Ndanda FC waiduwaza Azam Nangwanda Mtwara
Heka heka langoni mwa Azam, wakati Ndanda waliposawazisha bao kupitia kwa mshambuliaji Omary Mponda katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Ndanda walishinda 2-1. |
Nahodha wa Ndanda, Kigi Makasy akiwatambulisha wachezaji wenzake kwa katibu tawala wa mkoa wa Mtwara-Alfred Luanda. |
Kikosi cha Ndanda FC kilichoanza katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. Ndanda walishinda magoli 2-1. |
|
JUMA MOHAMED, MTWARA.
Ndanda FC
leo hii wameiduwaza Azam katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara katika
mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufunga magoli 2-1
Azam
walianza kupata bao la kuongoza katika dakika ya saba likifungwa na Francisco
Zekumbawira, kabla ya Omary Mponda kuisawazishia Ndanda dakika ya 41 na baadae
Riphat Khamisi kufunga bao la ushindi kwa shuti kali dakika ya 84.
Mshambuliaji wa Ndanda FC, Omary Mponda akijaribu kumtoka mlinzi wa Azam FC David Mwantika ktika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Nangwanda Sijaona Mtwara. Ndanda walishinda 2-1 |
Manaodha wa
timu zote mbili wamezungumza baada ya mchezo huo ambapo Nahodha wa Azam John
Bocco anasema wamekubali matokeo na sasa wanajipanga kwa michezo inayofuata,
huku nahodha wa Ndanda Kigi Makasy, akiwataka mashabiki kuzidi kuwaunga mkono
katika michezo yao.
Huo ni
mchezo wa pili kwa Ndanda kupata ushindi, baada ya wiki iliyopita kuwafunga
majimaji ushindi kama huo wa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika mjini Songea.
No comments:
Post a Comment