Tuesday, April 24, 2012

Monday, April 23, 2012


LULU ALIZA WATU KISUTU, KESI YAPIGWA KALENDA


Lulu akitoka mahakamni na kurudishwa mahabusu gereza la Segerea

MWIGIZAJI nyota wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo amewatoa machozi baadhi ya watu waliohudhuria kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
Lulu mwenye umri wa miaka 17, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya mwigizaji mwenzake, Steven Charles Kanumba, aliwasikitisha watu na baadhi kumwaga machozi, kutokana na jinsi alivyowasili Mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza.
“Masikini biti anapata matatizo sasa, inatia huruma, nawaonea huruma wazazi wake, wanakosa raha sasa,”alisikika mtu mmoja akisema mahakamani hapo.
Pamoja na kufikishwa mahakamani hapo,
Hakimu Mkazi wa Mahakama Kisutu, Ritha Tarimo aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 7, mwaka kwa sababu upelelezi bado unaendelea.
Lulu anayekabiliwa na tuhuma za kumuua The Great Kanumba aliyefariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake Vatican, Sinza Dar es Salaam, hii ni mara ya pili kufikishwa mahakamani hapo.
Lulu aliyecheza filamu kadhaa na marehemu Kanumba waliyeibuka naye katika kundi la Kaole, Magomeni, hakutakiwa kutoa maelezo yoyote Mahakamani, kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Wakati kesi hiyo ikiwa katika hatua za mwanzoni, Polisi bado inaendelea na uchunguzi wake na baadhi ya watu wakiwemo wasanii wamekuwa wakihojiwa kulisaidia jeshi hilo upelelezi.
Taarifa za awali baada ya kifo cha Kanumba, zilisema kwamba mwigizaji huyo alifariki baada ya kusukumwa na Lulu nyumbani kwake Sinza Vatican, ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake.
Inaelezwa baada ya tukio hilo, Lulu alikimbia nyumbani kwa Kanumba na mdogo wa Ther Great, Sethi Bosco akaenda kuchukua gari kumpeleka kaka yake hospitali ya Muhimbili, ambako alipofika iligundulika amekwishafariki dunia.
Sethi alikaririwa akisema kwamba siku ya tukio, Lulu alikwenda kwao usiku wa manane na alipofika yeye (Sethi) alimuacha aongee na kaka yake. Sethi alidai aliwaacha sebuleni akaingia chumbani kwake na baadaye akasikia wameingia chumbani (kwa Kanumba).
Sethi alisema baada ya muda alisikia kelele za dalili ya ugomvi na baada ya muda Lulu alitoka kumwambia (Sethi) juu ya hali ya Kanumba kubadilika na kuwa mbaya.
Sethi alidai aliposikia hivyo akashituka na kwenda chumbani ambako alimkuta kaka yake katika hali mbaya, povu likimtoka mdomoni hivyo kuchukua hatua ya kumuita daktari wake, kabla ya kumkimbiza Muhimbili.
Lulu alikamatwa asubuhi ya kuamkia siku ya tukio hilo, linalodaiwa kutokea usiku wa manane na kuwekwa kizuizini katika kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam.
Tayari baadhi ya wanaharakati wa haki za wanawake wamekwishatangaza azma yao ya kumsaidia Lulu katika kesi hii.
Miongoni mwao ni Mbunge wa Jimbo la Kawe, (CHADEMA), Halima Mdee.
Bado watu wanajiuliza maswali mengi kuhusu kifo cha Kanumba, mojawapo kama kweli Lulu anayedaiwa kumuuwa wakati wakigombana ‘ana ubavu’ huo.
Lakini pia, siku ya kifo cha Kanumba, inadaiwa alionekana katika ukumbi wa starehe, Club Maisha akinywa pombe.
Uchunguzi wa madaktari katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ulisema pombe kali aina ya Jackie Daniels ilisababisha kifo cha mwigizaji huyo.
Lakini baadhi ya vielelezo vilipelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali, ili kutaka kujua kama msanii huyo aliwekewa sumu.
Kifo cha Kanumba kimewaumiza wengi, kwani msanii huyo alikuwa mahiri na kipenzi cha wapenzi wa filamu nchini.
Wapembuzi wa mambo wanasema huu ni msiba wa kwanza kuteka hisia za watu wengi zaidi, tangu kifo cha baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba mwaka 1999.

GARI WATAKALOGOMBEA MABONDIA MAUGO NA CHEKA HILI HAPA


Msemaji wa Mpambano wa Ngumi kati ya Mada Maugo na Francis Cheka , Yasini Abdallah akionesha mkana na gari atakalopewa mshindi wa mpambano huo.picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
  1. Johannes Lugenge kushoto na Promota wa Mpambano wa Mada Maugo na Francsis Cheka, Lucas Rutainurrwa wakionesha mkana wa Ubingwa wa I.B.F Afrika na gari atakalochukua bingwa wa mchezo huo Dar es salaam.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com




Na Mwandishi Wetu

WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gari watakalogombania Mabondia Mada Maugo Na Francis Cheka Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.


LULU MAHAKAMANI LEO, WAANDISHI WAZUIWA KUMPIGA PICHA

Mtuhumiwa wa mauaji ya mwigizaji Steven Charles Kanumba, Elizabeth Michael 'Lulu' akiingia Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kesi yake leo, chini ya ulinzi mkali wa askari wa Magereza, ambao walikuwa wanawazuia Waandishi wa habari kupiga picha. Habari inakuja.

ALONSO AIWANGIA BARCELONA KWA CHELSEA


Xabi Alonso - Real Madrid
Xabi Alonso - Real Madrid
KIUNGO wa Real Madrid, Xabi Alonso ameihakikishia Chelsea kwamba Barcelona si timu isiyofungika kwenye Uwanja wake wa Camp Nou.

The Blues ina kipaumbele cha bao dhidi ya klabu hiyo ya Katalunya ikijiandaa kumenyana nayo katika mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kesho, na Alonso, mmoja wachezaji wa Real Madrid walioifunga timu hiyo ya Pep Guardiola katika El Clasico Jumamosi , anaamini kwamba licha ya vipaji vyao, mabingwa hapo watetezi wanafungika.

"Sababu hiyo haitokani na leo tu," alisema Alonso . "Lakini siku nyingine pia. Tuliona Chelsea wakiwafunga.

"Tunafahamu kwamba miaka michache iliyopita, Barcelona wamekuwa na mafanikio ile mbaya, kwamba walikuwa wakicheza babu kubwa, soka ya kustaajabisha. Lakini wao si timu isiyofungika.

"Chelsea wanaongoza. Wako mbele katika mabao. Kucheza hapa ni vigumu, lakini tutaona kitakachotokea."alisema.

AVATAR LA KICHINA HILI HAPA



'Avatar 2': Made in China?

Add to Mixx!
Add to Yahoo! Buzz
ALTMore and more Hollywood filmmakers are looking across the Pacific these days, and James Cameron is among them. Walt Disney Co., Relativity Media, and DreamWorks Animation have all announced plans to co-finance and release films in China, and now Cameron has traveled to the country to explore the possibility.

During a five-day visit to Beijing, the Titanic director told Reuters, "We're all looking very seriously at the possibility of a co-production. The question is, what's required of us? In terms of configuring the market for the Chinese marketplace, and what economic benefit do we get in return?" He added, "If it works — and I want to definitely stress if — it seems to me it could be very advantageous to the Chinese film community, because for us to do a film like Avatar which is an entirely studio shoot, we wouldn't be here for the scenery ... We'd be bringing in infrastructure to do virtual production, to do 3-D photography and so on, which I would think would be a positive technology exchange into this film-making community."

However, like other filmmakers, Cameron is concerned about the restrictions the Chinese government would place on Hollywood films. "It all needs to be dealt with upfront. Here's the script, this is what we're doing, and if there's a problem with that then I have to decide creatively if I'm going to accommodate, or if I'm going to pass," he explained. Currently the government limits the number of foreign films that can be distributed in the country, and bans films which contain content deemed inappropriate. However, Cameron thinks that the Chinese people, who are huge fans of American films, should have the final say in what's acceptable to see in theaters. "I think that any restrictions that are not strictly market driven are unnecessary," he said. "I think the Chinese people will vote with their wallets about what it is they want to see."

HII NIMEITOA FULL SHANGWE, SOMENI


SBL KUBADILISHA MAISHA YA WATEJA WAKE!

Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia vinywaji vyake bora kabisa vya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager iameandaa promosheni kubwa na ya aina yake itakayofanyika Tanzania nzima katika kipindi cha wiki 16 ambapo zawadi mbalimbali zitashindaniwa.
Promosheni hiyo ya aina yake imesheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta 16 , Pikipiki 8, Bajaji 8, Gari ndogo maarufu kama saloon car 8, pamoja na zawadi zingine nyingi ambapo kila baada ya wiki mbili gari 1 aina ya saloon itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki mbili Bajaji 1 itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki Pikipiki moja itashindaniwa na kila baada ya wiki moja Jenereta moja itakuwa inashindaniwa.

Akizungumzia promosheni hiyo kabambe Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, bwana Ephraim Mafuru amesema promosheni hiyo sio tu inalenga kuongeza mauzo ya vinywaji hivyo bali pia inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hiyo kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa aina yake.

“Kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya taifa letu katika maeneo mbalimbli kupitia jamii inayotuzunguka na wateja wetu kimaisha, hivyo promosheni hii pamoja na ukweli kuwa inalenga kuongeza tija katika masoko ya bidhaa zetu bado unaweza kuona zawadi zitakazoshindaniwa katika promosheni hii ni zawadi kubwa ambazo kwa namna moja ama nyingine inaweza kubadilisha maisha ya mshindi wetu kutoka hatua aliokuwepo hadi hatua nyingine, kwa hivyo sisi SBL tunasema tunajivunia kuwa sehemu mojawapo inayochangia maendeleo ya watanzania wateja wetu na taifa kwa ujumla” alisema bwana Mafuru.
Kwa upande wake Meneja wa bia ya Tusker Lager, Bi Rita Mchaki, amesema kampuni ya bia ya Serengeti inazalisha bidhaa zinazopendwa na watanzania wengi kutokana na ubora wa kipekee wa bidhaa hiyo, na kwamba promosheni hiyo kabambe nisawa nakurudisha shukrani zake kwa watanzania kwa kufanikisha kampuni hiyo kufikia malengo yake kibiashara.
Watanzania wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi na wanaotumia bidhaa zetu zilizoainishwa katika promosheni hii wanaombwa kushiriki kwa wingi bila kukata tamaa kwani zawadi zinazoshindaniwa zinaweza kubadilisha maisha kwa yeyote atakayebahatika kuibuka na ushindi.

KAMATI YA MAZISHI YA KANUMBA KATIKA SHUGHULI NZITO ILIYOGHARIMU FEDHA NYINGI

Akiwa katika huzini kubwa, ni Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Mahugila Madega tayari kuchangia na Millene Happy Magesse tayari kuandika kilichoingia
Irene kushoto bize na simu na msosi, kama Janguo kulia
Millene Happiness magesse kulia na Issa Mussa 'Cloud' kushoto. Fedha zote za michango alikuwa anapokea Cloud, halafu Happy Magesse anaandika kitabuni.
Ruge na Dk Nchimbi
Kamati ya Mazishi ya Steven Kanumba ikiwa kazini katika michakato ya bajeti. Wa kwanza kutoka kulia ni Ruge, anayemfuatia ni Dk Nchimbi, JB na Wajumbe wengine wa Kamati hawapo pichani.

SAGNA ASEMA ARSENAL HAWAKUWA BORA KWA CHELSEA


Bacary Sagna and Abou Diaby
Barclays Premier LeagueArsenalMatch MenuChelsea
Arsenal 0-0 Chelsea
Barclays Premier League
J'mosi Aprili 21, 2012,

Bacary Sagna amesema Arsenal haikuwa katika kiwango chake cha ubora katika mechi dhidi ya Chelsea, lakini amefurahia kucheza mechi tano kati ya saba bila nyavu zao kuguswa
Sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates inawabakiza watoto wa Arsène Wenger nafasi ya tatu, wakiizidi pointi tatu Newcastle ambao wana mchezo mmoja mkononi.
Sagna bado hajiamini kwamba wanaweza kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa na amesema timu yao lazima irejeshe fikra zake kwenye mechi dhidi ya Stoke Jumamosi haraka sana.
“Nafikiri dhidi ya Chelsea tulihangaika kugongeana pasi kama kawaida yetu.Hatukukaa sana na mpra na tulisota kutengeneza nafasi,” alisema Sagna . “Lakini angalau hatukufungwa na tumeendeleza kutoruhusu nyavu zetu kutikiswa, hivyo lazima tuangalie mbele katika mchezo ujao.
“Tunataka kurfuzu Ligi ya Mabingwa na tunataka kumaliza katika nafasi ya tatu. Haitakuwa rahisi, lakini tunataka kufanya hivyo.
“Kila mmoja anataka kufuzu Ligi ya Mabingwa . Tottenham wapo nyuma yetu, Newcastle hawako mbali.”alisema.

MKUTANO MKUU TFF HAUNA LOLOTE LA MAANA, USANII MTUPU


WENGI walitarajia Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Jumamosi na Jumapili, ungejadili mambo ya msingi katika kutafuta suluhisho la matatizo sugu katika soka yetu, lakini kulingana na taarifa ambayo bongostaz.blogspot.com imetumiwa na TFF, Mkutano huo ulikuwa bure tu.
Zaidi taarifa ya TFF imejaa siasa tu na si kuhusu namna ya kuikwamua soka yetu kutoka hapa ilipo, maana yake chini ya TFF hii tumekwisha!

SOMA MWENYEWE TAARIFA YAO UJIONEE, KUNA KITU HAPA?
MKUTANO MKUU WA MWAKA 2011 WA TFF
Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) wa 2011 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umefanyika kwa siku mbili (Aprili 21-22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront na kuhudhuriwa na wajumbe 104. Mkutano ulipokea taarifa, kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali na mengine yaliyojitokeza kama ifuatavyo;
EL MAAMRY, NDOLANGA WATUNUKIWA URAIS WA HESHIMA
AGM ilipitisha pendekezo la kuwatunuku urais wa heshima wa TFF, Alhaji Said Hamad El Maamry na Muhidin Ahamadi Ndolanga lililowasilishwa na Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
Alhaji El Maamry ambaye ni mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) alikuwa Mwenyekiti wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) kuanzia mwaka 1973 hadi 1986. Alhaji Ndolanga aliongoza FAT kuanzia mwaka 1993 hadi 2004.
BAJETI YA MWAKA 2012
Bajeti ya Mwaka 2012 ya sh. 7,246,628,650 kwa ajili ya matumizi ya TFF ilipitishwa. Kwa mwaka 2012 TFF inatarajia kukusanya sh. 7,572,991,433 kupitia vyanzo mbalimbali.
Vyanzo hivyo ni viingilio vya uwanjani vinavyotarajiwa kuingiza asilimia 22 ya mapato yote, udhamini (asilimia 74) na vyanzo vingine kama haki za matangazo ya televisheni, ada za ushiriki wa timu katika mashindano mbalimbali, misaada kutoka FIFA na CAF ambayo kwa pamoja vinatarajiwa kuingiza asilimia nne ya mapato yote.
KAMATI YA LIGI YA TFF
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaendelea na mchakato wa kupendekeza mifumo mitatu tofauti ya chombo kitakachosimamia/kuendesha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ikieleza faida na athari za kila mfumo uliopendekezwa na baadaye kuwafanya mawasilisho (presentation) kwenye Kamati ya Utendaji.
Baada ya kuwasilisha mifumo hiyo kwa Kamati ya Utendaji, Kamati ya Ligi itapendekeza mfumo upi kati yao hiyo inaoona unafaa kabla ya kufanyika uamuzi wa mwisho.
Lengo la kuunda chombo maalumu cha kuendesha ligi ni kuongeza ufanishi katika uendeshaji wa VPL na FDL, na pia kuifanya Sekretarieti ya TFF kushughulikia zaidi shughuli za maendeleo.
UUZWAJI WA TIMU
Uuzaji wa timu linabaki kuwa suala la kisheria. Lakini TFF imeweka utaratibu ufuatao; lazima Mkutano Mkuu wa klabu husika uidhinishe uuzaji, na timu ikishauzwa inabaki katika mkoa husika.
MFUMO WA MASHINDANO
Kwa vile kuna tatizo la ligi mbalimbali kuwa fupi, hali inayosababisha baadhi ya wachezaji katika madaraja ya chini kucheza ligi zaidi ya moja katika msimu mmoja, mfumo wa ligi/mashindano utaangaliwa upya.
Mfumo uliopo sasa uliwekwa kwa ajili ya kuvutia uwekezaji katika mpira wa miguu ambapo mwekezaji anaweza kuanzisha timu, na ndani ya miaka mitatu ikacheza Ligi Kuu. Pili, ilikuwa ni kuondoa mlolongo mrefu wa ligi, na kuwafanya wanachama wa TFF (mikoa) nao kuendesha ligi zao mikoani.
Ijulikane kuwa ligi za mikoa (regional leagues) zinachezwa. Kwa sababu TFF inaendeshwa kwa mfumo wa shirikisho (federation), nia ni wanachama wa federation nao kuwa na majukumu ya kusimamia na kuendesha ligi, kwa vile TFF haiwezi kusimamia ligi zote.
MAREKEBISHO YA KATIBA
Mkutano Mkuu wa TFF umepitisha marekebisho ya Katiba katika maeneo mawili; moja ni kuanzisha Baraza la Wadhamini ambalo linatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watatu na wasiozidi watano.
Marekebisho mengine ni kuongeza idadi ya kanda kutoka kumi na moja za sasa hadi 13. Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na Serikali kuongeza mikoa mipya ya kijiografia.
Kanda mpya sasa zitakuwa Kagera/Geita, Arusha/Manyara, Kilimanjaro/Tanga, Katavi/Rukwa, Njombe/Ruvuma, Dodoma/Singida, Dar es Salaam, Shinyanga/Simiyu, Mwanza/Mara, Lindi/Mtwara, Kigoma/Tabora, Mbeya/Iringa na Pwani/Morogoro.
Ukiondoa mamlaka ya uteuzi aliyonayo Rais kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji huchaguliwa kwa kanda.
HESABU ZILIZOKAGULIWA
Mkutano Mkuu ulipitisha hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2010 (Audited Accounts) , na pia kuiteua kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya TAC Associates kuwa mkaguzi wa hesabu za TFF kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
YANGA YAOMBA RADHI MKUTANO MKUU
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambaye pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha klabu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Bhinda aliwaomba radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kitendo cha wachezaji wake kumpiga mwamuzi Israel Nkongo kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu.
Pia alimuomba Rais wa TFF, Leodegar Tenga kutoa msamaha wa adhabu ya kulipa faini iliyotolewa na Kamati ya Ligi ya TFF kwa wachezaji wawili wa Yanga ambao mpaka sasa hawajalipa faini hiyo.
Rais Tenga alimshukuru Bhinda kwa ujasiri alioonesha wa kuomba radhi mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kitendo kile. Aliongeza kuwa kwa vile yeye ni muumini wa kanuni, na adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni hawezi kutoa msamaha, hivyo wachezaji hao walipe faini hizo.
Pia Rais Tenga alisema binafsi haziingilia kamati za TFF katika uamuzi ambao zinafanya kwa vile zina watu waadilifu, na angekuwa yeye binafsi ndiye anayetoa adhabu, angetoa adhabu kali zaidi kwa vile vitendo vya kupiga waamuzi havikubaliki katika mchezo wa mpira wa miguu.
KANUNI ZA NIDHAMU, MAHAKAMA YA USULUHISHI
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Rais Tenga aliwaambia wajumbe kuwa Kanuni za Nidhamu (Disciplinary Code) za TFF na uundaji wa Mahakama ya Usuluhishi (Arbitration Tribunal) ya TFF ambacho ndicho kitakuwa chombo cha juu cha kutoa haki kwa masuala ya mpira wa miguu nchini vitakamilika mwaka huu.
Pia TFF itaendelea kutafuta wadhamini kwa ajili ya timu za Taifa za vijana na wanawake, itaendelea kuendesha semina na makongamano katika nyanja mbalimbali za mpira wa miguu, kutengeneza mtaala wa academy na kutengeneza mpango wa maendeleo (Comprehensive Plan) baada ya ule wa awali kumalizika mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

UBINGWA BADO WA MAN UNITED TU


Papers: Mancini backs Reds

23/04/2012 08:00
Roberto Mancini
Mancini: Put your money on UnitedManchester City boss Roberto Mancini saw his side claw their way back into the title race, then insisted: Put your money on United. City closed to within three points of Sir Alex Ferguson's Manchester United thanks to their win at Wolves and United's slip-up against Everton. Leaders United travel to the Etihad Stadium a week today, where victory for Mancini's men would put them back in the driving seat. But despite that, the Italian reckons the title remains an impossible dream. “I don't bet, I don't like it, but maybe you can put your money on Manchester United, 100 per cent,” said Mancini, while insisting he is not playing mind games. “Only one team can win this title. We have three points less and after the derby game we play Newcastle, who are fighting for the Champions League, and QPR, who are fighting relegation. I don’t think United are under pressure because they are used to this every year. For us it is different – it’s our first time. At the moment we don’t have any pressure because we don’t have any chance to win. It’s impossible. We will probably lose to United. Everyone wrote that the title race was finished seven days ago.”
Dave Armitage, Daily Star
City goalkeeper Joe Hart says City are ready for the Manchester derby: “We’ve always been focused on finishing the season well and we have given ourselves a really good chance. Our title chances are certainly a lot better than they were at the start of Sunday. We are excited, we feel ready, we are firing goals in. We are looking forward to it.”
All of the papers have already begun the countdown to the derby with many running Sir Alex's quote about it being "the biggest derby I've been involved in."

MCHEZAJI AZAM AFIA GESTI SINZA

Baadhi ya wachezaji wa Azam

RAIA wa Nigeria, Ferdinand Uzoma Onyenso(31), amekutwa amekufa katika chumba alichokuwa amepanga katika nyumba ya kulala wageni Fanaleki iliyopo Sinza wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mtu huyo alikutwa amekufa juzi saa 6:30 mchana katika chumba namba 110 huku maiti yake ikiwa imelala kitandani na haikuwa na jeraha lolote.
Kenyela alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Onyenso alikuja hapa nchini kwa ajili ya
shughuli za kimichezo kuchezea mpira wa miguu katika timu ya Azam FC iliyopo Ligi Kuu Tanzania Bara.
Alisema chumba chake kilipopekuliwa ilipatikana hati yake ya kusafiria namba A03512586 iliyotolewa nchini Nigeria pamoja na hati ya Uhamiaji iliyotolewa hapa nchini yenye namba 01767922.
Aidha alisema kuwa Onyenso alikuwa amepanga chumba hicho Aprili 20 na maiti yake imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa upelelezi zaidi.
Wakati huohuo, Mwandishi Timzoo Kalugira anaripoti kuwa klabu ya Azam imedai Onyenso si mchezaji wake na wala haimtambui.
Katibu Mkuu wa Azam, Nassoro Idrissa akizungumza na gazeti hili jana alisema kuwa wameshtushwa na taarifa hizo za polisi na kuomba ufanyike uchunguzi haraka ili kuweza kubaini ukweli halisi.
“Hatuna mchezaji kutoka Nigeria ambaye tunataka kumsajili, inawezekana kuna watu wanatumia jina la timu yetu au walimchukua huyo mchezaji kwamba asubiri baada ya ligi wamtafutie timu, pengine ndiyo wamemwambia watamleta Azam.
“Ni tukio la kusikitisha kibinadamu kwamba ametangulia mbele ya haki, lakini naomba uchunguzi ufanyike namna alivyoingia ili kubaini ukweli ni upi, lakini sisi Azam huwa mambo yetu tunapenda kuweka hadharani, huyo si mchezaji wetu,” alisema.


KOMBE LA YANGA KUGOMBEWA JUNI

Kikosi cha Yanga
MICHUANO ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ itafanyika jijini
Dar es Salaam, kuanzia Juni 23 hadi Julai 7 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amethibitisha kwamba michuano hiyo kwa mara nyingine tena itafanyika jijini Dar es Salaam, baada ya kufanyika kwa mafanikio zaidi mwaka jana.
Kwa mujibu wa Musonye, kufanyika kwa michuano hiyo nchini Tanzania ni kutokana kuwa na
uhakika wa udhamini mkubwa.
Bingwa mara 12 wa Ligi Kuu ya Rwanda na bingwa mara nne wa Kombe la Kagame, APR, ambayo imekiimarisha kikosi chake msimu huu, licha ya kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imejipanga kulitwaa kombe hilo kwa mara ya tano.
Mwaka jana APR na Etincelles zilitolewa hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Mwaka jana Yanga ilitwaa taji la michuano hiyo kwa kuifunga Simba kwa bao 1-0 hatua ya fainali, ambapo Yanga ilikuwa ikinolewa na Mganda Sam Timbe ambaye hilo lilikiwa ni taji lake la nne la Cecafa, baada ya kulibeba mwaka 2009 akiwa na Atraco, Polisi Uganda (2006)
na SC Villa (2005).
Rais Paul Kagame amekuwa akidhamini kombe hilo kwa zawadi za washindi kwa dola 60,000 sawa na shilingi 93,600,000.

SAMATTA AREJEA NA USHINDI MAZEMBE

Samatta katika game la jana
Some lessons from this 1-0 victory against the TPM Lupopo. The Ravens have established themselves with relative ease and can now focus on next Sunday's crucial match in the Champions League against Al Merreikh. Guy LUSADISU scored in the 53rd minute the only goal of the game on a low cross from defender Eric NKULUKUTA turf.A few days before the match against Al Merreikh, TPM was playing without suspended Rainford Kalaba, but recovered a Mbwana SAMATA back after an injury that had sidelined for three weeks.The physiognomy of the meeting was taking shape very quickly. The Crows monopolized leather and were walking in front of a team Lupopo folded in his own half.Tactics chosen by the Railwaymen in an attempt to limit the damage by not taking any risk in this part. Totaling more than 80% of possession, Lamine Ndiaye's men opened the path to the goal by SAMATA twice but each time the puncher was reported in position offside.Zero goals throughout the first 45 minutes late. The Ravens regained their ascent from the start of the second period, Nathan Sinkala relayed Patrick Ochan in midfield but the TPM was almost surprised at the 47th minute with a header MPIANA KIDIABA captured by net.LUSADISU on caviar "Papala"It was not until the 53rd minute to see, finally, the TPM take the lead. NKULUKUTA Eric did all the work on his right flank, the ball spun to Treasury MPUTU who played in one to two, thereby shifting to his teammate. NKULUKUTA overflowing right center chained a low shot LUSADISU turf, which, in the small rectangle, had only to put the leather into the net. The TPM deservedly led by 1-0.Mazembe as in training, passed around the leather very easily face a Lupopo unarmed.The coach Lamine eager to celebrate his first victory on Lupopo KANDA rose instead of SAMATA (65th) to intensify the offensive of the Ravens who let their opponent get away anyway after a double chance in the 79th minute, hitting Patrick Ilongo under the crossbar and the sequence of Singuluma on goalkeeper KIKANDA.Despite the rise of instead of Mihayo LUSADISU scorer, the game ended with the only offensive movement of Railway, but the strike was Carington's glove KIDIABA deflecting the ball for a corner.A well deserved victory that propelled the Ravens to head the partial classification, 16 points.Another resultDCMP-V. CLUB 0-1Purpose: MUTOMBO Diego (30 ')

CHRIS BROWN AIBUKA NA SWAGA ZA MBWA


Chris Brown's Selling Puppies Online Now

Add to Mixx!
Add to Yahoo! Buzz
ALTChris Brown is known for a lot of things: epic morning show freakouts, jaw-dropping dance moves, Twitter wars, and, oh yeah, that little Rihanna incident.

But now, add another thing: Dog breeder and salesman. Brown put seven puppies up for sale at the web site www.cbbreeds.webs.com. The price tag? $1,000 per pooch.

And the dogs are pretty darn adorable, with names like Precious, Pretty, Music and Beauty.

Sure, Brown hasn't had the best track record with dogs. Last year, he was accused of racing dogs in the hallway of his West Hollywood complex after residents complained he was "the neighbor from hell."

Won't you help these little guys find a nice home?

No comments: