Monday, July 23, 2012

HATIMAYE MAN UNITED YAMNASA LUCAS MOURA KWA PAUNI MILIONI 26


Gossip logo
22 July 2012Last updated at 22:39 GMT

Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya


HATIMAYE MAN UNITED YAMNASA LUCAS MOURA KWA PAUNI MILIONI 26


KLABU ya Manchester United imekubali kutoa dau la pauni Milioni 26 kuinunua saini ya kinda Mbrazil, Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Sao Paulo.
Lucas Moura
Moura yuko na Brazil kwenye Olimpiki ya London 2012.
MAN United pia iko tayari kumsajili nyota wa Fulham, Moussa Dembele, mwenye umri wa miaka 25.
KLABU ya Arsenal inataka mshambuliaji wake anayetaka kuhama, Robin van Persie adai pauni Milioni 10.1 kwa mwaka, iwe Manchester United, City au Juventus ambazo zote zinamtaka Mholanzi huyo.
KLABU ya Manchester City imetega mitego yake kwa Daniele De Rossi, mwenye umri wa miaka 28, kwa mara nyingine tena baada ya kushindwa kumpata Mtaliano huyo msimu uliopita.
KLABU ya Tottenham anamtaka mshambuliaji wa AS Roma, Marco Borriello, mwenye umri wa miaka 30, baada ya kuambiwa hawana nafasi ya kumsajili nyota wa Atletico Madrid, Adrian Lopez.
Luka Modric
Modric anataka kuhamia Real Madrid
MCHEZAJI mwenye mkataba na Blackburn Rovers, Junior Hoilett hatajiunga na Queens Park Rangers, vinginevyo klabu hiyo ya London ilipe dau la pauni Milioni 6 au pendekezo la kubadilishana na Jamie Mackie.
KLABU mpya katika Ligi Kuu ya England, Southampton inataka kumsajili beki wa Blackburn, Scott Dann, mwenye umri wa miaka 25.
KLABU ya Fulham imempata kwa mkopo wa muda mrefu mshambuliaji wa Chelsea mwenye thamani ya pauni Milioni 18, Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 19.
KLABU ya Crystal Palace inaweza kuendelea kuboresha kikosi chake kwa kumsajili mshambuliaji wa KIfaransa, Alexis Allart,mwenye umri wa miaka 25, ambaye atawagharimu pauni 300,000

AVB AKERWA NA MODRIC

KOCHA wa Tottenham, Andre Villas-Boas amekerwa na kitendo cha kiungo anayetaka kuhama klabu hiyo, Luka Modric raia wa Croatia kutoonekana mazoezini .
MWENYEKITI mwenye hasira kali nwa Spurs, Daniel Levy anaweza kuzuia uhamisho wowote wa Luca Modric baada ya mchezaji hujyo kutoonekana mazoezini mwishoni mwa wiki na atamtoza faini mchezaji huyo kwa mara ya tatu ndani ya siku nne ikiwa atashindwa kuhudhuria mazoezi na leo.

BALOTELLI ANAKUFURU JAMANI..

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli, mwenye umri wa miaka 21, amevunja rekodi ya matumizi kwa jinsi anavyotumia katika holiday yake huko Ibiza na kulipa 'bill' kubwa kubwa.
 

YANGA WASAKA NUSU FAINALI LEO


Kikosi cha Yanga kilichoipiga APR 2-0

Na Prince Akbar
MABINGWA watetezi wa Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Yanga SC ya Dar es Salaam, leo wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na Mafunzo ya Zanzibar katika hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo.
Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet katika mchezo wa leo, atamkosa kiungo Nizar Khalfan ambaye anasumbuliwa na maradhi ya nyonga, wakati hali ya kinara wa mabao wa timu hiyo, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ hadi jana haikuwa ya kumpa uhakika wa kucheza mechi hiyo.
Bahanuzi anasumbuliwa na maumivu ya mgongo, wakat kiungo Nizar Khalfan yeye kwa asilimia 100 hatacheza kutokana na maumivu hayo ya nyonga.
Saintfiet aliiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, Nizar hatacheza kabisa, lakini wachezaji wengine watatu, Bahanuzi, kipa Yaw Berko anayesumbuliwa na goti, kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Hamisi Kiiza wanaosumbuliwa na quadriceps wako kwenye hatihati kucheza.
Mtakatifu Tom amesema kwamba, Daktari wa Yanga, Sufiani Juma anaendelea kufuatilia kwa karibu hali za Bahanuzi, Kiiza, Berko na Chuji ili kuhakikisha wanakuwa fiti kwa ajili ya mechi ya leo.
Amesema sababu ya wachezaji wake kuumia mara kwa mara ni kutokana na kucheza mechi mfululizo na kulingana na kanuni za mashindano hayo, hawezi kutumia wachezaji zaidi ya 20, hivyo hana namna nyingine zaidi ya kupambana na hali hiyo.
Bahanuzi ndiye kinara wa mabao wa Yanga hivi sasa, hadi sasa akiwa amekwishaifungia timu hiyo mabao manne, hivyo kuingia kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha mashindano hayo, ambayo tayari kwenye kabati la Yanga kuna mataji manne yamehifadhiwa.
Mshambuliaji huyo mpya kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, Ijumaa alikaribia kuondoka na mpira uwanjani, kama si refa Dennis Batte kutoka Uganda kukataa bao lake moja siku ambayo alifunga mawili yaliyokubaliwa dhidi ya APR ya Rwanda, Yanga ikishinda 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Katika mchezo huo, Kocha Tom alimpumzisha Bahanuzi dakika ya 72 na nafasi yake ikachukuliwa na Jerry Tegete, wakati Nizar Khalfan kabla ya hapo alimpisha Juma Seif ‘Kijiko’.
Matatizo ya mgongo kwa Spider Man
yalianzia kwenye mechi na APR
Mchezo kati ya Yanga na Mafunzo, utaanza saa 10:00 jioni na utatanguliwa na mechi nyingine ya Robo Fainali kati ya URA ya Uganda na APR ya Rwanda, wakati kesho Atletico Olympique Sport ya Burundi itamenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Robo ya Fainali ya tatu mchana, kabla ya Azam FC na Simba SC, zote za Dar es Salaam, kuhitimisha awamu ya Nane Bora ya michuano hiyo.
Michuano hii, iliyoanza Julai 14 na inatarajiwa kufikia tamati Julai 28, inadhaminiwa na Azam na SuperSport Televisheni.

RATIBA ROBO FAINALI
Julai 23, 2012
URA vs APR (Saa 8:00 mchana)
Mafunzo vs Yanga (Saa 10:00 jioni)
Julai 24, July
Atletico vs AS Vita (Saa 8:00 mchana)
Azam vs Simba SC (Saa 10:000 jioni)

WIKI MBILI KUAMUA HATIMA YA OKWI BUNDESLIGA


Okwi

Na Princess Asia
EMMANUEL Okwi, mshambuliaji wa Simba SC amepewa wiki mbili zaidi za kuendelea na majaribio katika klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Austria yenye maskani yake Wals-Siezenheim, nchini humo na baada ya hapo ndipo majibu yatatoka.
Katibu wa Simba Evodius Mtawala ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku kwamba, Okwi ambaye tayari yuko huko kwa wiki moja, hadi sasa anafanya vizuri ndio maana kapewa wiki mbili zaidi, ili kocha wa klabu hiyo ajiridhishe zaidi na kiwango cha Mganda huyo.
Klabu hiyo inayotumia Uwanja wa Red Bull Arena, ikiwa zaidi inafahamika kama SV Austria Salzburg kabla haijanunuliwa na kampuni ya Red Bull mwaka 2005, imewahi kufika Fainali ya Kombe la UEFA mwaka 1994 na inacheza Ligi Kuu ya Austria, iitwayo Bundesliga kama Ligi Kuu ya Ujerumani.
Timu hiyo ni kama timu ambayo Okwi, anachezea kwa sasa, Simba SC, kwani nayo inavaa jezi za rangi ya nyeupe na nyekundu na imewahi kutwaa taji la Bundesliga ya Austria mara saba na pia ilicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 1994–1995 kama Casino Salzburg, na kuwa timu pekee, ambayo haikufungwa na mabingwa wa wakati huo, Ajax Amsterdam.
Awali, Okwi aliikosesha Simba Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini na kuamua kwenda Austria, ambako inaelezwa klabu hiyo iko tayari kutoa Euro 600,000 akifuzu.
Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
Hata hivyo, Simba SC ilisema imeshindwa kumshawishi Okwi kwenda kucheza Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe anataka kucheza Ulaya tu. Wakala aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha ofa nyingine kutoka Mamelodi, ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni 2, lakini bado mabingwa hao wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda Ligi Kuu ya Afika Kusini (PSL).
 

MANJI NA JESHI LAKE LA MIAMVULI WAWAPA SUMU WACHEZAJI YANGA KUUA WAZENJI KESHO

Wapiganaji wa Yanga wakiteta kabla ya kuzungumza na wachezaji leo
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akiwaeleza jambo viongozi wenzake wa Yanga
Manji, Sanga, Katabalo na Bin Kleb wakijadiliana jambo kabla ya kuzungumza na wachezaji
Manji akiondoka klabuni kwa gari lake binafsi baada ya kuzungumza na wachezaji leo. (Picha zote na Emmanuel Ndege wa blogu ya Liwazozito).


MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji leo ametembelea tena makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kuzungumza na wachezaji.
Manji alifika klabuni hapo akiwa ameongozana na makamu wake, Clement Sanga, wajumbe wa kamati ya utendaji, Abdalla Bin Kleb na Mussa Katabalo pamoja na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili, Seif Ahmed.
Viongozi hao walikutana na wachezaji kwa saa kadhaa na kuzungumza nao mambo mbalimbali kwa lengo la kuwaweka sawa kabla ya mechi yao ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
Yanga inatarajiwa kushuka dimbani leo kucheza na Mafunzo katika mechi ya pili ya robo fainali itakayoanza saa 10 jioni. Katika mechi ya awali, URA ya Uganda itavaana na APR ya Rwanda.
Katika kikao hicho cha faragha, inasemekana kuwa Manji na viongozi wenzake waliwataka wachezaji kutambua vyema jukumu lililo mbele yao na kuongeza jitihada ili waweze kufika mbali zaidi.
Alisema mechi hiyo ni muhimu kwao kwa vile iwapo wataishinda Mafunzo watafuzu kucheza nusu fainali na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa.

SAMATTA ATOA PASI MBILI ZA MABAO, MAZEMBE IKIBANWA 2-2 NA CHELSEA NYUMBANI


Samatta. Picha ta Maktaba

Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’, leo ametoa pasi zote za mabao mawili ya klabu yake, Tout Puissant Mazembe, kwenye Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Berekum Chelsea ya Ghana, uliomalizika hivi punde kwa sare ya 2-2.
Mapande yote ya Samatta leo yalitumiwa vema na Tressor Mputu Mabi katika dakika za 11 na 32 kuipatia mabao Mazembe, wakati Chelsea ya Ghana ilionyesha yenyewe ni moto kweli kwa kupata sare Lubumbashi. Mabao ya Chelsea yalifungwa na Emmanuel Atukwei Clottey katika dakika za 71 na 84. Dakika ya 75, Samatta alimpisha Francis Kasonde wakati huo wenyeji wakiwa wanangoza 2-1, lakini kutoka kwake kulisababisha jahazi kuzama kabisa.
Katika mchezo wa kwanza, Mazembe ilifungwa 1-0 wiki iliyopita, Samatta akifunga bao la kufutia machozi Cairo na sasa mabingwa hao mara nne Afrika wana pointi moja tu ndani ya mechi mbili, kuashiria kwamba wana kibarua kizito kutimiza ndoto zao za kutwaa ndoo ya tano Afrika.
Mechi nyingine ya Kundi lao, itafuatia saa 5:00 usiku, kati ya wapinzani wa jadi katika soka ya Misri, Zamalek na Al Ahly.

SPIDER MAN HATARINI KUWAKOSA MAFUNZO, NIZAR HATA JEZI HAVAI KESHO, BERKO, CHUJI, KIIZA NAO NJE NDANI


Said Bahanuzi 'Spider Man'

Na Prince Akbar
MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ yuko hatarini kuikosa mechi ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kesho dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, kutokana na maumivu ya mgongo, wakat kiungo Nizar Khalfan yeye kwa asilimia 100 hatacheza kutokana na maumivu ya nyonga.
Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, Nizar hatacheza kabisa, lakini wachezaji wengine watatu, Bahanuzi, kipa Yaw Berko anayesumbuliwa na goti, kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Hamisi Kiiza wanaosumbuliwa na quadriceps wako kwenye hatihati kucheza.
Mtakatifu Tom amesema kwamba, Daktari wa Yanga, Sufiani Juma anaendelea kufuatilia afya za Bahanuzi, Kiiza, Berko na Chuji ili kuhakikisha wanakuwa fiti kwa ajili ya mechi ya kesho, lakini kwa Nizar kocha huyo wa zamani wa Namibia na Ethiopia, amekwishakata tamaa kumtumia kwenye mechi na Mafunzo.
Amesema sababu ya wachezaji wake kuumia mara kwa mara ni kutokana na kucheza mechi mfululizo na kulingana na kanuni za mashindano hayo, hawezi kutumia wachezaji zaidi ya 20, hivyo hana namna nyingine zaidi ya kupambana na hali hiyo.
Bahanuzi ndiye kinara wa mabao wa Yanga hivi sasa, hadi sasa akiwa amekwishaifungia timu hiyo mabao manne, hivyo kuingia kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha mashindano hayo, ambayo tayari kwenye kabati la Yanga kuna mataji manne yamehifadhiwa.
Mshambuliaji huyo mpya kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, juzi alikaribia kuondoka na mpira uwanjani, kama si refa Dennis Batte kutoka Uganda kukataa bao lake moja siku ambayo alifunga mawili yaliyokubaliwa dhidi ya APR ya Rwanda, Yanga ikishinda 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Katika mchezo huo, Kocha Tom alimpumzisha Bahanuzi dakika ya 72 na nafasi yake ikachukuliwa na Jerry Tegete, wakati Nizar Khalfan kabla ya hapo alimpisha Juma Seif ‘Kijiko’.
Wakati huo huo: Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), leo limesema kwamba mechi ya Yanga kesho itakuwa ya pili, kama ambavyo itakuwa kwa Simba keshokutwa.

RATIBA ROBO FAINALI
Julai 23, 2012
URA vs APR (Saa 8:00 mchana)
Mafunzo vs Yanga (Saa 10:00 jioni)
Julai 24, July
Atletico vs AS Vita (Saa 8:00 mchana)
Azam vs Simba SC (Saa 10:000 jioni)

No comments: