KOCHA JUVENTUS AKAMATWA NA POLISI KWA KUPANGA MATOKEO, KAMBI YA ITALIA EURO 2012 YAVAMIWA
NAHODHA wa Lazio amekamatwa na
polisi kwa uchunguzi wa kupanga matokeo mchezoni.
Kiungo Stefano Mauri, mwenye
umri wa miaka 32, alishikiliwa kwa pamoja na kiungo wa zamani wa Genoa, Omar
Milanetto, polisi ilisema.
Kocha wa Juventus, Antonio
Conte, ambaye ameiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Serie A katika msimu wake
wa kwanza kazini, ni miongoni mwa waliohojiwa na polisi.
Maofisa wa Polisi walitembelea
pia kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Euro 2012 kumuhoji beki Domenico
Criscito, mwenye umri wa miaka 25.
Polisi walipekua nyumba zaidi
ya 30, zikiwemo za wachezaji, makocha na viongozi wa klabu za Serie A, Serie B
na madaraja ya chini zaidi.
Polisi ilisema Conte
alifanyiwa uchunguzi juu ya shaka ya kushiriki mchezo mchafu wa kupanga matokeo
mchezoni kati ya klabu yake ya awali, Siena na Novara, Aprili mwaka 2011. Watu
wengine watano walikamatwa pia nchini Hungary kwa kuhisiwa kuwa sehemu ya
mchezo huo mchafu, unaopigwa vita kali.
MILIONEA WA YANGA ANENA BUSARA TUPU
Bin Kleb akimkabidhi jezi Haruna Niyonzima baada ya kumsajili mwaka jana mjini Kigali 'kwa bei chafu' kutoka APR ya Rwanda |
MDAU wa soka nchini, Abdallah
Ahmed Bin Kleb ameomba ijitokeze kampuni ya kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu ya
soka Tanzania Bara, ili kuwawezesha kujimudu na kufanya kazi zao kwa ufanisi
zaidi.
Akizungumza na BIN
ZUBEIRY usiku huu, Bin Kleb aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya
Yanga, kabla ya kujiuzulu alisema kwamba marefa wa Tanzania wanafanya kazi
katika mazingira magumu na wanalipwa posho kidogo mno na TFF.
“Nasikia wanalipwa Sh. 70,000,
hizi ni fedha kidogo sana, haziwezi kuwatosheleza kujikimu, naomba ijitokeza
kampuni maalum, kwa ajili ya kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu, kwa sababu kwa
kufanya hivyo kampuni zitanufaika kwa sababu watatangazwa
kibiashara,”alisema.
Bin
Kleb alisema kwamba, wakati mwingine watu wanakosea kuwatupia shutuma nyingi
waamuzi kwamba wanapenda rushwa, ingawa hutokea hatakwa waamuzi walio waadilifu
wakaingia kwenye mitego kwa sababu ya hali halisi inayowakabili.
Aidha, Bin Kleb alisema
anastaajabishwa mno na vyombo vya habari nchini, kuelekeza nguvu zao katika
mechi za Ligi Kuu zinazochezwa Dar es Salaam pekee, wakati mikoani ndiko kuna
mambo mengi ‘ya ajabu’.
“Unakuta Televisheni
zinaonyesha mechi za Dar es Salaam pekee, wakati huko mikoani ndiko kuna mambo
ya ajabu kweli kweli, ambayo yanatakiwa yaripotiwe ili yakomeshwe, kwa hivyo
natoa haya mawili kama changamoto kwa maslahi ya soka yetu,”alisema Bin
Kleb.
CECH ASAINI MKATABA MPYA CHELSEA MIAKA MINNE
Cech |
KIPA
wa Chelsea, Petr
Cech amemwaga wino akitia saini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu
hiyo bingwa Ulaya kwa miaka minne zaidi.
Kipa huyo wa kimataifa wa Czech, alijiunga na The Blues mwaka 2004, akitokea Rennes Ufaransa kwa dau la pauni Milioni 9 na hadi sasa amedaka mechi 369 katika klabu hiyo, akiiwezesha kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, manne ya FA, mawili ya Carling na moja la Ligi ya Mabingwa na sasa atakuwa Stamford Bridge hadi mwaka 2016.
Kipa huyo wa kimataifa wa Czech, alijiunga na The Blues mwaka 2004, akitokea Rennes Ufaransa kwa dau la pauni Milioni 9 na hadi sasa amedaka mechi 369 katika klabu hiyo, akiiwezesha kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, manne ya FA, mawili ya Carling na moja la Ligi ya Mabingwa na sasa atakuwa Stamford Bridge hadi mwaka 2016.
"Ninafurahi mno kuwa ni sehemu
ya klabu hii maarufu kwa kipindi cha miaka mine zaidi," alielezea mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 30.
"Ninatumaini miaka hiyo minne
ijayo itakuwa ni sawa na miaka minane ambayo nimekuwa nikikichezea
klabu."
Cech, ambaye mkataba wake wa
awali ulikuwa umalizike mwaka ujao, ni mchezaji muhimu kwa Chelsea
Cech pia alitangazwa kama
mchezaji bora zaidi wa Chelsea mwaka jana, 2010/11.
"Chelsea inatambua kikamilifu
mchango muhimu kutoka kwa Petr wakati huu wa klabu kupata ufanisi wake mkubwa
zaidi katika historia yake," alielezea mkurugenzi mkuu wa Chelsea, Ron
Gourlay.
Kipa msaidizi wa Cech, Thibaut
Courtois kutoka Ubelgiji, huenda akaachiwa mechi zaidi za ligi kuu ya Premier
ili kujinoa zaidi, baada ya kuonyesha uhodari wake akiwa mchezaji wa mkopo
katika klabu ya Uhispania ya Atletico Madrid, ijapokuwa kijana huyo wa miaka 20
huenda akaazimwa kwa timu nyingine kwa muda mfupi.
Courtois alijiunga na Chelsea
kutoka klabu ya Racing Genk, mwezi Julai mwaka jana, na kwa kuelekea Uhispania
na kutofungwa, aliiwezesha klabu ya Atletico Madrid kuibuka mabingwa wa klabu ya
Europa mapema mwezi huu.
VIWANJA VYA EURO 2012 NA WASIFU WAKE
Euro 2012: Viwanja na maelekezo Fainali za Mataifa ya Ulaya...
FAINALI za Kombe
la Mataifa UlayaThe 2012 zitachezwa katika viwanja nane, vinne nchini Poland na
vinne Ukraine.
Viwanja
vitano vipya vimetengenezwa maalum kwa ajili ya michuano hiyo - na vingine
vitatu vimefanyiwa ukarabati wa uhakika.
Fainali
hizo zinaanza Juni 8 kwa wenyeji washiriki Poland kufungua dimba na Ugiriki
katika Uwanja wa Taifa wa Warsaw, na kufikia tamati Julai 1katika Uwanja wa
Olimpiki mjini Kiev, Ukraine.
Hapa
BIN ZUBEIRY kwa msaada wa BBC Sport inakuletea viwanja ambavyo
vitatumika kwa fainali hizo na wasifu wake.
Warsaw
KUJENGWA: 2011,
WANAOUTUMIA:
Timu ya
taifa Poland
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Mechi tatu za Kundi A, ya ufunguzi kati ya Poland
Ugiriki Juni 8, Poland na Urusi Juni 12, na Ugiriki na Urusi Juni 16.
UMBALI:
Kutoka Kiev: Kilomita 820.
Wroclaw
KUJENGWA: 2011
WANAOUTUMIA: Slask
Wroclaw
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi
A
UMBALI:
Kutoka Warsaw: kilomita 350 na
kutoka Kiev kilomita 1,090.
Gdansk
KUJENGWA: 2011
WANAOUTUMIA: Lechia
Gdansk
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi
C.
DUMBALI:
Kutoka Warsaw: Kilomota 345 na kutoka Kiev kilomita 1,190.
Poznan
KUJENGWA: 1980
(Kukarabatiwa 2010)
WANAOUTUMIA: Lech
Poznan na Warta Poznan
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi C
UMBALI:
Kutoka Warsaw: Kilomita 320 na kutoka Kiev kilomita 1,140.
Kiev
KUJENGWA: 1923
(Kukarabatiwa 2011)
WANAOUTUMIA:
Timu ya taifa ya Ukraibe.
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi
D
UMBALI:
Kutoka Warsaw: kilomita 820.
Donetsk
KUJENGWA: 2009
WANAOUTUMIA: Shakhtar
Donetsk
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi
D
UMBALI
kutoka Kiev: Kilomita 700 na kutoka Warsaw
kilomita 1,465.
Kharkiv
KUJENGWA: 1926
(Kukarabatiwa 2009)
WANAOUTUMIA: FC
Metalist Kharkiv
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi B.
UMBALI:
Kutoka Kiev kilomita 480 na kutoka Warsaw
kilomita 1,250.
Lviv
KUJENGWA: 2011
WANAOUTUMIA: FC
Karpaty Lviv
MECHI
ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi B
UMBALI:
Kutoka Kiev kilomita 540 na kutoka Warsaw
kilomita 385.
GARETH BARRY AENGULIWA ENGLAND KIKOSI CHA EURO
KIUNGO
Gareth Barry ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya Euro 2012,
kwa sababu ya majeruhi ya nyonga, Chama cha Soka
kimethibitisha.
Kiungo huyo
England mwenye umri wa miaka 31, alifanyiwa vipimo mapema leo, ambavyo
vimethibitisha ana maumivu makubwa.
"Ninasikitishwa
sana kumpoteza Gareth," alisema kocha Roy Hodgson. "Nina uhakika ataendelea kuwa
sehemu ya kikosi cha England baada ya Euros."
Hodgson
amemuita beki wa Everton, Phil Jagielka kuchukua nafasi ya
Barry.
"Kikosi cha
mwisho cha England cha wachezaji watatu lazima iwe kimewasilishwa kwa ajili ya
fainali hizo za Poland na Ukraine mchana wa kesho.
Barry,
ambaye ameichezea tmu ya taifa mechi 50, alilazimika kutoka nje baada ya dakika
30 tu baada ya kuingia akitokea benchi katika mechi ya kirafiki na Norway mjini
Oslo, Jumamosi.
Uamuzi wa
Hodgson kumuita Jagielka unaweza kumfanya Phil Jones ahamie kwenye nafasi ya
kiungo, ambako aliwahi kucheza wakati katika klabu yake, Manchester United
mwishoni mwa msimu.
Bado
wachezaji Danny Welbeck na Glen Johnson, ambao wamepona hivi karibuni maumivu ya
kifundo cha mguu wanaangaliwa afya zao, na wawili hao wanatarajiwa kuwasili
kambini, Watford kesho.
Scott Parker
pia alikuwa majeruhi, lakini amethibitisha yuko fiti akitokea benchi dakika ya
55 katika mechi ya ushindi wa England wa 1-0 dhidi ya Norway mwishoni mwa
wiki.
MISS DAR INTER COLLEGE MAZOEZINI
TEVEZ ATAKIWA KWA UDI NA UDUMBA AC MILAN
Monday's gossip column
IVANOVIC AITAMANI OFA YA REAL MADRID, LAKINI...
BEKI wa Chelsea, Branislav
Ivanovic, mwenye umri wa miaka 28, anavutiwa na ofa ya mabingwa wa Hispania,
Real Madrid ingawa amesema anafurahi kubaki Stamford Bridge.
WAKALA
wa mchezaji anayetakiwa na klabu ya Manchester City, Thiago Silva, mwenye umri
wa miaka 27, amesema beki huyo anaweza kukubali kuondoka San Siro ikiwa AC Milan
itataka kumuuza.
KLABU
ya AC Milan inataka kumsajili mshambujliaji wa Manchester City, Carlos Tevez,
mwenye umri wa miaka 28, baada ya kukwama kumsajili Muargentina huyo
Januari.
KOCHA
aliyekalia kuti kavu Blackburn, Steve Kean anataka kumsajili kinda wa Manchester
United, mwenye umri wa miaka 19, pacha Michael Keane kwea mkopo wakati Rovers
ikijiandaa na Ligi Daraja la Kwanza.
MSHAMBULIAJI
wa Manchester City, Sergio Aguero, mwenye umri wa miaka 23, kwa dau la pauni
Milioni 50 anawaniwa na klabu ya Real Madrid, lakini amegoma kuhama Etihad.
"Maisha yangu yapo Manchester City. Nataka kubaki hapa," alisema.
MSHAMBULIAJI
wa Arsenal,
Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, amethibitisha yupo kwenye mazungumzo
na klabu kadhaa juu ya mpango wa kuhama Emirates.
HODGDON KWENDA BRAZIL
KOCHA
wa England, Roy Hodgson amejipanga sawa sawa kwa ajili ya Fainali za Kombe la
Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 ili afanye vizuri na kujitengenezea mazingira ya
kuwa kocha wa muda mrefu wa timu hiyo.
KOCHA
wa England, Roy Hodgson atasafiri kwenda Brazil moja kwa moja baada ya
mashindano ya Euro 2012, kwenda kukagua sehemu ambayo itafaa kwa Three Lions
kuweka kambi ya kujiandaa na Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini
humo.
BEKI
wa Fulham, raia wa Norway, Brede Hangeland, mwenye umri wa miaka 30, amesema
wachezaji wa England wanatakiwa kudhihirisha ubora wao kwenye Euro 2012, baada
ya msimu mrefu wa mafanikio.
NYOTA
Scott Parker, mwenye umri wa miaka 31, amezungumzia anavyojisikia vizuri baada
ya kuwa fiti kwa ajili ya kuiwakilisha England kwenye Euro 2012, baada ya
kuumizwa na klabu yake kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu
ujao.
KIUNGO
Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 33, anakabiliwa na mkanganyiko wa mawazo
kwenye Euro 2012 baada ya kocha wa England, Roy Hodgson kuamua chaguo lake la
kwanza katika safu ya kiungo ya timu ni Steven Gerrard na Scott
Parker.
BEKI
wa zamani wa Arsenal na Tottenham, Sol Campbell amewaonya mashabiki wa England
kutokwenda kwenye fainali za Euro 2012, kwa sababu wanaweza kurejea na
maumivu.
NYOTA
wa Tottenham, mwanaoska wa kimataifa wa Mexico, Giovani Dos Santos, mwenye umri
wa miaka 23, anaweza akaomba kuondoka, vinginevyo ahakikishiwe kuchezeshwa
kwenye Uwanja wa White Hart Lane.
KLABU
ya Liverpool itafanya mazungumzo na kocha wa Swansea, Brendan Rodgers katika
kukamilisha msako wao wa kumtafuta mrithi wa Kenny Dalglish.
MMILIKI
wa Wigan, Dave Whelan yuko tayari kutimiza masharti ya kocha Roberto Martinez,
ili kumzuia asihamie Liverpool au Aston Villa.
THE
Latics wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Waandishi wa Habari, ili Martinez
aseme kama atapenda kubaki au kuondoka.
MUGABE CHELSEA DAMU
RAIS
wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema yeye ni shabiki wa Chelsea tangu klabu hiyo
ya London, itwae taji la Ligi ya Mabingw3a Ulaya kwa kuifunga Bayern
Munich.
SERENGETI YAZIDI KUWANUFAISHA WATANZANIA
Mshindi wa Bajaj bw Godfery
Shao ndani ya bajaj akipongezwa na wafanyakazi, wawakilishi, wapenzi na wadau wa
kampuni ya bia ya Serengeti baada ya kukabidhiwa bajaj mpya
kabisa
|
Sunday, May 27, 2012
DROGBA AONGOZA ORODHA YA WAAFRIKA BORA 20 KUWAHI KUCHEZA ENGLAND
Didier Drgoba, ambaye SuperSport.com imempa namba moja katika orodha ya wanasoka bora 20 wa Afrika waliowahi kucheza Ligi Kuu ya England, ikitimiza miaka 20 mwaka huu. Tazama orodha kamili chini. |
1. Didier Drogba - Ivory Coast (Chelsea)
2. Nwankwo Kanu - Arsenal (West Brom, Portsmouth)
3. Michael Essien - Ghana (Chelsea)
4. John Obi Mikel - Nigeria (Chelsea)
5. Tony Yeboah - Ghana (Leeds)
6. Lucas Radebe - South Africa (Leeds)
7. Emmanuel Eboue - Ivory Coast(Arsenal)
8. Austin Jay-Jay Okocha - Nigeria (Bolton)
9. Lauren Etama-Mayer - Cameroon (Arsenal)
10. Stephen Pienaar - South Africa (Everton, Tottenham Hotspur)
11. Kolo Toure - Ivory Coast (Arsenal, Manchester City)
12. Yaya Toure - Ivory Coast (Manchester City)
13. Alex Song - Cameroon (Arsenal)
14. Peter Ndlovu - Zimbabwe (Coventry)
15. Papiss Demba Cisse - (Newcastle)
16. Yakubu Aiyegbeni – Nigeria (Portsmouth, Middlesbrough, Everton, Blackburn Rovers)
17. Emmanuel Adebayor - Togo (Arsenal, Manchester City, Tottenham)
18. Joseph Yobo - Nigeria (Everton)
19. Bruce Grogbelaar - Zimbabwe (Liverpool, Southampton)
20. Peter Osaze Odemwingie - Nigeria (West Brom)
POULSEN MDOGO AOMBA APEWE MUDA STARS
Kim Poulsen |
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema timu yake inaweza kufanya
vizuri, lakini lazima wapewe muda. Gazeti la Habari Leo, limeandika leo kwamba kutokana na hali hiyo amewaomba mashabiki nchini kuwa wavumilivu na kwamba ipo siku wataikubali na kuanza kuwashangilia wachezaji. “Ni mwanzo mzuri wa safari yangu, kutoka sare nadhani ni mwanzo mzuri, sio matokeo mabaya kwangu na wala sio matokeo mabaya kwa Malawi, nahitaji kupewa muda zaidi,”alisem Kim baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Stars na Malawi juzi uliomalizika kwa timu hizo kutofungana. Alisema amefurahishwa na kiwango ambacho timu yake ilikionesha na kuomba kupewa muda zaidi ili ifanye vizuri kwani kikosi chake bado ni kichanga na kinaundwa na wachezaji wengi chipukizi hivyo hawezi kuibadilisha timu hiyo kipindi cha wiki moja tokea aanze kuifundisha timu hiyo. Kocha huyo aliyekuwa akifundisha timu za taifa za vijana aliwataka wachezaji wa timu hiyo kucheza vizuri muda wote ili kuwanyamazisha mashabiki wachache waliokuwa wakiizomea kwenye mchezo huo. “Ukiona mashabiki wanazomea ujue bado haujawafurahisha, nafikiri wakicheza vizuri hawatazomewa, naelewa hisia za mashabiki kuwa wanataka timu ishinde na ichezea vizuri lakini hilo lisipotokea ni wazi watazomea,”alisema Kim. Taifa Stars itacheza na timu ya Taifa ya Ivory Coast Juni 2 huko Abdijani kujiandaa na mchezo wa awali wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia. Mbali na miamba hiyo ya soka ya Afrika Magharibi Stars iko kundi moja na Gambia na Morocco. |
MAANDAMANO YA SHEREHE ZA UBINGWA SIMBA YALIVYOKUWA
Baadhi
ya wachezaji wa Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao wakati wakipita
katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam leo.
Mashabiki
na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika maandamano kuelekea katika Ukumbi wa Dar
Live kusherehekea ubingwa wa timu yao leo.
Pikipiki
zikiongoza msafara huo kuelekea Dar Live.
Maandamano
yakipita katika mitaa leo.
Mashabiki
wa Simba wakimuenzi kiungo wa timu hiyo, Marehemu Patrick Mafisango aliyefariki
katika ajali ya gari hivi karibuni.
Mashabiki
wakishangilia wakati wa maandamano hayo.
Wachezaji
na mashabiki wa Simba wakipozi na kombe lao.
Mashabiki
wa Simba wakiingia ndani ya Ukumbi wa Dar Live tayari kwa sherehe za
ubingwa.
(Picha
na Issa Mnally /GPL)
MATOKEO MECHI ZA KIRAFIKI ZA KIMATAIFA HADI LEO DUNIA NZIMA
Landon Donovan (10) wa Marekani akimtoka Scott Brown wa Scotland, kulia, kipindi cha kwanza katika mechi ya kirafiki ya kimataifa jana, mjini Jacksonville, Fla. Marekani ilishinda 5-1. |
27 May 2012 | |||
Fifa Internationals | |||
Tunisia | 5 - 1 | Rwanda | Monastir |
Albania | 1 - 0 | Iran | Istanbul |
Oman | 1 - 1 | Lebanon | Muscat |
Honduras | 0 - 1 | New Zealand | Dallas |
USA | 5 - 1 | Scotland | Jacksonville |
El Salvador | 2 - 0 | Moldova | Houston |
26 May 2012 | |||
Fifa Internationals | |||
Algeria | 3 - 0 | Niger | Blida |
Norway | 0 - 1 | England | Oslo |
Greece | 1 - 1 | Slovenia | Kufstein |
Czech Republic | 2 - 1 | Israel | Graz |
Netherlands | 1 - 2 | Bulgaria | Amsterdam |
Finland | 3 - 2 | Turkey | Salzburg |
Cameroon | 2 - 1 | Guinea | Metz |
Spain | 2 - 0 | Serbia | St Gallen |
Switzerland | 5 - 3 | Germany | Basel |
Portugal | 0 - 0 | Macedonia | Leiria |
Poland | 1 - 0 | Slovakia | Klagenfurt |
Republic of Ireland | 1 - 0 | Bosnia-Herzegovina | Dublin |
Brazil | 3 - 1 | Denmark | Hamburg |
Mozambique | 0 - 0 | Namibia | Maputo |
Burkina Faso | 2 - 2 | Benin | Malabo |
Tanzania | 0 - 0 | Malawi | Dar Es Salaam |
Costa Rica | 3 - 2 | Guatemala | San Jose |
25 May 2012 | |||
Fifa Internationals | |||
Morocco | 0 - 1 | Senegal | Marrakech |
Belgium | 2 - 2 | Montenegro | Brussels |
Croatia | 3 - 1 | Estonia | Rijeka |
Russia | 1 - 1 | Uruguay | Moscow |
24 May 2012 | |||
Fifa Internationals | |||
Georgia | 1 - 3 | Turkey | Salzburg |
Japan | 2 - 0 | Azerbaijan | Shizuoka |
Peru | 1 - 0 | Nigeria | Lima |
El Salvador | 2 - 2 | New Zealand | Houston |
Venezuela | 4 - 0 | Moldova | Puerto Ordaz |
22 May 2012 | |||
Fifa Internationals | |||
Albania | 2 - 1 | Qatar | Madrid |
Poland | 1 - 0 | Latvia | Klagenfurt |
Egypt | 3 - 0 | Togo | Khartoum |
International Friendly | |||
Bayern Munich | 3 - 2 | Netherlands | Munich |
No comments:
Post a Comment