|
Straika mpya wa Manchester United, Robin van
Persie akishangilia baada ya kufunga 'hat-trick' dhidi ya Southampton wakati wa
mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Saint Mary's mjini
Southampton, kusini mwa England leo. Man U ilishinda 3-2. Picha:
REUTERS |
|
Beki wa Manchester United, Rio Ferdinand
akishangilia baada ya Robin van Persie kufunga 'hat-trick' dhidi ya Southampton
wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Saint Mary's mjini
Southampton, kusini mwa England leo. Man U ilishinda 3-2. Picha:
REUTERS |
|
Straika mpya wa Manchester United, Robin van
Persie (haonekani pichani) akifunga goli lake la tatu dhidi ya Southampton
wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Saint Mary's mjini
Southampton, kusini mwa England leo. Man U ilishinda 3-2. Picha:
REUTERS |
|
Straika mpya wa Manchester United, Robin van
Persie (kushoto) akikosa penalti aliyoipiga kwa staili ya "Panencra" dhidi ya
Southampton wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Saint
Mary's mjini Southampton, kusini mwa England leo. Man U ilishinda 3-2. Picha:
REUTERS |
|
Straika mpya wa Manchester United, Robin van
Persie akishangilia goli lake la tatu dhidi ya Southampton wakati wa mechi yao
ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Saint Mary's mjini Southampton, kusini
mwa England leo. Man U ilishinda 3-2. Picha:
REUTERS |
|
Beki wa Manchester United, Rio Ferdinand
akishangilia baada ya Robin van Persie kufunga 'hat-trick' dhidi ya Southampton
wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Saint Mary's mjini
Southampton, kusini mwa England leo. Man U ilishinda 3-2. Picha:
REUTERS |
|
Straika mpya wa Manchester United, Robin van
Persie (kulia) akishangilia goli lake la tatu pamoja na wachezaji wenzake wakati
wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa Saint Mary's mjini Southampton,
kusini mwa England leo. Man U ilishinda 3-2. Picha:
REUTERS |
|
Kiungo wa Newcastle United, Hatem Ben Arfa
akifunga goli dhidi ya Aston Villa wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England
mjini Newcastle, kaskazini mwa England Septemba 2, 2012. Picha:
REUTERS |
|
Kiungo wa Newcastle United, Hatem Ben Arfa
akishangilia goli alilofunga dhidi ya Aston Villa wakati wa mechi yao ya Ligi
Kuu ya England mjini Newcastle, kaskazini mwa England Septemba 2, 2012. Picha:

LONDON, England
ROBIN van Persie alifunga magoli
mawili ya dakika za lala-salama na kukamilisha 'hat-trick' yake iliyowapa
Manchester United ushindi wa aina yake wa 3-2 dhidi ya Southampton katika mechi
yao ya Ligi Kuu ya England leo.
Mholanzi huyo alikosa penalti wakati timu yake
ikiwa nyuma 2-1 na kuonekana kama Man U ilikuwa ikielekea katika kipigo chao cha
pili katika mechi tatu za ufunguzi za ligi lakini alirekebisha makosa yake kwa
magoli mawili katika dakika za lala salama na kuzoa pointi zote.
Goli lake la kichwa katika dakika
ya 92 lilikuwa ni bao lake la 100 katika Ligi Kuu ya England na la nne katika
mechi tatu alizoichezea Man U tangu alipojiunga akitokea Arsenal kwa ada ya
uhamisho ya paundi milioni 24 katika kipindi cha usajili kilichomalizika Ijumaa.
Mapema leo, Lukas Podolski, mtu
ambaye ana jukumu la kuziba pengo la Mholanzi huyo kwa Arsenal, alifungua
akaunti yake ya mabao katika Ligi Kuu ya England katika ushindi wa 2-0 ugenini
dhidi ya Liverpool. Goli jingine la Arsenal lilifungwa na Santi
Cazorla.
Ulikuwa ni ushindi wa
kwanza wa Arsenal, na magoli yao ya kwanza msimu huu, baada ya sare mbili za
0-0, wakati Liverpool pointi moja waliyonayo katika mechi zao tatu za kwanza za
msimu inaweka rekodi ya mwanzo mbovu zaidi katika miaka 50.
Katika mechi nyingine ya leo jioni, Newcastle
United walishikiliwa kwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Aston Villa, na kuwaacha
Southampton wakiwa timu pekee ya Ligi Kuu ya England ambayo haijapata pointi
hata moja
SOURCE:STRAIKA
No comments:
Post a Comment