JOEY BARTON ATOLEWA KWA MKOPO DARAJA LA KWANZA HUKO
KLABU ya Queens Park Rangers
inataka kumtoa kwa mkopo kiungo mtukutu, Joey Barton, mwenye umri wa miaka 29,
kwenda klabu ya Daraja la Kwanza, na Blackburn ndio inaongoza mbio za kumnasa
mchezaji huyo.
KLABU
ya Fulham inatumai pauni Milioni 9 pamoja na Clint Dempsey, mwenye umri wa miaka
29, zitatosha kwa Liverpool kumruhusu mshambuliaji Andy Carroll, mwenye umri wa
miaka 23, ahamie Craven Cottage.
KLABU
ya Liverpool imekubali dili la pauni Milioni 12 kumnasa Fabio Borini, mwenye
umri wa miaka 21, awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha wao mpya, Brendan
Rodgers, na Mtaliano huyo anatarajiwa kukamilisha usajili wake mwishoni mwa
wiki.
KUSAJILIWA
kwa Fabio Borini kutahitimisha zama za Craig Bellamy katika Uwanja wa Anfield,
na QPR na Cardiff zote zinaiwania saini ya mshambuliaji huyo wa Liverpool.
KLABU
ya Tottenham inaelekea kuwapiga bao Arsenal katika kuwania saini ya mshambuliaji
wa Atletico Madrid, Adrian Lopez, mwenye umri wa miaka 24, na wako tayari kutoa
dau la pauni Milioni 15 kumaliza suala lake.
KOCHA
wa Porto, Vitor Pereira amesema kwamba Tottenham inamtaka Joao Moutinho, mwenye
umri wa miaka 25, lakini amesistiza klabu hiyo ya White Hart Lane itatakiwa
kulipa pauni Milioni 31.5 kumnasa kiungo huyo.
BEKI
wa Manchester City, Kolo Toure, mwenye umri wa miaka 31, anatakiwa na Bursaspor,
na klabu hiyo ya Uturuki iko tayari kulipa pauni Milioni 6, kwa mchezaji huyo
ambaye alisajiliwa kwa dau la pauni Milioni 16 mwaka 2009.
KLABU
ya Southampton inatumai kumnasa beki wa kulia wa Crystal Palace, Nathaniel
Clyne, mwenye umri wa miaka 21.
FERGUSON KUTUA NOTTNGHAM
MMILIKI
mpya wa klabu ya Nottingham Forest, anamtaka kocha wa Peterborough, Darren
Ferguson, mwenye umri wa miaka 40, aifundishe timu hiyo baada ya kumfukuza Steve
Cotterill.
MCHEZAJI
wa West Ham, Ricardo Vaz Te, mwenye umri wa miaka 25, anatafakari mustakabali
wake katika klabu ya West Ham, baada ya kukwama kwa ombi lake la nyongeza ya
mshahara.
Kyle
Walker, mwenye umri wa miaka 22, amesema kwamba chumba cha kuvalia nguo cha
Tottenham kitampa fursa ya mafanikio kocha mpya wa klabu hiyo, Andre Villas-Boas
katika Uwanja wa White Hart Lane. "Anaenda kutupa nafasi, nasi tunaenda kumpa
nafasi. Matumaini ni kufanhya vema na kutwaa mataji."
No comments:
Post a Comment