Sunday, July 29, 2012

COASTAL UNION YAMSAJILI RASMI JERRY SANTO ALIYEWAHI KUCHEZA SIMBA

Klabu ya Coastal Union jana imetangaza rasmi usajili wa kiungo wa kimataifa wa Kenya Jerry Santo, ambaye msimu wa 2010-2011 alikuwa mmoja ya viungo bora wa klabu bingwa ya soka ya Tanzania klabu ya Simba.

Santo ambaye aliondoka Simba kwa madhumuni ya kwenda kucheza soka nchini Albania kabla ya mambo kumuendea sivyo na kurudi Tusker ya Kenya. Amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga.

Kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa facebook wa klabu ya Coastal mchezaji huyo anakuwa wa mwisho katika usajili wa mwaka huu.

TSC MWANZA YAENDELEA KUFANYA VIZURI KWENYE ZIARA YAKE NCHINI UJERUMANI - YATINGA NUSU KOMBE LA FALLERHOF

TSC Mwanza.

Timu ya soka ya kituo cha TSC Mwanza imeendelea kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali inayoshiriki hapa nchini Ujerumani baada ya kuweza kutinga nusu fainali ya kombe la Fallerhof inayoshirikisha timu sita.
Stuttgart Kickers
TSC walipangwa kundi A, ambalo lilikuwa na timu kama VFL Bochum, Stuttgarter Kickers na wao TSC. Kwenye mchezo wa kwanza walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Kickers, goli la TSC likifungwa na Said Ndemla, na mechi ya pili wakatoka sare ya 0-0 na VFL Bochum.

VFL Bochum
Kwa matokeo hayo ikishika nafasi ya pili kwenye kundi na kufanikiwa kuingia nusu fainali na leo watacheza dhidi ya FC Freiburg.

Fc Freiburg

 

No comments: