Tuesday, July 10, 2012

MJADALA: LIONEL MESSI NA RONALDINHO GAUCHO MKALI NANI? - VALDES WA BARCA KAMCHAGUA DINHO.

Kipa wa Barcelona Victor Valdes amesema amecheza na wachezaji wote wawili Ronaldinho na Lionel Messi lakini kwa asilimia 100 anaamini Gaucho alikuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa kuliko wote ambao amewahi kuwashuhudia akiwemo Messi. Kipa huyo mwenye miaka 30, aliiambia Terra TV. Akiwa anatajwa sana kama mmoja ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea ulimwenguni, Messi ameuwasha moto kwenye La Liga katika kipindi cha miaka 8, akivunja rekodi mbalimbali ikiwemo ya kufunga mabao mengi. Lakini, Valdes anaamini Ronaldinho kipekee zaidi aliibadilisha historia ya Barca alipowasili Nou Camp 2003, na kuchangia kwa mafanikio wanayoyapata kikosi cha sasa. "Siku zote nimekuwa nikisema kwamba Rony aliibadilisha historia ya klabu alipokuwa akicheza hapa. Alikuwa kiongozi wa timu ambayo ilibadilisha histori yetu. "Hatukuwa tumeshinda taji lolote kwa miaka mingi. Alikuja na kuifanya Barca kuwa na nguvu na kuifanya kuwa klabu kubwa inayojulikana duniani kote kwa uwezo wake. Namshukuru sana kwa hilo. Naweza kusema ndio mchezaji mwenye kipaji kikubwa kuliko wote ambaye nimewahi kushea nae chumba cha kubadilishia nguo. Alikuwa anafanya vitu vyake vya kustajaabisha kila siku.

WAADAU MNA MAONI GANI? NANI MKALI
 

UTAMU WA SODA YA PEPSI WAMKOSESHA BILLIONI 2 ZA COCA-COLA RONALDINHO

Apparently utamu wa Pepsi umemkosesha dili lenye thamani ya zaidi ya Billioni 2 za kibongo mchezaji wa kimataifa wa Brazil Ronaldinho Gaucho baada ya kampuni ya Coca-Cola kumpiga chini kwenye kazi ya ubalozi baada ya kuonekana akitumia kinywaji cha wapinzani wao kibiashara.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa akiwahesabu Coca-Cola kama moja ya makampuni mengi anayofanya nayo kazi kwa kumdhamini, lakini akufanya kosa la kuonekana akinywa kinywaji cha Pepsi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.

Kiwango cha Ronaldinho tangu arudi Brazil na ugomvi wake na klabu ya Flamengo umekuwa ukimfanya atengeneze sana vichwa vya habari vya magazeti kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.

Na kufuatia kwa kosa lake la hivi karibuni, Coke hawakuonyesha kusita katika kuukatisha mkataba wao na kiungo huyu mwenye miaka 32 na mchezaji bora wa dunia wa zamani wa FIFA.

"Kitendo cha kuonekana akinywa Pepsi kimeharibu taswira yake mbele ya wanywaji wa Coke. Watamuelewa vipi balozi anayewatangazia bidhaa hi halafu yeye anatumia nyingine. Kwa hili tumeamua kuuistisha mkataba wake na sisi." - alisema Mkuu wa masoko wa Coca-Cola Marcelo Pontes
.
 

MPINZANI WA MANJI UCHAGUZI WA YANGA: EDGAR CHIBULA SOMA SERA ZAKE

Zikiwa zimebaki siku kadhaa mpaka kufanyika kwa uchaguzi wa klabu ya Yanga, site hii itakuwa ikikuletea mahojiano maalum na wagombea wa nafasi mbalimbali wanaowania uongozi kwenye klabu hiyo kongwe ya Tanzania.

Kwa kuanzia leo tunaye mgombea wa nafasi ya mwenyekiti Bw.Edgar William Chibula akiongelea nia na madhumuni ya kugombea uongozi wa Yanga, pamoja na sera zake kwa ujumla.

Jina: Edgar William Chibula
Umri: 38
Utaifa: Mtanzania
Elimu: Degree ya Ualimu, Amesomea ukocha chini ya ukufunzi wa Eugene Mwasamaki - pamoja na kozi ya uamuzi chini Leslie Liunda.

SABABU NA MADHUMUNI YA KUGOMBEA UONGOZI NDANI YANGA
Akiwa mmoja ya wanachama halali wa Yanga - Bwana Chibula anayo haki ya kimsingi kugombea nafasi ya uongozi wowote kwenye uchaguzi wa klabu hiyo. Sasa kwenye huu uchaguzi ujao wa Yanga ameamua kugombea nafasi ya uenyekiti. Kwanini ameamua kugombea nafasi?

"Nimeamua kugombea uenyekiti wa Yanga kwa sababu zifuatazo: Nina uwezo mkubwa kuiongoza na kuitoa Yanga hapa ilipo na kuifanya kuwa na hadhi inayostahili kama klabu yenye zaidi ya miaka 70.
Kiukweli klabu hii imedumaa, haikuwi kila siku hipo kama ilivyokuwa huko nyuma. Yanga imekuwa kama mtoto mwenye ugonjwa wa upungufu wa homoni za ukuaji hivyo inashindwa kukua na mwishowe inadumaa. Hii inatokana kupata malezi mabovu kutoka kwa wazazi wake nikimaanisha viongozi ambao wamekuwa wakichaguliwa kuiongoza klabu hii. Timu imekuwa ikiendeshwa kienyeji na sio kwa mfumo wa kisasa. Viongozi hawana mipango endelevu - wamekuwa wakiendesha timu kwa mipango ya zimamoto. Wamekuwa wakiitumia Yanga kwa manufaa yao binafsi na kuifanya timu kubwa kama hii iendelee kutegemea vijipesa vya gate collection.
Mimi nataka kuingia kwenye uongozi wa juu niondoe hii hali kwa sababu naamini hakuna linaloshindikana, Yanga ni mtaji tosha hivyo kila kitu kinawezekana kufanyika kinachohitajika ni uongozi mzuri wenye ubunifu na utakaoendesha timu kisasa.

Ikiwa utafanikiwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Yanga utaifanyia nini klabu?

"Kiukweli jambo langu kubwa nitakalofanya kwanza ni kuifanya Yanga kuwa timu inayojiendesha yenyewe kwa maana ya kiuchumi bila kumtegemea mtu wa kikundi cha watu. Mpira siku hizi umekuwa biashara kubwa sana duniani na mfano mzuri tunaona kwa vilabu vya nje ya mipaka yetu hasa barani ulaya. Hivyo timu ikiweza kujitegemea na kujiendesha kwa faida tutafanikiwa kufanya vitu vingi sana.

Ili kuweza kufanikisha hili nitakaa chini na jopo la viongozi wenzangu na kuja na mipango bora ya klabu kuitumia brand yake kufanya biashara ya bidhaa tofauti zitakazotengenezwa kwa kutumia jina la "Yanga" ambazo ndio kitakuwachanzo kikuu cha mapato ya klabu ambayo tayari ina utajiri wa rasilamali watu ambao ni utitiri wa mamilioni ya watanzania wenye mapenzi makubwa na klabu yao.

Jambo lingine kubwa ambalo nitashughulikia ni kuunda mfumo mzuri utakaosimamia hesabu za fedha na matumizi yake ambayo itabidi yawe wazi ili kuepeusha suala la ubadhirifu wa fedha za klabu.

Kuunda mfumo bora wa wanachama wetu kuweza kuchangia mawazo tofauti kupitia kwenye matawi na hatimaye yafike kwenye uongozi wa juu na kufanyiwa kazi mara moja.

Lingine nitakalolifanya ni kuigueza klabu kuwa kampuni itakayokuwa chini ya wanachama Yanga. Naamini Yanga imebarikiwa na wanachama wenye ujuzi tofauti ambao kama ungetumika vizuri Yanga inaweza kufaidika nao kuliko kukaa klabuni na kuanza kupiga domo bila kuleta impact yoyote. Kampuni ya Yanga itaweza pia kutoa ajira kwa wanachama wenye uwezo na watakaokidhi matwaka na ajira zitakazotengenezwa na mwisho wa siku kila mwanamachama wa Yanga afaidike na klabu yake na kwa upande timu yetu ikiendelea kukua.

Nitaweka mkazo na mazingira mazuri kwa soka la vijana nikmaanisha academy ya Yanga ambayo nitaanzisha na kuweza kuchukua watoto wenye vipaji na kuwakuza na kwa hakika baadae watainufaisha klabu kwa namna moja au nyngine.

Umoja - moja ya matatizo mengi yanayoipelekea klabu yetu kushindwa kuendelea mbele ni kukosekana kwa umoja miongoni mwa wanachama wote wa klabu hii. Kuna makundi ambayo kiukweli mie naona ni adui wa maendelea ya klabu. Hivyo nitahakikisha kunapatikana umoja wa wanachama wote wa Yana ambao tutafanya kazi kwa pamoja kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la klabu yetu tunayoipenda kwa dhati."


KWANINI WANACHAMA WA YANGA WAKUCHGUE WEWE NA SIO WENGINE?

Kwanza kabisa katika wanachama wenzangu wote wanaogombea uenyekiti - no offense lakini hakuna aliye na sifa kama zangu.
Mimi ni mwalimu wa soka pia ninajua mpira kuucheza na kusimamia sheria zote za soka kwa kuwa tayari nilishasomea kozi ya ukocha na uamuzi.

Nina uzoefu mkubwa kwenye kuongoza vilabu vya soka, kwanza nimeshawahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Abajalo FC ya Dar es Salaam, na nikafanikiwa kuiongoza kutoka kwenye ligi ya daraja la tatu mpaka la kwanza huku tukipata mafanikio ya kubeba vikombe vingi sana. Pia niliweza kuifanya klabu kujitegemea kwa asilimia nyingi sana kwa kubuni mipango ya biashara ambazo ambazo kiukweli zililipa na kuifanya klabu kujitegemea.

Abajalo chini ya Uongozi wangu iliweza kutoa wachezaji wengi wakubwa na hasa wale waliokuja kuichezea klabu yetu ya Yanga akiwemo Kally Ongara, Ally Mayay na wengine kibao.

Lingine nina mapenzi makubwa na klabu hii na naamini mimi ndio mtu sahihi ambaye Yanga inahitaji. Yanga inahitaji kuwa kiongozi ambaye atakuwa yupo full committed na kazi yake 24/7. Yanga haihitaji kiongozi wa kutuma tu inahitaji mwenyekiti mtendaji atakayekuwa ana-over see shughuli za kila siku za klabu. Kwenye kundi la watu wanaoutaka uenyekiti ni mimi pekee ninayekidhi viwango hivyo."
 

UMEDUNGUA NINI KATIKA HII PICHA???



umegundua nini katika hii picha???

 

AZAM ACADEMY YAINGIA ROBO FAINALI YA ROLLING STONE!

Azam Academy leo imeifunga Kyazanga FC ya Uganda na kuwa timu ya kwanza kutinga robo fainali ya Rolling Stone kufuatia kufikisha pointi 6 baada ya kushinda michezo yake miwili mfululizo... Katika mchezo wa awali Azam Academy iliifunga 3-0 Nyirakongo Academy ya DRC,...Dah hawa vijana wananifanya nijisikia fahari kuwa shabiki wa Azam FC...

MARIO BALOTELLI, JOEY BARTON NA WACHEZAJI WENGINE WANAOTEGEMEWA KULAMBWA KADI NYEKUNDU KWENYE MSIMU UJAO WA EPL

SUPER MARIO BALOTELLI

Nani mwingine zaidi ya kijana mwenye asili ya Ghana Super Mario?

Mario Balotelli alionyesha kwamba kidogo anaanza kukomaa kiakili na kutlia wakati wa Euro 2012, lakini wote tunatambua kwamba ni kichaa kiasi gani.

Kwa hakika japokuwa ameonyesha kutulia kidogo, lakini kwa Mario Balotelli unapoandama mwezi mchanga kwake basi tegemea lolote kutoka kwake akiwa uwanjani.

Marefa wa England wanasubiri ligi ianze wakutane na Balotelii aliyestaharabika lakini vinginevyo tutaendelea kuona kadi kadhaa nyekundu zikiigharimu timu yake ya Manchester City.

Na Mario ataendelea kujiuliza kila "Why Always Me" mpaka atakapoacha utukutu dimbani atleast.

JOEY BARTON

Inapotajwa listi ya wachezai watukutu nadhani jina la huyu kijana wa kiingereza haliwezi kukosa.

Ni maarufu kwa matukio yake ya ukosefu wa nidhamu kuliko soka lake, alianza kupata umaarufu kwa tabia zake za nidhamu ndogo tangu akiwa Manchester City, lakini dunia ilimtambua zaidi pale alimpokaribisha kwenye Premier League mchezaji kutoka Ivory Coast ambye ndio kwanza alikuwa akiichezea timu yake mpya ya Arsenal mechi ya kwanza ya EPL 0 na kwa bahati mbaya akakutana na mtoto wa mjini Joey Barton na akamsababishia kadi nyekundu kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya England msimu uliopita kati ya Newcastle na Arsenal.

Ukichaa wake kwenye msimu uliopita haukushia Newcastle tu, alipohama kwenda QPR aliendeleza ukorofi wake, na tukio kubwa zaidi alilifanya kwenye mechi ya lazima kupata matokeo chanya kwa timu ili kuweza kubaki ligi kuu dhidi ya Manchester City - matokeo yakiwa moja moja Joey Barton akaanza mtiti na Carlos Tevez na akapigwa red card, kabla ya kumtandika ngumi ya mbavu Sergio Aguero akiwa anaelekea nje ya dimba.

Pia amekuwa na matukio mengi ya kustaajabisha nje ya uwanja lakini mmiliki wa QPR sasa amempa nafasi ya mwisho huku akimvua unahodha - kwa jinsi alivyo huyu jamaa ni vigumu kuacha mtukutu Joey Barton.

Kwenye msimu unaonza ndani ya kipindi cha siku zisizopungua 35 tutashuhudia Barton akilamba kadi nyekundu nyingine kama ilivyo ada.

RYAN SHAWCROSS


Ni maarufu zaidi kwa tukio lake la kumvunja mguu mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey mwezi wa pili 2010, Mchezaji huyu wa Stoke City amekuwa na historia ya kucheza rafu mbaya sana.

Na huku akiwa anaichezea klabu inayojulikana kwa kutumia mabavu haistui kumuona kwenye listi hii.

Yeye pamoja na patna wake kwenye ulinzi Roberto Huth wanabidi wajitazame upya na aina yao ya kufanya tackling. Lakini la sivyo tegemea kumuona mchezaji huyu kinda la Old Trafford akiendelea kulamba kadi nyekundu msimu ujao.

NIGEL DE JONG

Kiungo wa Manchester City anajulikana zaidi kwa aina ya mchezo wake wa kukaba na kutumia nguvu zaidi. Nae ana historia ya matukio ya ajabu kwenye soka.

Makubwa zaidi ni pale alimpovunja mguu nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa na Newcastle Hatem Ben Arfa na lile teke la kung-fu alilompiga kiungo wa Spain Xabi Alonso kwenye world cup 2010.

Umuhimu na kuapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kunaweza kukawa kumepungua kwa mbingwa hao wa watetezi wa EPL katika miezi ya karibuni, lakini kwa hakika zaidi ataendelea kupata nafasi kwenye kikosi na endapo atacheza basi tegemea lolote kutoka kwa kiungo huyu wa kidachi.

CHEIK TIOTE


Story ni ile ile kwa kiungo wa Newcastle Cheik Tiote.

Anaweza kuwa moja ya viungo bora wa Premier league kutokana na kazi kubwa anayoifanya dimbani hasa kwenye kulinda safu ya ulinzi, lakini rekodi ya nidhamu yake inaweza kumuangusha.

Ni mmoja ya wachezaji wanaocheza tackling za hatari dhidi ya wapinzani - huku akionyesha ni namna gani anavyojituma kwenye kuulinda ukuta wa kikosi cha Alan Pardew.

Matokeo yake msimu uliopita alipata kadi za njano 11 - hivyo tegemea kumona akiendelea kuingia kwenye vitabu vya marefa kwa red card.
 

LUCAS MOURA: KIJANA WA KIBRAZIL ANAYEMTOA UDENDA FERGUSON, MADRID, INTER NA CHELSEA



Kwa takribani siku kama mbili hivi kumekuwepo na habari zilizoenea kwenye mitandao tofauti na mikubwa nchini Uingereza kwamba klabu ya Manchester United imewatuma ujumbe wa baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kwenda nchini Brazil kufanya mazungumzo na hatimaye kukamilisha usajili wa kinda la Sao Paolo Lucas Moura.

Moura ambaye pia aliwahi kuhusishwa na kujiunga na Real Madrid, kabla ya taarifa nyingine kutoka kwamba klabu yake ilikataa ofa ya €30million kutoka kwa Chelsea wakati wa kipindi cha usajili kilichopita.

Sasa usiku wa Jumapili inasemekana viongozi wa United walikwea pipa mpaka nchini Brazil na leo jumanne wameanza mazungumzo ya kumnyakua kinda hilo. Sao Paolo wamezungumza na kukiri kwamba wanajua United wanavutiwa na kiungo lakini hawajakanusha kama kuna ofa tayari imeshatumwa na mashetani wekundu.

Lucas ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na moja ya wachezaji wachanga wanaounda kikosi cha Brazil kitakachoshiriki kwenye michuano ya Olympics itakayofanyika London.

Kwa hakika ukiwa umeangalia hiyo video hapo juu utajua kwanini kinda la miaka 19 linasababisha vigogo wa soka barani ulaya wagombanie saini yake.
 

HAMIS KIIZA NA CANAVARRO WAING'ARISHA YANGA TAIFA - WAKIIFUNGA JKT RUVU 2-0

Dakika chache zilizopita mechi ya kirafiki kati ya mabingwa wa Africa mashariki na kati Dar Young African na JKT Ruvu imemalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa 2-0. Magoli ya Yanga yamefungwa na beki Nadir Haroub Cannavaro kwenye dakika ya 18, na Hamis Kiiza kwenye dakika ya 73.
Hamis Kiiza mfungaji wa bao la pili la Yanga.

No comments: