Tuesday, May 15, 2012

MANCINI AMALIZA UTATA; BALOTELLI ANABAKI MAN CITY


CHAMPION ... Mario Balotelli celebrates Manchester City's title win with boss Roberto Mancini
MABINGWA ... Mario Balotelli akishangilia na wenzake wa Manchester City ubingwa, wakiwa na kocha wao Roberto Mancini
Published: Today at 10:06

ROBERTO MANCINI amethibitisha Mario Balotelli anabaki Manchester City.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Inter Milan, amekuwa akihusishwa na habari za kurejea Serie A baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi na Arsenal, ambayo timu ilifungwa huku Mancini akikaririwa kusema angemuuza.
Na taarifa nchini Italia zimesema kwamba AC Milan ilikuwa inajiandaa kumnyakua mpachika mabao huyo kwa kubadilishana na Zlatan Ibrahimovic.
Lakini Mancini amezipiga chini tetesi hizo kwa kusema: “Ibra ni mchezaji mkubwa, lakini sifikirii kama Milan wanataka kumuuza.
Wakati huo huo, Balotelli — aliyempa pasi Sergio Aguero kufunga bao la ushindi katika mechi na QPR iliyowapa ubingwa dakika ya 94, ameitwa kwenye kikosi cha awali cha Italia kwa ajili ya Fainali za Euro 2012.

WAKALA WA VAN PERSIE AKUTANA NA KIGOGO WA MAN CITY ETIHAD


EPL: Robin van Persie, Wolverhampton v Arsenal
Getty
EXCLUSIVEBy Wayne Veysey | Chief Correspondent

WAKALA wa Robin van Persie amesema kwamba alialikwa na Mtendaji Mkuu wa klabu ya Manchester City, Brian Marwood kuangalia mechi Uwanja wa Etihad.
Sign up with 188BET for a FREE bet up to £25 – Great Prices, Every Game

Kees Vos, mwakilishi wa mshambuliaji huyo wa Arsenal ameaimbia Goal.com alikuwa mgeni wa Marwood katika Uwanja wa nyumbani wa City “kiasi cha miezi mitatu iliyopita”.

Lakini Vos amekataa kwamba kikao hicho kilikuwa cha kujadili uhamisho wa nyota huyo kwedna kwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu England.

“Ndio, nilikuwa mgeni wa Marwood, Manchester City, huo ni ukweli, ilikuwa miezi mitatu iliyopita.

ORANJE TIDE?
8.0 Netherlands are 8.0 with 188Bet to win Euro 2012
“Nilikutana na watu wengi. Kwa nini natakiwa kujieleza? Nafanya kazi katika kampuni ambayo ina wateja 450 na wachezaji 350 wa kimataifa.

“Mimi si wakala wa Robin pekee. Pia ni wakala wa Thomas Vermaelen, Keisuke Honda, Jeremain Lens na Stefan de Vrij.”

Licha ya ufafanuzi huu wa Vos, ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sports Entertainment Group ya Uholanzi, wachezaji ambao wanaonekana kuwatoa udenda City dhahiri kabisa ni Van Persie na Vermaelen, ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka minne Arsenal Oktoba, mwaka jana.

WACHEZAJI YANGA TATIZO LILIKUWA AFYA, DAKTARI WAO AFICHUA



Dk Sufiani Juma wa Yanga
RIPOTI za madaktari wa Yanga, zimebainisha kwamba asilimia 30 ya wachezaji wa klabu hiyo wakiwemo wote wa kigeni walikuwa na matatizo mazito kiafya msimu uliopita na Rashid Gumbo anahitaji matibabu na uangalizi wa karibu.
Yanga imeyumba katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kujikuta ikiishia nafasi ya tatu huku Simba ikiipora ubingwa na Azam Fc ikishikilia nafasi ya pili.
Gazeti la Mwanaspoti leo limeandika kwamba, wamefanikiwa kuona ripoti mbalimbali zilizoandikwa na madaktari waliokuwa na Yanga kwa vipindi tofauti msimu mzima zimebainisha kwamba usajili wa kiholela bila kufanya vipimo vya awali umechangia matatizo hayo ya kiafya.
Madaktari hao wameonyesha kuwa matatizo makubwa yaliyojitokeza kwa asilimia kubwa ni kuchanika kwa msuli mgumu (ligaments), nyama, kuvimba kwa vifundo vya miguu na maungio ya mifupa.
Matatizo mengine ni pamoja na afya ya akili (matatizo ya kisaikolojia)na ulevi wa kuvuta sigara na unywaji wa pombe.
Kwa mujibu wa ripoti hizo ambazo zimeushutumu uongozi kwa kutokuwa makini wakati wa usajili, zimeeleza kuwa asilimia kubwa ya wachezaji hao kama uchunguzi wa kitaalamu ungefanyika awali baadhi yao wasingesajiliwa kwavile wangelazimika kukaa nje muda mwingi kwa matibabu.
Kuhusu Gumbo, habari za ndani zinasema kuwa madaktari wameeleza kuwa ana tatizo ambalo linahitaji uangalizi wa kitaalamu.
Sehemu ya ripoti hizo inasema kuwa ; "Tatizo la Gumbo si la kudumu bali linaweza kutokea anapokuwa mchezoni hususani anapokuwa anachinja mipira(kupiga daglish au kupiga mipira outer). Tatizo hilo humfanya asiweze kabisa kuendelea na mchezo kwa siku husika na humchukua takribani dakika 45 hadi saa 2 kupoa bila kutumia dawa. Kimsingi mchezaji huyu kwa hali ya Tanzania anaweza kutumika chini ya uangalizi wa daktari kwa vile msuli kamba unaounganisha mifupa kwenye maungio unaomsumbua imesababishwa na kulegea kwa msuli kamba (subluxation of ligament) na hivyo kuwa inatoka katika sehemu yake pindi kiungo hicho cha goti la kulia kinapowekwa katika mkao tofauti."
Uchunguzi unaonyesha kuwa asilimia 30 ya wachezaji ambao ni wale muhimu na wa kutegemewa kwenye kikosi cha kwanza wakiwemo wote wa kigeni wana wamegundulika kuwa na matatizo ya kiafya ambayo kwa kiasi fulani yamechangiwa na matunzo mabovu ya kitaalamu katika mazingira waliyoyakuta ndani ya Yanga.
Katika ripoti hizo mbalimbali uongozi umeshauriwa kuwa na timu ya afya yenye ujuzi na vyeti ambayo itapima afya za wachezaji kabla na wakati wa mapumziko ya ligi ili kudurusu afya zao na kisha kujua tatizo kabla ya kumuondoa kabisa mchezoni kwa matibabu.
Wataalamu hao kwa upande mmoja wameulaumu uongozi kwa kutowaamini wanataaluma wanaowaajiri hususani madaktari kwenye kufanya maamuzi na pia kuboresha miundo mbinu ya gym na sehemu ya kuogelea kwenye jengo la klabu kukabiliana na matatizo ya wachezaji

KASEJA AFICHUA SIRI NZITO SIMBA KUTOLEWA AFRIKA

Kaseja wa pili kutoka kulia katika kikosi cha Simba SC
PATRICK Mafisango haamini kama Simba imetolewa kwenye michuano ya kimataifa, lakini kipa Juma Kaseja ametoa siri nzito za wachezaji baada ya kutamka kwamba aliwalazimisha kupiga penalti.
Simba imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Al Ahly Shandy, juzi Jumapili.
Mafisango na Kaseja ndio wacheza
ji waliokosa penalti Simba ilipofungwa kwa penalti 9-8 baada ya muda wa mchezo kumalizika kwa jumla ya mabao 3-3.
"Nilijiskia vibaya kukosa penalti sababu nilijua ilikuwa muhimu kwangu kwa timu, ila ni bahati mbaya, sijui nini kimetokea uwanjani, ni sehemu ya mchezo ila tulijiandaa kushinda na kila mmoja wetu alijua hivyo."
Gazeti la Mwanaspoti leo, limemnukuu Nahodha wa Simba, Juma Kaseja akisema kuwa walifungwa kutokana na kuvurugikiwa kisaikolojia baada ya wapinzani wao kurudisha mabao yote matatu ndani ya dakika 15 za kwanza za kipindi cha pili.
"Tulipoteana uwanjani, hakuna kati yetu aliamini kuwa wangeweza kusawazisha yale mabao. Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana, ila ndani ya dakika tano za kipindi cha pili walifunga mabao mawili na la tatu hatukuamini," alisema Kaseja.
"Nina uzoefu na wachezaji wa Simba, baada ya kufungwa mabao matatu, niliwaangalia usoni na kuona wamebadilika." Alisema ndio maana ulipofika wakati wa penalti, wachezaji wenzake waliogopa kupiga kwa kuogopa lawama na wengi walikuwa wamepoteza morali.
"Nikiwa kama nahodha niliwalazimisha kupiga, kocha ananiuliza Kaseja nani anapiga, nikimtaja mtu anaogopa, ikabidi nitumie nguvu, sababu ilibidi tupige," alisema Kaseja.
"Walishinda kwa sababu penalti, siku zote hata kwa timu kubwa kama Real Madrid au Barcelona, haina mwenyewe ni kama kitu cha bahati, tucheza vizuri ila makosa madogo yalikuwa chanzo, ila kwa sasa tusilaumiane, tuangalie tulipojikwaa kwa ajili ya michuano ijayo," alisema.
Kaseja alidokeza kuwa uchovu kwa wachezaji wake ni kikwazo pia."Kwa muda mfupi tumecheza mechi nyingi na wachezaji ni wale wale tu, kama mabadiliko ni kidogo sana.
Kocha asilaumiwe kwa kuchezesha wachezaji wale wale kwa sababu anajaribu kutengeneza timu ya pamoja, iliyokaa kwa muda mrefu na kuelewana kama vile ilivyo kwa Manchester United na timu nyingine kubwa duniani."
"Najua wengi watashangaa kwa nini tumeweza kushinda nyumbani mabao 3-0 na kufungwa ugenini mabao kama hayo katika muda wa dakika 90 na baadaye kupoteza penalti, hii ni kawaida, kwani, kawa tuliweza kuwafunga nao pia inawezekana kwa upande wao, mpira hauna kanuni, tuliweza kuruka vizingiti na kushinda mengi ngumu na kupoteza kwa timu ya kawaida kama Al ahly shandy, huu ndio mpira,"alisema Kaseja kwa huzuni.
"Ni kweli, kwa mtazamo wangu, tunahitaji kusajili wachezaji mahiri, kutokana na upungufu tuliouona ila tusitumie kigezo cha kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho kama kigezo cha kuvuruga timu.
"Ili timu ielewane, inahitaji kukaa pamoja viongozi waangalie maeneo ambayo yanahitaji kuongezewa nguvu na kusajili wachezaji wazuri kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya klabu bingwa ya Afrika itakayokuja mbele yetu, majina hayachezi uwanjani, tuangalie uwezo wa wachezaji katika kuisaidia timu ishinde na kufanya vizuri."
Ushindi huo wa Shandy ambao haukutegemewa kwa wenyeji kutokana na kuwa na uzoefu mdogo katika michezo ya kimataifa na hofu yao kwa Simba, umesogeza timu hiyo hatua ya 16 bora

No comments: