Wazee Newala ‘wamlilia’ DC
kusuluhisha mgogoro wa vijiji Vitatu kuhusu uhaba wa maji.
Juma Mohamed, Mtwara
Kero ya maji
iliyodumu kwa miaka 12 katika vijiji vya Mnali na Mapinduzi wilayani Newala
mkoani Mtwara, imezua mgogoro baina ya wananchi wa vijiji hivyo na kijiji cha
Nanda, na kupelekea wananchi hao kuanza kupeana vitisho hali ambayo imezua hofu
kwa wazee wa vijiji hivyo.
Juma
News ilifika katika
vijiji hivyo na kufanikiwa kuzungumza na wazee hao ambao wanadai kuwa hali ya
usalama inaelekea kuwa mbaya kutokana na vitisho vinavyotolewa na vijana wa
vijiji hivyo, na kuamua kumuomba mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo
kukaa na wazee wa vijiji vyote ili kusuluhisha mgogoro huo.
Afisa tarafa
ya Kitangali, Victoria Fredy, alitoa ushuhuda wa kijana mmoja ambaye hakumtaja
jina aliyeamua kuchukua Upupu wa kuwasha na kummwagia meneja wa Maji wakiwa
katika shughuli ya kurekebisha miundombinu ya maji.
Mkuu wa
wilaya ya Newala Aziza Mangosongo, ambaye amefanikiwa kumaliza tatizo hilo la
maji baada ya kuweka kambi ya siku Tatu akiwa na timu yake, alikiri kuwapo kwa
hujuma zilizokusudia kukwamisha upatikanaji wa maji katika vijiji vya Mnali na
Mapinduzi na kuahidi kukaa na wazee ili kumaliza tofauti zilizopo.
Wananchi wa
Mnali na Mapinduzi wameamua kumpa zawadi mbalimbali mkuu wa wilaya kutokana na
kufanikisha upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo.
No comments:
Post a Comment