Monday, July 23, 2012

YANGA WAANGUSHA PATI LA USIKU TAIFA

 


Jerry Tegete kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakimpongeza Chuji- nyuma nyuma ni Bahanuzi 'Spider Man'


Benchi Yanga likiomba dua wakati Chuji anakwenda kupiga penalti ya mwisho

Said Bahanuzi 'Spider Man''

Mmanga akiwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu

Hapa ni mara tu baada ya kuanguka akisaidiwa kwa kupepewa na wenzake
YANGA imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wawakilishi wa Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yanga wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala, lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
Katika mchezo huo, Juma Othman Mmanga alipoteza fahamu na kuwaweka roho juu wachezaji wenzake na mashabiki, akatolewa nje akipepewa na hakuweza kuendelea na mchezo, lakini taarifa za baada ya mchezo zilisema anaendelea vizuri.
Kipa wa Yanga Berko aliumia dakika ya 69 na akatibiwa kwa dakika tatu, kabla ya kutolewa nje dakika ya 72, nafasi yake ikichukuliwa na Ally Mustafa Barthez ambaye ukaaji wake mazuri langoni wakati wa penalti ulimfanya Said Mussa Shaaban wa Mafunzo akapiga nje na kuipa Yanga ushindi.
Saidi Bahanuzi alipiga penalti ya kwanza, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ya pili, Hamisi Kiiza ya tatu, ya nne Haruna Niyonzima na Athumani Iddi ‘Chuji’ alipiga ya mwisho na kuwainua maelfu ya mashabiki wa Yanga Uwanja wa Taifa.
Yanga SC; Yaw Berko/Ally Mustafa, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika/Idrissa Assenga, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo/Jerry Tegete.
Mafunzo; Khalid Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour/Hajji Abdi Hassan, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga/Sadik Habib Rajab, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim/Kheir Salum Kheir na Ally Juma Hassan.
 

BALL BOY 'AKIPIGA MZIGO' TAIFA

Kijana muokota mipira katika mechi ya leo ya Kombe la Kagame, kati ya Yanga na Mafunzi, akiwa ameuchapa usingizi, nadhani kutokana na kuzidiwa na sauwm, nyuma ya lango la Mafonzo cha kwanza.


NI YANGA NA APR TENA NUSU FAINALI

MAHADHI MPYA; Kipa wa Mafunzo, Halid Mahadhi Haji akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi

Yanga


Mafunzo
YANGA imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-4, kufuatia sare bya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wawakilishi wa Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yangab wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala, lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo.
Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shamte Ally, Ladislaus Mbogo, Godfrey Taita, Juma Seif ‘Kijiko’, Jerry Tegete na Idrisa Rashid.
Mafunzo; Khalid Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim na Ally Juma Hassan.
Benchi; Salum Mohamed Pangani, Hajji Abdi Hassan, Kheir Salum Kheir, Sadik Habib Rajab na Thabit Mohamed Abdallah.

MECHI YA KWANZA....
Wachezaji wa APR wakimpongeza Ndikumana, aliyeinua vidole juu kushoto kwa kufunga bao la pili

Dan Wagaluka wa URA kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa APR kulia

 

MILIONEA WA KIARABU AWAPA SIMBA UZI MKALI WA BEI MBAYA


Wachezaji wa Simba muda si mrefu wataanza kung'aa na uzi mpya wa maana pigo za Man City

Na Princess Asia
KLABU ya soka ya Simba jana imepokea msaada wa jezi, raba, viatu vya kuchezea mpira, mabegi na suti za michezo (tracksuit) – vyote vya kisasa kabisa, kutoka kwa familia ya Al Ruwahi. Msaada huo umetolewa kwa mapenzi mema ambayo familia hiyo inayo kwa klabu.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mahusiano baina ya familia ya Al Ruwahi (Ruwehi) na Simba yamedumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
Amesema takribani miaka 30 iliyopita, familia hiihii ilitoa zawadi ya basi (Nissan Coaster) kwa Simba na kuifanya klabu yetu kuwa ya kwanza nchini kumiliki basi lake yenyewe.
Amesema msaada huo wa sasa kwa Simba una thamani ya Sh milioni 18 kwa ujumla wake na Simba sasa itavaa jezi hizo katika pambano lake la kesho dhidi ya Azam katika michuano ya Kombe la Kagame.
Amesema klabu ya soka ya Simba inatumia nafasi hii kuwakaribisha wapenzi na wanachama wake kujitokeza kuisaidia klabu kwa namna yoyote ile, kama ilivyofanya familia hii ya Al Ruwahi, ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya klabu.
"Simba ni ya kila mmoja na haina mwenyewe. Umoja na mshikamano baina ya viongozi, wadhamini, wapenzi na wanachama wake, ndiyo utakaoifanya izidi kuwa bora hapa nchini na nje ya mipaka ya taifa letu,"alisema Kamwaga maarufu kama Mr. Liverpool.
Wakati huo huo: Kamwaga amesema hali za wachezaji wa timu hiyo waliopo kambini katika hoteli ya Vina, Mabibo mjini Dar es Salaam zinaendelea vizuri tayari kwa mechi ya Robo Fainali, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kesho dhidi ya Azam. Amesema hadi sasa majeruhi ni mmoja tu, Amir Maftah na Abdallah Juma 'Dullah Mabao' amefanyiwa vipimo jana na majibu yake yanatolewa baadaye leo.
Amesema kwa mujibu wa kanuni za mashindano haya, wachezaji wote waliokuwa na kadi moja ya njano kwenye hatua ya makundi wamefutiwa kadi zao na hivyo Simba itaingia uwanjani kesho Jumanne kwenye pambano dhidi ya Azam ikiwa haina mchezaji mwenye adhabu.
Simba imesifiwa na CECAFA kuwa ni miongoni mwa timu zenye nidhamu nzuri kwenye michuano ya Kagame mwaka huu, mfano ukitolewa kwenye pambano lake dhidi ya AS VITA ya DR Congo, ambapo hakukuwapo na kadi yoyote iliyotolewa mechi nzima.

No comments: