Friday, August 3, 2012

NGASSA ATAMBULISHWA RASMI SIMBA AKABIDHIWA JEZI NAMBA 16, AAHIDI MATAJI MSIMBAZ

Kaburu akimkabidhi Ngassa jezi




Ngassa akiwasili kama unavyoona umati unamlaki


Kaburu akizungumza, kushoto Ngassa


Meneja Vifaa wa Simba SC, Kessy Rajab akiwa nyuma ya Ngassa


Ngassa


Ngassa


Ngassa


Waandishi, Asha Kigundula na Dina Ismail kulia


Mwandishi Somoe Ng'itu


Ngassa anavaa jezi


Imempendezaje?


M16 wa Msimbazi


TABASAMU; Kijana anafurahia maisha mapya


KARIBU SANA; Kaburu akipeana mikono na Ngassa baada ya kusaini


Kaburu akimuangalia Ngassa wakati anazungumza


MISHA POPOTE; Ngassa leo yuko Simba


AAHIDI MATAJI; Anasema anataka kushinda mataji na Simba
Na Mahmoud Zubeiry
MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Iric Nyange ‘Kaburu’, majira ya saa 5:00 asubuhi ya leo, amemtambulisha kiungo mshambuliaji mpya wa klabu hiyo, Mrisho Khalfan Ngassa ambaye alisajiliwa rasmi jana kwa dau la jumla la Sh. Milioni 55, kutoka klabu ya Azam FC, akisaini mkataba wa miaka miwili.
Ngassa alipokewa kwa shangwe makao makuu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo, na kuingizwa kwenye ukumbi wa mikutano kutambulishwa rasmi. Tendo bila kuchelewa, katika ukumbi uliosheheni Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, ‘Mr Liverpool’, Ezekiel Kamwaga, Ofisa Habari wa Simba SC alimkaribisha Nyange Kaburu amtambulishe Ngassa.
Pamoja na kuzungumzia Mkutano Mkuu wa Simba, utakaofanyika Jumapili katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, Kaburu alimtambulisha Ngassa na kumkabidhi jezi namba 16, ambayo alikuwa anaivaa Azam.
Ngassa alisema kwamba anashukuru kwa mapokezi mazuri Simba SC, yamemfariji na sasa wana Simba wasubiri kulipwa fadhila zao. “Naamini tu nitafanya vizuri katika klabu hii, kushinda mataji na Simba ndio ndoto zangu, namshukuru Mungu. Hii ni klabu kubwa, klabu ambayo hata baba yangu aliichezea,”alisema Ngassa.
Simba ilifanikiwa kumalizana na Ngassa jana na kusaini naye mkataba wa miaka miwili, ambao umemfanya aondoke na zaidi ya Sh. Milioni 35, Milioni 12 akipewa taslimu na nyingine akipewa gari (Milioni 18), wakati mpenzi mwingine wa Simba amemuongezea Milioni 5.
Katika mkataba huo wa Simba na Ngassa, mshambuliaji huyo atakuwa akilipwa Sh. Milioni 2 mshahara kwa mwezi, Milioni 1 ipo kwenye fomu ya mkataba na Milioni 1 atakuwa akiongezewa na mtu.
Usajili wa mchezaji huyo, ulikakamilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Hans Pop, ambaye ndiye alitoa fedha hizo na baada ya kumsainisha na kumkabidhi haki yake, ili kumuondolea usumbufu akambadilishia ‘chipu’ ya simu, ili akina Seif Magari wasimpate.
Juzi Simba ilimnunua Ngassa kutoka Azam kwa Sh. Milioni 25, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Yanga akagoma kwa sababu hakushirikishwa katika dili hilo.
Kwa kumuongeza ‘kifurushi’ cha Sh. Milioni 35, ina maana Simba imemsajili Ngassa kwa Sh. Milioni 60 kwa miaka miwili, ambalo ni dau kubwa zaidi la usajili kwa mchezaji huyo tangu aanze kucheza soka.
Yanga ilimsaini kwa Sh. Milioni 25 jumla kutoka Kagera Sugar mwaka 2007 pamoja na uhamisho wake akasaini mkataba wa miaka mitatu, wakati miaka miwili iliyopita, Azam ilimsajili kwa Sh. Milioni 55 pamoja na uhamisho wake (Sh. Milioni 30) ikimsainisha mkataba wa miaka mitatu, ambao ulitarajiwa kumalizika mwakani.
Azam ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya mchezaji huyo iliyemsajili kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya Yanga baada ya kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Na uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo.

No comments: