Rais wa Mazembe, Moise Katumbi |
Na
Prince Akbar
MAKAMU wa
Rais wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mohamed
Kamwanya amesema kwamba Thomas Emmanuel Ulimwengu anachelewa kuingizwa kwenye
kikosi cha kwanza kwa sababu kiwango chake bado.
Thomas Ulimwengu |
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Lubumbashi jana, Kamwanya alisema
kwamba, Ulimwengu kila anapopewa ruhusa ya kurejea Tanzania kujiunga na timu za
taifa, kwanza huchelewa kurudi Lubumbashi na pia hurudi akiwa hayuko
fiti.
“Hicho ndio
kinamchelewesha, lakini kama siyo hivyo angekuwa anacheza tu kama mwenzake. Na
nyinyi watu wa vyombo vya habari mtusaidie, kwa sababu wachezaji wakija huko
wanafanya anasa, wanarudi huku hawako fiti, sasa inakuwa mbaya,”alisema
Kamwanya.
Akiwa
anaingia msimu wa pili tangu asajiliwe na Mazembe, lakini Ulimwengu bado yupo
kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba wa timu hiyo na hachezi Ligi Kuu wala Ligi
ya Mabingwa, kama mwenzake Mbwana Ally Samatta ambaye
anang’ara.
Akimzungumzia
Samatta juu ya habari kwamba kuna klabu zinamataka Ulaya, Kamwanya alisema
kwamba hadi sasa Mazembe haijapokea ofa yoyote kutoka kwa wakala au klabu na
hawawezi kujadili mambo yanayozungumzwa au kuandikwa kama
tetesi.
“Tutakuwa
tayari kusema, iwapo tutapata ofa ya maandishi, lakini kwa sasa tunasema Samatta
tupo naye tu ni mchezaji wetu tegemeo,”alisema Kamwanya.
Saturday, July 28, 2012
KIUNGO WA NGUVU LA LIGA ATUA ARSENAL
Tetesi za Jumapili magazeti Ulaya
NEWCASTLE YAMRUDIA ANDY CARROLL
KLABU ya Newcastle
itarefufua nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll baada
ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kusema ataondoka Anfield ili apate furaa
ya kucheza michuano ya Ulaya.
Lakini
Newcastle itamrejea mshambuliaji wake huyo wa zamni iwapo tu itamuuza
mshambuliaji wake mwenye thamani ya pauni Milioni 7, Demba Ba, 27.
KLABU
ya Arsenal inatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 15 wa kiungo wa
Malaga, Santi Cazorla, mwenye umri wa miaka 27 Jumanne.
KOCHA
wa Manchester City, Roberto Mancini anaamini mabingwa wa Ligi Kuu watatangaza
wachezaji wao wapya, iliyowasajili muda si mrefu ujao.
KOCHA
wa West Brom, Steve Clarke amethibitisha kwamba mshambuliaji Shane Long, mwenye
umri wa miaka 25, hauzwi, baada ya Reading kuonyesha nia ya
kumsajili.
KLABU
ya Fulham iko tayari kuomba kumsajili kiungo wa kimataifa wa Urusi, anayechezea
Arsenal, Andrey Arshavin, mwenye umri wa miaka 31, ambaye inaaminika anataka
kubaki London.
KLABU
ya Manchester City inaweza kumkosa mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie,
mwenye umri wa miaka 28, bdaada ya kiongozi wake, Brian Marwood kughairi
kumfanya awe mchezaji ghali katika klabu hiyo.
WAKALA
aliyefanikisha mpango wa mshambuliaji Emmanuel Adebayor kutoka Arsenal kwenda
Manchester City anaamini mshambuliaji huyo hapendi kuhamia to Tottenham.
SCHOLES ALIKUWA TAYARI KURUDI ENGLAND
KIUNGO
wa Manchester United, Paul Scholes angeweza kurejea kwenye kikosi cha England
kilichocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, lakini hakupigiwa simu na
kocha wa timu hiyo, Roy Hodgson.
VERMAELEN AZINGUANA NA REFA...
NYOTA
wa Arsenal, Thomas Vermaelen alizinguana na refa msaidizi, Sian Massey katika
mechi ambayo timu yake ilifungwa 2-0 na Manchester City mjin Beijing,
China.
NGORONGORO NA NIGERIA LEO TAIFA BONGE LA GAME
Kikosi cha Ngorongoro cha mwaka juzi |
Na Prince
Akbar
TIMU ya soka
ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo inashuka
dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na vijana wenzao wa
Nigeria, Flying Eagles katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili kuwania kucheza
Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika mwakani nchini
Algeria.
Kocha Mkuu
wa Ngorongoro Heroes, Menmark Jakob Michelsen na Nahodha wa timu hiyo, kiungo
Omega Seme wamesema timu yao iko tayari kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na
waamuzi kutoka Kenya.
Michelsen
amesema timu yake imepata mechi mbili za kujipima nguvu dhidi ya Rwanda, lakini
pia aliishuhudia Flying Eagles ikicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young
Amavubi) uliofanyika Julai 24 mwaka huu jijini Kigali.
“Timu iko
vizuri na wachezaji kama Frank Domayo, Simon Msuva na Ramadhan Singano ambao pia
wanachezea timu A (Taifa Stars), hivyo uzoefu wao ni muhimu kwa mechi ya
kesho.
“Nigeria ni
mabingwa watetezi wa michuano hii kwa hiyo tunatarajia upinzani mkubwa, lakini
tumejiandaa kwa hilo. Nigeria ni nchi yenye mfumo mzuri wa timu za vijana, na
sisi tunaelekea huko huko” amesema Michelsen.
Kwa upande
wake, Kocha Mkuu wa Flying Eagles, John Obuh amesema haijui vizuri Ngorongoro
Heroes lakini anaiheshimu kutokana na ukweli kuwa inacheza raundi ya pili baada
ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.
“Sina
mchezaji yeyote anayecheza mpira wa kulipwa nje ya Nigeria, lakini tumekuja
kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza raundi ya mwisho na
hatimaye tucheze fainali mwakani,” amesema Obuh aliyefuatana na nahodha wake
Samuel Okan ambaye ni mlinda mlango.
Katika mechi
hiyo, itakayochezeshwa na refa Moses Osano, akisaidiwa na Peter Keireni na Elias
Wamalwa, Thomas Onyango mezani, viingilio vitakuwa Sh. 3,000 kwa viti vya rangi
ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa
VIP A ni sh. 10,000.
Osano
atasaidiwa na Peter Keireini na
HESHIMA IMERUDI DAR YOUNG AFRICANS AKA YANGA
Yanga wakishangilia mwali wao wa Kagame |
Na Mahmoud
Zubeiry
MICHUANO ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame imefikia tamati jana
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa klabu ya Yanga, kufanikiwa kutetea taji lao,
baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0.
Shukrani
kwao Hamisi Kiiza Diego na Said Bahanuzi, wafungaji wa mabao hayo moja kila
kipindi na sasa Yanga inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, inaingia
kwenye orodha ya mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, kwa kutwaa taji hilo
mara tano.
Yanga sasa
imebakiza mara moja kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba (1974,
1991, 1992, 1995, 1996 na 2002) kutwaa Kombe hilo, mara tano kwa sita. Yanga
ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.
Kiiza
alifunga bao lake, baada ya kuuwahi mpira aliokuwa anarudishiwa kipa Deo Munishi
‘Dida’ na beki Said Mourad na kumpiga chenga kipa huyo kisha kuusukuma mpira
nyavuni.
Bahanuzi
aliuwahi mpira mrefu uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa
Azam kabla ya kumtungua Dida.
Mechi hiyo
ilichezeshwa vema na refa Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi, aliyekuwa
akisaidiwa na Simba Honore wa Rwanda na Peter Sabatia wa
Kenya.
Katika
mchezo huo kikosi kilichoweka historia ya Kombe la tano la Kagame, Yanga SC
kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo/Juma Seif
‘Kijiko’, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende.
Azam FC; Deo
Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris,
Jabir Aziz, Kipre Tcheche/Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’,
Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’. Benchi; Mwadini Ally, Samir Haji
Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha ‘Vialli’ na
Gaudence Mwaikimba.
Katika
mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na Magola
Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika ya 67, wakati la kufutia machozi
la timu ya jeshi la Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya 89.
Ikumbukwe,
Yanga ilikaribishwa kwenye michuano ya mwaka huu na kipigo cha 2-0 kutoka kwa
Atletico ya Burundi katika Kundi C, kabla ya kushinda 7-1 dhidi ya Waw Salaam ya
Sudan Kusini, na 2-0 dhidi ya APR ya Rwanda, ilishinda kwa penalti 5-3 dhidi ya
Mafunzo katika Robo Fainali, kufuatia sare ya 1-1 na ikashinda 1-0 dhidi ya APR
katika Nusu Fainali ndani ya dakika 120.
Michuano
hii, imemuibua kinara mpya wa mabao Yanga, Said Bahanuzi ‘Spider Man’, ambaye
katika mabao 13 iliyofunga Yanga hadi sasa kwenye michuano ya mwaka huu, yeye
amefunga sita, mengine matano Hamisi Kiiza ‘Diego’ na mengine mawili, moja
Stefano Mwasyika na lingine Nizar Khalfan.
Mafanikio
haya yanajuka wiki mbili tu tangu Yanga ipate viongozi wapya, Mwenyekiti Yussuf
Manji, Makamu wake Clement Sanga na Wajumbe Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro,
Aaron Nyanda na George Manyama.
Yanga pia
inajivunia udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake,
Kilimanjaro Premeum Lager, ambao ni wa kwanza tangu wapoteze udhamini wa kampuni
ya Shivacom.
Ikumbukwe,
Kilimanjaro Premium Lager ilianza kuidhamini Yanga Agosti 18, mwaka 2008, katika
mkataba uliosainiwa kwenye hoteli ya Movenpick (sasa Serena), mjini Dar es
Salaam.
Kilimanjaro
Premium Lager, ambao ni wadhamini wakuu wa wapinzani wa jadi wa Yanga, Simba SC,
imekuwa ikihakikisha udhamini wake unafika maeneo yote muhimu katika shughuli za
uendeshwaji wa klabu.
Na
inaaminika udhamini huo ndiyo chachu ya mafanikio ya miaka ya kmaribuni ya klabu
hiyo, ikiwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu katika kipindi cha miaka
mitano (2008, 2009 na 2011) sambamba na ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame mwaka jana na mwaka huu.
ILIVYOTWAA
KOMBE MWAKA 2011:
Yanga
ilifanikiwa kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama
Kombe la Kagame, 2011 baada ya kuifunga Simba bao 1-0, katika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Shukrani
kwake mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Kenneth Asamoah aliyefunga bao hilo,
pekee dakika ya 108, akiunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa kitaalamu na
kiungo Rashid Gumbo.
Kabla ya
taji hilo walilotwaa Jumapili sambamba na dola za Kimarekani 30, 000, sawa na
Sh. Milioni 45 za Tanzania, Yanga walitwaa tena Kombe hilo kwa mara ya kwanza
mwaka 1975 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, wakiifunga Simba mabao 2-0 na
baadaye mara mbili mjini Kampala, Uganda mwaka 1993 na 1999, mara zote
wakiifunga SC Villa ya huko.
Ulikuwa
mchezo mgumu ambao ulidumu kwa dakika 120, timu zikionyesha kucheza tahadhari,
kabla ya Asamoah kumaliza kazi.
Kikosi
kilichoipa Yanga kombe la nne la Kagame kilikuwa; Yaw Berko, Nsajigwa Shadrack,
Oscar Joshua, Chacha Marwa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Seif ‘Kijiko’/Rashid
Gumbo, Godfrey Taita/Julius Mrope, Nurdin Bakari, Davies Mwape, Jerry
Tegete/Kenneth Asamoah na Hamisi Kiiza.
Yanga
iliyokuwa Kundi B la michuano ya mwaka huu, ilifuzu kama kinara wa kundi baada
ya kujikusanyia pointi saba kutokana na kushinda mechi mbili na kutoka sare
moja.
Katika Robo
Fainali, Yanga ilikutana na Red Sea ya Eritrea na kushinda kwa penalti 6-5,
kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo
huo.
Katika Nusu
Fainali, Yanga ilikutana na St George ya Ethiopia na kushinda tena kwa penalti
5-4, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120, kabla ya kuiteketeza
Simba SC katika fainali.
Ikumbukwe
katika michuano ya mwaka huu, Yanga iliingia kama ‘viti maalumu’, kwani Simba SC
ndio walikuwa wawakilishi halisi kama mabingwa wa Bara.
Ili
kushiriki mashindano ya mwaka huu, ilibidi Yanga wailipe CECAFA dola za
Kimarekani 20,000 kama faini ya kugomea mechi ya mshindi wa tatu wa michuano
hiyo, mwaka 2008 mjini Dar es Salaam.
Yanga
ilitakiwa kucheza na Simba mwaka huo kuwania nafasi ya tatu, ikiwa chini ya
Mwenyekiti aliyekuwa na misimamo mikali, Wakili Imani Omar Madega, Yanga iligoma
kwa sababu hawakukubaliana na TFF juu ya mgawanyo wa mapato ya milangoni.
ZANZIBAR
MWAKA 1975:
Iliingia
kama bingwa wa Tanzania baada ya kuifunga Simba SC katika fainali ya Ligi mwaka
1974 Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, wakati watani wao hao waliingia kama mabingwa
watetezi wa michuano.
Yanga
ilipangwa Kundi B pamoja na Express ya Uganda na Mufulira Wanderers ya Zambia.
Yanga ilianza kwa kuifunga Express FC mabao 4-0 na baadaye kutoka sare ya 1-1 na
Mufulira, hivyo kuongoza Kundi hilo na kukata tiketi ya kuingia Nusu
Fainali.
Katika Nusu
Fainali, Yanga iliifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 na kukata tiketi ya
kuingia fainali Janauri 13, mwaka huo ilipokutana na watani wao wa jadi, Simba
SC.
Mabao ya
Sunday Manara ‘Computer’ na Gibson Sembuli (sasa marehemu) yaliipa Yanga ushindi
wa 2-0 na taji la kwanza la michuano hiyo.
KAMPALA,
UGANDA MWAKA 1993:
Ilikwenda
kama bingwa wa Bara na watano wao, Simba walikwenda kama watetezi wa taji na
huko Yanga walipangwa Kundi A pamoja na wenyeji SC Villa na Malindi ya Zanzibar.
Katika
mchezo wa kwanza, Yanga ilifungwa 3-1 na Villa, siku hiyo kabla ya kuibuka na
kuifunga Malindi mabao 2-1, yote yakitiwa kimiani na Said Nassor Mwamba
‘Kizota’, sasa marehemu, hivyo kukata tiketi ya kuingia Nusu Fainali.
Katika Nusu
Fainali, Yanga ilikutana na Express FC na kushinda mabao 3-1, hivyo kutinga
fainali ambako ilikutana tena na SC Villa.
Kwa
kuzingatia matokeo ya mchezo wa awali kwenye Kundi A, Yanga haikupewa nafasi
kabisa ya kufurukuta mbele ya SC Villa, lakini mambo yalikuwa tofauti, mabao ya
Said Mwamba na Edibily Lunyamila, yaliipa timu hiyo ushindi wa 2-1 pamoja na
taji la pili la michuano hiyo.
Marehemu
Kizota aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.
KAMPALA,
UGANDA MWAKA 1999:
Ilikwenda
kama bingwa wa Bara, ikiwa mwakilishi pekee na ilitua huko, huku mashabiki wengi
wa soka Uganda wakiwa na kumbukumbu ya kile kilichofanywa na klabu hiyo mwaka
1993.
Timu
zilizoshiriki michuano hiyo ni Vital'O ya Burundi, Mebrat Hail ya Ethiopia, AFC
Leopards ya Kenya, Kiyovu Sport, Rayon Sport za Rwanda,
Naadiga
Dekedaha ya Somalia, KMKM ya Zanzibar, Al Hilal ya Sudan, Yanga, wenyeji
Express na SC Villa za Uganda wakati Red Sea ya Eritrea ilijitoa dakika za
mwishoni.
Kwa matokeo
hayo, Kundi D ilimokuwa Yanga lilibakiwa na timu mbili tu, yaani mabingwa hao wa
Bara na mabingwa watetezi.
Mechi ya
kwanza, Yanga ilifungwa 3-0 na Rayon Januari 4 na ziliporudiana siku mbili
baadaye, Yanga walilipa kisasi kwa ushindi wa 3-0 pia, mabao
ya
Sekilojo
Chambua dakika ya 23 na 57 na Kali Ongala dakika ya 59.
Katika Robo
Fanali, Yanga ilikutana na Al Hilal Januari 10 na kushinda mabao 2-1, wafungaji
Salvatory Edward dakika ya 14 na Edibily Lunyamila dakika ya 89 kwa
penalti.
Katika Nusu
Fainali, Yanga ilikutana na Vital’O ya Burundi Januari 13 na kushinda mabao 3-2,
wafungaji Kally Ongara dakika ya 16, Bakari Malima dakika ya 78 na Said Mhando
dakika ya 90.
Hivyo kwa
mara ya pili, Yanga ilikutana na SC Villa kwenye fainali kukumbushia vitu vya
mwaka 1993 na safari hii mambo yalikuwa mazito zaidi, kwani dakika 120
zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 Lunyamila akiisawazishia Yanga
dakika ya 42, baada ya Hassan Mubiru kutangulia kufunga dakika ya saba tu ya
mchezo huo.
Mchezo
ukahamia kwenye mikwaju ya penalti na Manyika Peter akaingia kwenye orodha ya
makipa hodari wa kupangua penalti baada ya kupangua mikwaju miwili, Yanga
ikishinda kwa penalti 4-1, Uwanja wa Nakivubo.
Hivyo ndivyo
Yanga ilivyotwaa mataji yake matano ya Kombe la Kagame. Je, watawafikia
wapinzani wa Simba mwakani? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na
kuona.
Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji akisalimiana na Ngassa |
No comments:
Post a Comment