SHIRIKISHO
la soka Tanzania (TFF) limesogeza mbele kipindi cha kuwasilisha usajili kwa
klabu za ligi kuu na ligi Daraja la kwanza msimu wa 2012/2012 hadi Agosti 15
mwaka huu.Awali zoezi hilo lilikuwa likamilike leo.
Katibu
Mkuu wa TFF , Angetile Osiah alisema kwamba marekebisho hayo yanatokana na
mkanganyiko uliojitokeza na kusababisha baadhi ya vilabu kuchelewa kuwasilisha
majina.
Alisema
kutokana na mabadiliko hayo, muda wa siku saba za kuwasilisha pingamizi utakuwa
kuanzia Agosti 15 hadi Agosti 22, 2012, kabla ya kamati ya Katiba, Sheria na
Hadhi za Wachezaji kukutana kupitisha usajili Agosti 24 hadi Agosti 25,
2012.
Alisema
klabu zinatakiwa ziwasilishe usajili pamoja na mikataba ya wachezaji kama kanuni zinavyotaka na usajili wa kwanza utahusu timu
za vijana walio na umri chini ya miaka 20.
Katibu
hiyo pia amezitaka klabu zote zinazoshiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza
kuwasilisha majina ya viwanja zitakazovitumia kwa ajili ya msimu
ujao.
“Pia
klabu husika ziwasiliane na vyama vyao vya mikoa ili viwasilishe maombi ya
kutumia viwanja hivyo kwa mechi za ligi kuu na ligi daraja la kwanza msimu mpya
wakati zikisubiri ratiba kutangazwa”, alionmgeza Osiah
No comments:
Post a Comment