Thursday, July 19, 2012

EMMANUEL OKWI ANATOKA KIMAPENZI NA SINTAH?

 

Baada ya kufanikiwa kuiwezesha Simba SC kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania, striker mwenye kutupia jersey namba 25 yaonekana sasa yuko in love with Sintah who used to be Juma Nature's girlfriend.
Kwa taarifa yako ni kuwa penzi la Emanuel Okwi na Christine John "Sinta" who proclamed herself as JLO wa Bongo liko wazi wazi hakuna cha kuficha even followers wa twosome hawa kwenye Twitter knows bout this.


"OMG! nani kawaambieni uwa mie na-date na Sintah? she use to be my close friend toka akisoma nchini kwetu UG, but is there any problem kama nikiwa na mahusiano ya kimapenzi nae?" aliuliza Okwi ambaye kwa sasa yupo Austria baada ya kutwangiwa phone na Mwandishi wa Baabkubwa.


Lakini side B kwa Sintah ambaye kwa sasa ni co-host wa show iitwayo "Hatua Tatu" alongside Steve Nyerere at Times FM ilikuwa hivi, "Jamani Okwi ni mshakaji wangu wa karibu, nilikuwa karibu nae toka na-xul Uganda but tukapotezana baada ya yeye kwenda kucheza Rwanda ambapo hivi majuzi mwenyewe ndio kanitafuta akitaka kunijulia hali"- alitok Sintah. Haikupita dakika kadhaa, Sintah called back asking about alichokisema Okwi, "Jamani simniambie amesemaje nifurahi jamani, niambieni kama kasema ananipenda au kama kanikana jamani?"
Okwi uko tayari kutunga nyimbo kama alivyofanya Nature?




 

MKOSI KWA SIMBA: AMIR MAFTAH KUIKOSA KAGAME - AVUNJIKA


BEKI wa pembeni wa Simba, Amir Maftar ameondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Maftar ameondolewa kwenye kikosi hicho baada ya kidole chake cha mkono wake wa kulia kuvunjika, kwenye mechi dhidi ya Ports iliyochezwa jana saa 10: 00 jioni iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0.

Kwa mujibu wa Daktari Mkuu wa timu hiyo, Cosmas Kapinga amesema kufuatia majeraha hayo aliyopata amevishwa P.OP kutokana na maumivu aliyoyapata katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Daktari huyo amesema, huenda akizikosa mechi zote zinazofuata za michuano hiyo inayoendelea, timu ikifuzu hatua ya robo ya fainali kwa ushindi huo walioupata .

“Maftar tumemuondoa kwenye kikosini, baada ya kupata majeraha ya kidole chake cha mkono wake wa kulia kuvunjika na kusababisha avishwe P.O.P, aliumia katika mechi na Ports tuliyocheza jana,” alisema Kapinga

No comments: