Rais JK akizungumza leo jijini London na wachezaji na maafisa wa timu ya taifa itakayoshiriki Olimpiki. |
JK akiteta leo jijini London na Balozi Kallaghe wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa itakayoshiriki Olimpiki. |
LIVERPOOL YAONA BORA HASARA KULIKO GALASA
Tetesi za Alhamisi magazeti ya Ulaya
LIVERPOOL YAKUBALI HASARA KULIKO GALASA
KLABU ya Liverpool iko
tayari kupoteza pauni Milioni 25 kwa mshambuliaji Andy Carroll, kwa mshambuliaji
huyo kurejeshwa Newcastle kwa dau la pauni Milioni 10.
KOCHA
mpya wa Tottenham, Andre Villas-Boas anamtaka kiungo wa Porto, Joao Moutinho
kama mbadala wa Luka Modric. Modric anatarajiwa kuondoka White Hart Lane na
Spurs iko tayari kumchukua Moutinho, ambaye aling'ara katika Euro 2012 akiwa na
kikosi cha Ureno.
MSHAMBULIAJI
wa Porto, Hulk amekanusha kwamba yupo karibu kusaini Chelsea. Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 25, ambaye yumo kwenye kikosi cha Olimpiki cha Brazil,
anafurahi kubaki Ureno.
KLABU
ya Reading inajiandaa kutoa pauni Milioni 5 kumchukua mshambuliaji wa Tottenham,
Jermain Defoe.
KLABU
za West Brom na Aston Villa, zote zinamtaka kiungo wa Rennes, Tongo
Doumbia.
KLABU
ya Brighton imenza maongezi na Arsenal juu ya kumchukua kwa mkopo beki kinda,
Ignasi Miquel, lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Barcelona B.
KLABU
ya Newcastle imejitosa kwenye mbio za kuwania saini ya winga wa Blackburn,
Junior Hoilett - ambaye amemaliza mkataba wake Ewood Park - baada ya pendekezo
lake la kwake Borussia Monchengladbach kufeli.
MSHAMBULIAJI
wa Tottenham, Rafael van der Vaart anaweza kuondoka kwenda kujiunga na klabu
moja Falme za Kiarabu (UAE), baadea ya dili lake la kuhamia Hamburg
kushindikana.
CAPELLO KUPEWA URUSI
KOCHA
wa zamani wa England, Fabio Capello yupo kwenye nafasi nzuri ya kuchukua nafasi
iliyo wazi ya Ukocha wa timu ya taifa ya Urusi, baada ya Harry Redknapp kuamua
mwenyewe kujiondoa.
KOCHA
wa Wales, Chris Coleman amesema kwamba winga Gareth Bale hayuko fiti kucheza
Olimpiki.
KIUNGO
mkongwe, David Beckham hatabakia London kwa muda wote wa Michezo ya Olimpiki,
baada ya kutemwa kwenye kikosi cha GB. Atarejea Los Angeles kuichezea klabu
yake, LA Galaxy.
RODGERS AJITABIRIA UGUMU LIVERPOOL...
KOCHA
mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba anatarajia changamoto kubwa
kabla ya kufikia mafanikio katika klabu hiyo ya Anfield.
NI FAINALI YA KUFA MTU SIMBA NA AZAM TAIFA LEO
Azam wakijinoa |
Na Prince
Akbar
FAINALI ya Kombe la Urafiki,
michuano inayoandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), inachezwa leo kuanzia
saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikizikutanisha bingwa wa Ligi Kuu
Simba SC na mshindi wa pili wa ligi hiyo ya Bara, Azam
FC.
Hatua ya awali ya michuano
hii, ilifanyika visiwani Zanzibar, lakini kutokana na timu zote za Bara kuingia
fainali, makubaliano yalifikiwa kwa sababu za msingi, mechi ya mwisho ya
michuano hiyo ifanyike Dar es Salaam.
Timu zote zililalamikia eneo
la kuchezea mpira (pitch) la Uwanja wa Amaan kwamba ni baya na linasababisha
wachezaji kuumia, hiyo ikawa sababu ya leo watu kuelekea
Taifa.
Timu zote zilirejea Dar es
Salaam juzi jioni na kuelekea kwenye kambi zao kwa maandalizi ya mwisho mwisho
kabla ya kuibukia Taifa usiku wa leo.
Kocha wa
Azam, Stewart Hall |
Kwa sasa, upinzani katika soka
ya Tanzania upo kwa Simba na Azam ambao waligombea ubingwa wa Ligi Kuu msimu
uliopita na ndio watakaoiwakilisha nchi kwenye michuano ya Afrika
mwakani.
Simba ni timu kongwe yenye
mashabiki mamilioni na leo maelfu ya mashabiki wake watakuwa uwanjani
kuishangilia timu yao, lakini Azam japo ni timu changa na haina mashabiki wengi,
itanufaika na utamaduni wa upinzani wa jadi katika soka ya Tanzania kwa maelfu
ya mashabiki wa Yanga kuwapa sapoti leo.
Kwa sababu hiyo, suala la
msisimko kwenye mchezo wa leo, halina mjadala- utakuwa wa hali ya juu
sana.
Simba iliyoanzishwa zaidi ya
miaka 70 iliyopita, ndio timu bora Tanzania hadi sasa, ikiwa imeweka rekodi
ambazo hazijafikiwa na klabu nyingine nchini, wakiwemo wapinzani wao wa jadi,
Yanga- kufika fainali ya Kombe la CAF 1993 na kufika Nusu Fainali ya Klabu
Bingwa Afrika 1974.
Kocha wa
Simba, Profesa Milovan Cirkovick |
Simba pia inaifuatia Yanga kwa
kubeba ubingwa wa Ligi Kuu, ikiwa imetwaa mara 17, katika miaka ya 1966, 1973,
1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004 na 2007
(Ligi Ndogo), 2010 na 2012. Yanga imechukua mara 22 katika miaka ya 1968, 1969,
1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997,
1998, 2002, 2005, 2006, 2008 na 2009 na 2011.
Hadi sasa, Azam iliyoanzishwa
mwaka 2004 na kupanda Ligi Kuu mwaka 2008, ina taji moja tu, ambalo ni Kombe la
Mapinduzi ililolitwaa Januari 16, mwaka huu kwa kuifunga Jamhuri ya Pemba mabao
3-1 kwenye fainali, katika michuano ambayo ilivitoa vigogo Simba na Yanga kabla
ya kupata tiketi ya kucheza mechi ya mwisho Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Simba iliingia fainali baada
ya kuifunga Zanzibar All Stars 1-0, bao pekee la kiungo wake mpya kutoka Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Patrick Kanu Mbivayanga, wakati Azam iliifunga
Super Falcon 2-0, mabao ya mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Kipre Herman
Tcheche.
Katika mchezo wa leo, Haruna
Moshi ‘Boban’ anaweza kuanzia benchi akitangulia Mbivayanga, wakati upo
uwezekano chipukizi Abdallah Juma akaanza sambamba na Mussa Mudde, Mwinyi
Kazimoto na Salim Kinje.
Kwa Azam, huenda mfungaji bora
wa Ligi Kuu, John Bocco ‘Adebayor’ akapewa jezi kufuatia Gaudence Mwaikimba kuwa
anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye Nusu Fainali, wakati Mrisho
Ngassa anaweza kutokea benchi sambamba na Abdulhalim
Humud.
Makocha wa timu hizo,
Muingereza Stewart Hall wa Azam FC na Mserbia Profesa Milovan Cirkovick wote
walitambiana jana kwamba kila mmoja ana matumaini ya kubeba Kombe hilo, ambalo
bingwa atajinyakulia zawadi ya Sh, Milioni 10 na atakayefungwa atapata kifuta
jasho cha Sh. Milioni 5.
Azam na Simba zitakazocheza
pia Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati sambamba na Yanga kuanzia mwishoni mwa
wiki hii mjini Dar es Salaam, zitafungua pia pazia la Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii mwezi ujao.
Katika mchezo wa leo, kikosi
cha Simba kinatarajiwa kuwa; Juma Kaseja, Shomary Kapombe, Amir Maftah, Lino
Masombo, Juma Nyosso, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Mussa Mudde, Abdallah Juma,
Kanu Mbivayanga na Salim Kinje.
Azam; Deo Munishi ‘Dida’,
Samir Hajji Nuhu, Ibrahim Shikanda, Said Mourad, Joseph Owino, George Odhiambo
‘Blackberry’, Ibrahim Mwaipopo, Kipre Michael Balou, Ramadhan Chombo ‘Redondo’,
John Bocco ‘Adebayor’ na Kipre Herman Tcheche.
Simba wakijifua |
REKODI YA SIMBA NA AZAM LIGI
KUU:
Februari 11,
2012
Simba SC 2 - 0 Azam
FC
Sept 11,
2011
Azam FC 0 - 0 Simba
SC
Jan 23, 2011
Simba 2-3 Azam
(Dar).
Sep 11,
2010
Azam 1-2 Simba
(Tanga).
Machi 14,
2010
Azam 0-2 Simba (Dar)
Okt 24,
2009
Simba 1-0 Azam (Dar)
Machi 30,
2009
Azam 0-3 Simba (Dar)
Okt 4,
2008
Simba 0-2 Azam
VAN PERSIE AFANYA MATANUZI JIRANI NA MANCHESTER, APIGA PAMBA ZA BLUU KAMA ZA CITY
ALIKUWA amevalia nguo za bluu
Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie alipokuwa kwenye 'matanuzi', lakini huo
unaweza kuwa mwanzo wa kuvua jezi ya klabu yake msimu ujao?
Van Persie, ambaye amebakiza
mwaka mmoja katika mkataba wake, anatakiwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya England,
Manchester City baada ya Mholanzi huyo kuonyesha dhamira ya kuondoka
Emirates.
TABASAMU TUPU: Nahodha
wa Arsenal akifurahia matanuzi na familia yake katika visiwa vya
Formentera
KIFAMILIA ZAIDI: RVP
anaweza kujiunga na mabingwa, Man City
Juventus na Manchester United
pia zinamtaka mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu, mwenye umri wa miaka 28, ambaye
alipigwa picha akila raha na familia yake.
Tofauti na wachezaji wenzake
wengi wa Ligi Kuu, Mholanzi huyo ambaye alivurunda kwenye Michuano ya Kombe la
Mataifa ya Ulaya, alikuwa akijiachia katika visiwa Ibiza.
Lakini Van Persie hakuwa mbali
na na tukio, akijirusha huko Formentera – kisiwa kidogo kinachofahamika vizuri
kama Ibiza.
Hata kama atachezea United, ni
oua na mdomo kwa ukaribu, ingawa mustakabali wake bado haujafikiwa na Arsene
Wenger anataka kumaliza suala la Van Persie haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
Sportsmail leo, Wenger amewaambia
Arsenal anataka suala la uhamisho wa mchezaji huyo limalizwe haraka - hata ikiwa
atamuuza mpachika mabao wake huyo tegemeo.
Kocha huyo wa Arsenal, anataka
kuzungumza ana kwa ana na Van Persie katika siku chache zijazo, kujaribu
kumshawishi asaini mkataba mpya. Lakini kama atashindwa kufanya
hivyo,
Wenger anataka amuuze haraka mshambuliaji huyo.
Mfaransa
huyo ni bora achukue fedha katika wakati ambao atapata fursa ya kusajili naye
wakali wengine, kuliko kama ilivyokuwa mwaka uliopita, wakati alipowauza Cesc
Fabregas na Samir Nasri karibu na kufungwa kwa dirisha la usajili na kuathiri
maandalizi yake ya msimu mpya.
Wanataka zaidi ya pauni
Milioni 30 kumuuza nyota huyo wa Uholanzi, lakini umri wa Van Persie na
ukichanganya na ukweli kwamba amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake, ina
maana wanastahili kumuuza kwa bei mbaya sana, pauni Milioni 20
No comments:
Post a Comment