho (WAKFU), Ramadhani Mmari, akitoa taarifa ya mfuko katika uzinduzi wa Ugawaji na Uhamasishaji wa Pembejeo za Ruzuku za Zao la Korosho msimu wa 2016/2017, uliofanyika katika maghala ya TANECU wilayani Tandahimba, Mtwara.


Na Juma Mohamed, Tandahimba.

MAWAKALA wa ugawaji wa pembejeo za zao la korosho nchini wametakiwa kutenda haki kwa wakulima na kuacha kufanya kazi hiyo kwa ajili ya masilahi yao na atakaefanya hivyo serikali itawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafilisi mali zao na kuwafunga.
Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, wakati wa uzinduzi wa ugawaji na uhamasishaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho msimu wa kilimo wa 2016/2017, uliofanyika wilayani Tandahimba, na kusema kuwa mawakala hao wanakwepa kufanya kazi na serikali za vijiji.

Halima Dendego



“Serikali ya kijiji ndio yenye watu, uongo kweli? Ndio yenye wakulima, uongo kweli?..leo wakala unasema hutaki kufanya kazi na serikali ya kijiji inamaana una watu wako kwenye mfuko unaotaka kuwapa pembejeo zetu za ruzuku, hatuta kubali kama kazi hii imekushinda ni hiyari, hacha wenyewe tutaifanya..” alisema.
Alisema, wakala atakaekwenda kinyume na matakwa ya serikali kwa kuuza pembejeo za ruzuku kwa bei anayotaka mwenyewe na hata ikibainika pembejeo hizo kuuzwa katika maduka kwa bei ya soko, utafilisiwa na kufungwa.

Baadhi ya wadau wa zao la korosho waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Ugawaji na Uhamasishaji wa Pembejeo za Ruzuku za Zao la Korosho msimu wa 2016/2017, uliofanyika katika maghala ya TANECU wilayani Tandahimba, Mtwara.



“Kwahiyo nitoe tahadhari kwa mawakala nchi nzima, mchezo wa kucheza na wakulima wetu uwe mwisho..” aliongeza.
Aidha, aliwataka wadau wa zao hilo kushirikiana na viongozi wa Bodi ya Korosho ya Korosho Tanzania (CBT), na viongozi wa serikali katika kuwapiga vita watu wachache wanaosambaza propaganda kuwaaminisha wakulima kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani haufai.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na kaimu katibu mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Zao la Korosho (WAKFU), Ramadhani Mmari, wakati wa kuangalia pembejeo za ruzuku za zao la korosho katika maghala ya Tandahimba.


Alisema, mfumo huo una manufaa makubwa kwa wakulima na ndio maana wataalamu wa zao hilo wameuamini ambapo kuna baadhi ya watendaji ndio wanataka kuuharibu hivyo jitihada za dhati zinahitajika kuweza kupambana nao.
Alisisitiza kwa mikoa na wilaya zinazolima zao hilo kujitahidi kuhamasisha mfumo huo ambao mkoa wa Pwani tayari wakulima wake wamehamasika kwa kiasi kikubwa kuutumia na kuona mafanikio yake.
Naye, mwenyekiti wa Bodi hiyo, Anna Abdallah, alisisitiza kwa wakulima kutekeleza agizo la waziri mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, la kuvitaka vijiji kupanda miche 5,000 na kila kaya angalau walime heka moja ya korosho.

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Anna Abdallah, akizungumza katika uzinduzi wa Ugawaji na Uhamasishaji wa Pembejeo za Ruzuku za Zao la Korosho msimu wa 2016/2017, uliofanyika katika maghala ya TANECU wilayani Tandahimba, Mtwara.

No comments: