Rage ambaye pia ni Mwenyekiti
wa klabu ya Simba alimuandikia Rais Tenga barua ya kujiuzulu wadhifa huo kwa
kile alichosema ‘kamati hiyo kushindwa kwa makusudi kusimamia sheria na kanuni
za uendeshaji wa mpira Tanzania zinavyoeleza.’
Amekataa ombi hilo kwa
maelezo kuwa kama Rage amehisi kuwepo udhaifu wa kutosimamia sheria na kanuni
kama inavyotakiwa, ni vyema akaendelea kuwemo kwenye kamati hiyo ili kuisaidia
kusimamia sheria na kanuni hizo kama inavyotakiwa badala ya
kujiuzulu.
“Kutokana na uzoefu na uwezo
ambao Rage anao katika uongozi wa mpira wa miguu, ni vyema akautumia kuisaidia
kamati kutekeleza wajibu wake kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria ili
kusaidia kusukuma mbele gurudumu za maendeleo ya mpira wa miguu,” amesema Rais
Tenga.
Pia Rais Tenga amesisitiza
kuwa ni muhimu kwa mpira wa miguu kuongozwa kwa kufuata sheria na kanuni
zilizopo, rai ambayo imetoa kwa kamati zote za TFF ili kuhakikisha kuwa mpira wa
miguu unaongozwa bila kuonea wala kupendelea upande wowote.
Rais Tenga amesisitiza kuwa
kamati hazina budi kuchukua hatua zinazostahili bila woga pale kanuni zinapotaka
hatua kuchukuliwa. Amezitaka kamati zisisite kwa namna yoyote ile kuchukua hatua
kwa vile kwa kufanya hivyo, uwezekano wa kutokea upendeleo au uonevu utapungua,
hivyo mpira wa miguu kuongozwa kwa sheria na haki.
No comments:
Post a Comment