Choo kinachotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Magomeni, manispaa ya Mtwara Mikindani. |
Na Juma
Mohamed, Mtwara.
Shule ya
msingi Magomeni iliyopo manispaa ya Mtwara Mikindani inakabiliwa na changamoto
ya uhaba wa miundombinu ikiwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vinane vya
madarasa, matundu ya vyoo pamoja na ukosefu ya nyumba za walimu.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa jengo la vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya
walimu kutoka kwa Benki ya Stanbic, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Rashid Kajonjo,
alisema licha ya msaada huo uliombatana na sare za wanafunzi, bado wanahitaji
wadau kuwasaidia Zaidi.
“kimsingi
tuna upungufu wa madarasa Manane kwa sasa kati ya madarasa 16 tunayohitaji
lakini tuna upungufu wa ofisi moja ya walimu lakini hatuna nyumba hata moja
katika eneo hili walimu wote wanatoka nje ya eneo hili sasa inakuwa ni hatari
kidogo kwa usalama..” alisema Kajonje.
Baadhi ya
wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo, wameshukuru msaada huo na kuwaomba
wadau wengine wazidi kusaidia shule hiyo, huku mkuu wa kitengo cha mawasiliano
wa Benki hiyo, Desderia Mwegelo akizungumza kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu
Ken Cockerill, ameahidi kuendelea kuisaidia shule hiyo.
“tunaomba na
serikali ya Jamhuri ya Muungano akiwemo na Rais John Pombe Magufuli Mungu ampe
maisha marefu kwakweli, azidi kutuunga mkono kwakweli azidi kutusaidia hiki
alichokitoa azidishe hapa wakiwemo wadau, wadahamini na wawekezaji wanaokuja
Tanzania kwa vile mkoa wa Mtwara tunawaombea kwakweli..” alisema Aisha Mwidini.
“Tumekuja kuzindua
rasmi boksi mbili za madarasa na ofisi ya mwalimu mkuu, pia kuna michango
kadhaa ilikuwa imeletwa na wafanyakazi wa Stanbickwa ajili ya kuwezesha ununuzi
wa sare za shule kwa wananfunzi wa Magomeni Primary..” alisema Desderia
Mwegelo.
Kwa upande
wake, mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amemwagiza mkurugenzi wa manispaa
hiyo kusimamia ujenzi wa chumba kimoja cha darasa ambacho amepiga marufuku
kutumika kutokana na kuwa na nyufa, huku akiwataka wazizi kushiriki kwa kutoa
michango katika ujenzi wa vyoo.
“Nimwagize
mkurugenzi ndani ya siku saba pale ni padogo sana, awe amekarabati darasalile
kabla ya watoto kuingia darasani..mkuu wa shule umenisikia watoto wasiingie,
mkurugenzi umenisikia ndani ya siku saba mimi na DC tutakuja kukagua lile
darasa.” Aliagiza Dendego.
Aidha,
aliendesha zoezi la harambee ya kuchangia ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa shule
hiyo ambapo aliwaamuru wazazi na walezi waliokusanyika shuleni hapo kwa kumtaka
kila mmoja achangie alichonacho.
Mkoa huo
umetekeleza agizo la kutatua changamoto ua uhaba wa madawati kwa shule za
msingi kwa Zaidi ya asilimia 100, kutokana na kuwa na ziada ya madawati 265.
No comments:
Post a Comment