Friday, May 27, 2016

Mafanikio ya Mourinho akiwa na vilabu Vinne tofauti..je, UTD itaingia kwenye mkumbo??


Mourinho

Jose Mourinho ametangaza rasmi kuwa meneja mpya wa klabu ya Manchester United.
Ametia saini mkataba wa miaka mitatu.
Mreno huyo anachukua nafasi ya Mholanzi Louis van Van Gaal, aliyefutwa kazi Jumatatu siku mbili baada ya kushinda Kombe la FA.
"José kusema kweli ndiye meneja bora zaidi wa soka kwa sasa," naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward amesema.


Mourinho, 53, amesema: "Kuwa meneja wa Manchester United ni heshima kubwa sana katika mchezo huu. Ni klabu inayofahamika sana na kuenziwa kote duniani.”
Amesema amekuwa akihisi mvuto wa kutaka kuwa Old Trafford na kwamba daima amekuwa akisikizana na mashabiki wa United.
“Nasubiri kwa hamu kuwa meneja wao na kujivunia uungwaji mkono wao miaka ijayo.
“Kuna hisia fulani na upendo ambao huwezi kupata kutoka kwa klabu nyingine.”


Mourinho amekuwa bila kazi tangu afutwe na klabu ya Chelsea Desemba mwaka jana.
Mourinho ametia saini mkataba baada ya mazungumzo ya siku tatu baina yake, wakala wake Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United.
Moja ya mambo ambayo anatarajiwa kuyafanya ni kumchukua mshambuliaji kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic, ambaye walifanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan.
Mourinho anaonekana kuwa ni kocha mwenye mafanikio makubwa hasa ukilinganisha rekodi zake katika vilabu Vinne alivyowahi kuvifundisha, sasa anakabidhiwa majukumu ya kuinoa timu ya Manchester United ambayo baada ya kuondoka mikononi mwa Sir Alex Ferguson bado mashabiki wake hawajatulizwa mioyo yao kwa kupata angalau mafanikio waliyokuwa wakiyapata wakati wa Mskoti huyo.

Swali ni Je, Mourinho ataweza kurejesha furaha kwa mashabiki wa UTD ambayo imeshindikana kwa Moyes na Van Gaal??????...

CHANZO: BBC SWAHILI



No comments: