POLISI Morogoro imeibamiza Coastal Union ya Tanga
1-0,. kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Bao hilo pekee, lilitiewa kimiani
Mokili Rambo dakika ta 80.
Mechi hiyo
ilikuwa ni maalum kwa timu zote kuvipima vikosi vyake kabla ya kuanza kwa msimu
mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bata.
Katika
mchezo huo, vikosi vilikuwa: Polisi Moro; Said Manzi,Nahoda Bakary,John
Bosco,Hamisi Mamiwa, Abdallah Rajab,Salmin Kiss, Admin Bantu, Pascal Maige,
Abdallah Juma, Mokili Rambo na Keneth Masumbuko
Coastal union; Jackson
Chove,Mbwana Bakary, Juma Jabu, Jama Macheranga, Philip Metusela, Hamisi Shengo,
Pius Kisambile, Razak Khalfan, Nsa Job, Suleiman Kassim 'Selembe' na Atupele
Green.
Kikosi cha timu Coastal Union
kilichoanza
Kikosi Polisi kilichoanza
Kipute
Kipute
Kipa wa Polisi, Saidi Manzi akiokoa moja ya hatari
langoni mwake
Suleiman 'Salembe' akitafuta mbinu za kuwatoka
Polisi
AZAM YAUA 8-0, SALAMU ZAO SIMBA SC
![]() |
John Bocco 'Adebayor' amefunga mawili leo Chamazi |
Na Mahmoud
Zubeiry
KATIKA
kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara, Azam FC leo wameichapa mabao 8-0 Transit Camp kwenye Uwanja wa Chamazi,
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo wa upande mmoja, Azam ikitawala zaidi, mabao yap yalitiwa kimiani na
Gaudence Mwaikimba, John Bocco ‘Adebayor’ na Papie, mshambujliaji aliye
majaribio kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kila mmoja mabao mawili,
wakati Kipre Herman Tcheche na Abdulhalim Humud kila mmoja alifunga bao moja.
Azam ambayo
ipo chini ya kocha mpya, Mserbia Boris Bunjak, inatarajiwa kuivaa Simba katika
mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Septemba 8, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam..
Kuchelewa
kwa mechi hiyo ambako kumeenda sambamba na kuchelewa kuanza kwa ligi hiyo,
kumetokana na kuchelewa kufikiwa mwafaka mapema wa mkataba mpya wa udhamini wa
Ligi Kuu.
Mkataba wa
awali wa Vodacom na TFF unafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu na kusainiwa
mkataba mwingine, baada ya majadiliano
yanayoendelea.
Lakini kwa
kuwa Mkutano Mkuu wa TFF uliopita uliridhia kuanzia msimu ujao Ligi Kuu
iendeshwe na kampuni itakayoundwa na klabu za Ligi Kuu mjadala kuhusu udhamini
mpya wa ligi umekuwa mrefu kutokana na kuhusisha pande tatu, klabu, wadhamini na
shirikisho.
Lakini sasa,
kwa vyovyote, hata maridhiano ya mkataba mpya wa udhamini na Vodacom yachelewe
tena, mechi hiyo itachezwa Septemba 8, ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa
Ligi Kuu.
Kihistoria
hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili
kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na
Yanga.
Mtibwa
ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na
kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado
inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager,
ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi
hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga
tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao
ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0.
Wakati huo
huo: Jana kikosi cha pili cha Azam, Azam Academy kililazimisha sare ya bila
kufungana (0-0) na Prisons ya Mbeya, iliyorejea Ligi Kuu, kwenye Uwanja huo huo
wa Chamazi.
Source:Bin Zubeiry
No comments:
Post a Comment