Sunday, July 27, 2014

EPHRAIM MASHABA, KOCHA MPYA BAFANABAFANA

Ephraim Mashaba
           

Na Juma Mohamed
 
Shirikisho la soka la Afrika Kusini (Safa), limemtangaza Ephraim Mashaba kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya nchini humo Bafanabafana.

Mashaba mwenye umri wa miaka 63 ameteuliwa kuchukuwa nafasi ilioachwa na Gordon Igesund ambae mkataba wake ulifikia tamati.
Akitangazia uteuzi huo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana, Rais wa Safa Dr Danny Jordaan, amesema “rekodi yake inadhihirisha wazi kuwa ni mchapa kazi na tunatarajia atatimiza ndoto zetu tunazozitarajia na kuwa katika nafasi za juu”. Alisema.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa kocha mkuu wa Bafanabafana, Mashaba amesema anaishukuru Safa kwa kumteuwa na amekubali kukumbana na changamoto zitakazomkabili.
Mashaba ambae alikuwa kocha wa timu ya taifa ya mali ya umri chini ya miaka 20, ameongeza kuwa atahakikisha kuwa anarejesha heshima ya timu ya taifa ya Afrika Kusini akishirikiana vyema na wadau wa soka wa nchi hiyo, lengo ni kuhakikisha timu inarudi kileleni.
Mashaba alizaliwa August 06, 1950 na aliifundisha Bafanabafana toka mwaka 2002-2004, ambapo hii itakuwa ni awamu yake ya pili kwa timu ya taifa.
Kibarua chake cha kwanza kwa Bafanabafana itakuwa katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco dhidi ya Sudani, itakayofanyika kati ya September 5-7, 2014 huko Khartoum.

SOURCE: Super Sport.

No comments: