Tuesday, September 4, 2012

SERENGETI BOYS KAMBINI MBEYA



TIMU ya taifa ya vijana wa umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imeondoka leo asubuhi kwenda mkoani Mbeya kuendelea na maandalizi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za vijana Afrika zitazofanyika nchini Morocco mwakani.
Timu hiyo imepangiwa kupambana na Misri katika hatua inayofuata, pambano hilo linatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu. Serengeti ilipata tiketi ya kumenyana na Misri, baada ya Kenya kujitoa kwenye michuano hii.
Serengeti imekwenda Mbeya kwa mwaliko wa Chama cha Soka Mbeya Mjini (MUFA), ambacho, kitaihudumia kwa malazi, chakula na huduma nyingine ndogondogo na itacheza mechi kadhaa za majaribio ikiwemo dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.

No comments: