Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika ufunguzi wa jengo la ofisi za sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya kusini lililopo mjini Mtwara. |
Makamu wa Rais wa Tanzania-Samia Suluhu Hassan akiwa na waziri wa nchi utumishi na utawala bora-Angela Kairuki na mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego |
Juma Mohamed, Mtwara
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhakikisha fomu za viapo vya
uadilifu na kutangaza mali, zinajazwa na viongozi kuanzia ngazi za chini ikiwa
ni pamoja na vijiji na kata.
Akizungumza
mkoani hapa katika ufunguzi wa jengo la ofisi ya sekretarieti ya maadili ya
viongozi wa umma kanda ya kusini, amesema wapo viongozi wa ngazi za chini ambao
wanajilimbikizia mali huku akimtaja diwani mmoja wa mkoa wa Lindi ambaye
amekamatwa akisafirisha korosho tani Nne visivyo halali.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego. |
“Lakini
nataka nikuambie kamishna, sisi mnaotuletea fomu tutangaze mali zetu hatuna
chochote kuliko hawa wa chini..huku chini kuna watu wamejilimbikizia mali
nyingi na itabidi zile fomu tunazojaza sisi mjipe mzigo mkubwa zaidi ziende
chin zaidi watu wajaze watangaze mali zao na muwakague..” alisema.
Naye, waziri
wa nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angela Kairuki, amewataka
watanzania wote kujiamini na kuitumia ofisi hiyo iliyowekwa kwa ajili ya kukuza
maadili ya viongozi wa umma.
“Kupitia
kwako mhe. Makamu wa Rais, mimi niendelee kuomba hadhara hii pamoja na
watanzania wote wanaotusikiliza, tujiamini ofisi hii ni yenu imewekwa kwa ajili
yenu katika kuhakikisha tunatunza maadili ya viongozi wa umma, katika
kuhakikisha hakuna ubadhirifu wa mali za umma..” alisema Kairuki.
Akitoa
taarifa ya jengo hilo, kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Jaji Mstaafu
Salome Kaganda ameeleza idadi ya viongozi waliorejesha matamko yao ya
rasilimali na madeni kuwa ni 1,286 mpaka mwezi Juni mwaka huu.
Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma nchini, Jaji Mstaafu Salome Kaganda, akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi za sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya kusini. |
Makamu wa
Rais yupo mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo baada ya uzinduzi
wa jengo hilo lililojengwa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2.1,
anatembelea kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba kabla ya kumalizia
ziara yake wilayani Tandahimba.
No comments:
Post a Comment