Thursday, August 9, 2012

SIMBA YANG'ARA SUPER 8, AZAM YAPIGWA NA MTIBWA NYUMBANI

SHUJAA WA SIMBA; Christopher Edward

 
SIMBA SC jioni imepata ushindi wa kwanza katika michuano ya BancABC Sup8r kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, baada ya kuifunga Mtende FC ya Zanzibar mabao 2-0.
Simba, ambayo kwenye mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya 1-1 na Jamhuri ya Zanzibar pia, mabao yake katika mchezo wa leo yalifungwa na Christopher Edward dakika ya 11 na 26 kwa penalti.
Mtende walilazimika kumaliza pungufu mechi hiyo, baada ya mchezaji wake, Rajab Mzee kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 86 kwa kumtolea lugha chafu refa wa kike, Judith Gamba.
Simba inatumia kikosi chake cha pili kwenye mashindano haya, ambacho kipo chini ya kocha Suleiman Abdallah Matola, Nahodha wa zamani wa Simba SC.
Katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam walifungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mabao yote ya Mtibwa yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji wakiwa ni Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Hussein Javu.
Mtibwa iliyoifunga Polisi Moro 2-0 kwenye mchezo wa kwanza, sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Azam yenye pointi tatu, ambayo katika mchezo wake wa kwanza, iliifunga Super Falcon 2-0.
 

MUAMBA ANAHITAJI UPASUAJI ZAIDI WA MOYO KUPATA MATUMANI YA KUCHEZA TENA


KIUNGO Fabrice Muamba ameambiwa anahitaji upasuaji zaidi wa moyo, kama anataka matumaini ya kucheza tena soka.
Kiungo huyo wa Bolton yupo Ubelgiji kwa mtaalmu wa tiba za moyo, miezi mitano baada ya 'kufariki dunia kwa dakika 78' kwenye Uwanja wa White Hart Lane katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Spurs.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amemtembelea mtaalamu Pedro Brugada kwa matumaini ya kutimiza ndoto zake za kurejea uwanjani siku moja kucheza tena soka.
Hoping for more: Fabrice Muamba is desperate to resume his playing career
Fabrice Muamba

Recovery: Muamba 'died' for 78 minutes during an FA Cup match at Spurs
Muamba alipofariki kwa dakika 78

No comments: