Saturday, April 14, 2012
WALCOTT AWAKUMBUSHA KITU ARSENAL HAWAWEZI KUSAHAU MSIMU HUU
Walcott katikati ya Song kulia na Sagna kushoto |
MUINGEREZA Theo Walcott amesema kwamba Arsenal ilianza ligi rasmi msimu huu baada ya kuifunga 5-3 Chelsea, Oktoba 29, mwaka jana.
Ushindi huo ulikuja baada ya Arsenal kuuanza msimu vibaya ikiwemo kutandikwa mabao 8-2 na Manchester United.
Walcott alicheza kwa kikubwa sana siku hiyo akiwa na jezi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, na akafunga bonge la bao lililodhihirisha kipaji na umahiri wake.
Dogo huyo wa umri wa miaka 23 amezungumzia mechi hiyo kama moja ya mechi ambazo hawezi kuzisahau msimu huu na ndiyo iliyowafufua.
"Mechi na Chelsea ilikuwa hatua kubwa kwa sababu tulijua tuko vizuri [wakati huo]," alisema Walcott.
"Kwenda nje ya nyumbani na kufunga mabao mengi, ilikuwa ni kila kitu. Ilikuwa babu kubwa jinsi tulivyoshirikiana, baada ya mechi (furaha yake) ilikuwa kama tumetwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
"Huo ni moja ya wakati ambao tunataka utokee tena na bahati nzuri umetokea tena katika wiki za karibuni."
Walcott amefunga mabao manane katika timu yake hadi sasa msimu huu, mawili kati ya hayo alifunga kwenye ushindi wa 5-2 dhidi ya Spurs, Februari.
GUARDIONA AMTEMBELEA ABIDAL HOSPITALI, AKAA NAYE DAKIKA 20
Abidal |
KOCHA wa Barcelona, Pep Guardiola amemtembelea beki Eric Abidal hospitali jana baada ya mchezaji huyo kufanyiwa upasuaji wa ini mapema wiki hii.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa amepigwa kisu na inasemekana anaendelea vizuri baada ya zoezi hilo gumu.
Guardiola alitumia muda wa dakika 20 akiwa na Abidal na familia yake, na amemtakia mchezaji huyo kupona haraka katika upasuaji huo wa pili juu ya tatizo hilo.
Rais wa Barcelona, Sandro Rosell alisema kwamba Mfaransa huyo anaendelea vizuri.
MAN CITY YAUA 6-1, TEVEZ APIGA TATU
Tevez |
MUARGENTINA Carlos Tevez amepiga hat-trick akiisaidia Manchester City kuitandika Norwich 6-1 na kupunguza pengo la pointi wanazozidwa na Manchester United hadi mbili katika Ligi Kuu ya England. United itacheza na Aston Villa kesho.
Tevez alifunga dakika ya 18, 73 na 80 wakati mabao mengine yalitupiwa na Aguero dakika ya 27 na 75 na Johnson dakika ya 90, wakati la wapinzani wao lilifungwa na Surman dakika ya 51.
Licha ya kocha wa City, Roberto Mancini kukata tamaa ya kuwakamata watoto wa Sir Alex Ferguson msimu huu, lakini ushindi huu bila shaka hata yeye unamfanya aone inawezekana.
No comments:
Post a Comment