Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza na watendaji wa serikali mkoani Mtwara jana. |
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwapungia mikono makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati akiwasili katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuzungumza na watendaji wa serikali. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
Waziri mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amewataka wakurugenzi
wa halmashauri nchini kuhakikisha wanamaliza migogoro yote iliyopo baina ya
wananchi na halmasahuri zao kwa ajili ya kufanikisha maendeleo ya pamoja.
Akizizungumza
mkoani Mtwara katika kikao cha pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali jana,
alisisitiza kuacha tabia ya kupuuza hoja zinazotolewa na madiwani kuhusu
matatizo yaliyopo kwenye kata zao huku akiwataka kuacha tabia ya kushinda
ofisini na baadala yake kwenda kusikiliza hoja za wananchi.
“Na tulisema
wakurugenzi piteni kwenye maeneo yenu, msikae ofisini, nyie kama watendaji
wakuu mjiridhishe kwamba yale yanayozungumzwa na Madiwani kwamba kuna tatizo
moja, mbili, tatu nne kweli yapo? Kama lipo je lina ukubwa gani wa tatizo na
linatakiwa kupata uharaka wa kiasi gani..kwahyowakurugenzi mnao wajibu mkubwa
wa kuhakikisha kwamba migogoro ya wananchi na halmashauri inakwisha..” alisema.
Aidha, alizitaka
halmashauri zote mkoani Mtwara kuhakikisha zinakuwa na benki ya ardhi kwa ajili
ya kutenga maeneo maalumu kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaji.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwapungia mikono makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati akiwasili katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuzungumza na watendaji wa serikali. |
Awali akitoa
taarifa ya mkoa, mkuu wa mkoa Mtwara,Halima Dendego alisema kuwa mkoa
unaendelea na ukusanyaji wa mapato ya ndani na kwaamba wamefanikiwa kukusanya
jumla ya shilingi Bilioni 16.6 katika halmashauri zote mpaka sasa huku
wakitaraji kufikia lengo.
“Lakini kwa
halmashauri mapato ya ndani tulipaswa kukusanya Bilioni 20 na mpaka leo
tumekusanya Bilioni 16.6 ni sawa na asilimia 82.2 na ninaamini kabisa bado
tunaendelea kukusanya na hasa tozo za ardhi ambazo tunatakiwa turudishiwe
kutoka wizara.” Alisema Dendego.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wabunge wa Mkoa wa Mtwara na mbunge wa Newala mjini, George
Mkuchika, alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Mtwara ni wapenda maendeleo lakini
wanayumbishwa na viongozi wao huku akidai kuwa sababu za mkoa huo kuchelewa
kupata maendeleo ni kwasababu ya kupigana vita na Msumbiji mwaka 1964-1974.
“Sisi
tulikuwa vitani, kule vita vikichafuka tulikuwa tunalala kwenye maandaki..kwahiyo
wakati wenzetu wanajenga sekondari sisi tulikuwa kwenye maandaki tukachelewa,
sasa ile mnayosikia Mtwara kuchelemaana yake katika lugha za mkoa huu zote
maana yake Mtwara kumekucha..” alisema.
Waziri mkuu
alitumia kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na baadhi ya wabunge kuzisisitiza halmashauri kusimamia
utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.
No comments:
Post a Comment