Thursday, August 9, 2012

SUALA LA USAJILI WA REDONDO KUTOLEWA UAMUZI NA TFF

Baada ya Azam kuendelea kumng'ang'ania kiungo Ramadhan Chombo 'Redondo' aliyejiunga na Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema suala hilo litamalizwa na Kamati ya Maadili, Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema kuwa hivi sasa hawatalitolea ufafanuzi wowote suala hilo kwa kuwa muda wa usajili bado mpaka Agosti 10 mwaka huu.

Alisema baada ya usajili huo wa wachezaji kukamilika ndipo Kamati ya Maadili, Sheria na Hadhi za wachezaji ambayo iko chini ya Alex Mgongolwa itakapokaa na kupitia usajili wa klabu zote.

Redondo juzi alitangaza kuwa ameamua kusajili klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupata ofa nono kutoka katika klabu ya Simba huku akisema yeye ni mchezaji huru kwa sababu mkataba wake na Azam umeisha tangu Juni mwaka huu.

Alisema kuwa viongozi wa klabu ya Azam awali walimwambia kuwa wangemuongeza mkataba, lakini walikuwa kimya mpaka alipokuja kupata ofa ya Simba na kuona asifanye makosa nafasi hiyo ndipo alipoamua kusaini Simba.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassoro alisema kuwa Simba wamekurupuka kumsajili mchezaji huyo kwani bado ni mali yao halali.

Alisema hiyo sio mara ya kwanza kwa Simba kukurupuka kwani awali walimchukua mchezaji wa Azam, Ibrahimu Rajabu 'Jemba', lakini mwisho wa siku walimrudisha, hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa Redondo siku ya mwisho

No comments: