Yanga watavuna kiasi hiki cha fedha iwapo watatwaa ubingwa wa Shirikisho..
Yanga imekuwa na mafanikio makubwa chini ya Hans van
der Pluijm baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu na kutinga hatua ya makundi
lakini ili isonge ni sharti ivuke vikwazo vyote
Bingwa wa kombe la shirikisho Afrika anavuna dola 625,000(billion
1.3), mshindi wa pili dola 432,000 (milioni 907.2), mshindi wa tau dola
239,000(milioni 501.9) na mshindi wa mwisho anapata dola 150,000(milioni
315)
Mwaka 1998 Yanga walifuzu hatua ya nane bora chini ya Tito Mwavalunda
aliyekuwa kocha kipindi hicho akishirikiana na Felix minziro. Baada ya
miaka takribani 18 Yanga inafuzu hatua ya nane bora chini ya Mholanzi
Hans Van Pluijim.
Yanga wamefanikiwa kuiondoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya
magoli mawili kwa moja, baada ya awali kushinda Tanzania kwa magoli
mawili kwa sifuri na kwenda kufungwa moja bila na Waangola hao.
Wiki hii ratiba ya makundi itapangwa kwa timu 8 zilizosalia ambazo ni
TP Mazembe (Congo) , Etoile du Dahel (Tunisia) , Mo Bejaia (Algeria) ,
Kawkab Marrakech (Morocco) , Ahli Tripoli (Libya) , Medeame (Ghana) ,na
Yanga yenyewe.
Goal inakuletea baadhi ya timu zitazokuwa kikwazo kwa Yanga endapo watapangwa kundi moja
TP Mazembe
Mabingwa wa mara 5 wa klabu bingwa Afrika (1967,1968, 2009, 2010,
2015) inamilikiwa na tajiri wa Congo Moise Katumbi, licha ya kutoanza
vizuri msimu huu na kupelekea kutolewa kwenye klabu bingwa, bado TP
Mazembe inasimama kama moja ya timu bora Afrika, aina ya wachezaji wao
wenye uzoefu kwenye michuano mikubwa na uwekezaji mkubwa, inaweza kuwa
kikwazo kwa Yanga kama wakiwa kundi moja, haitakuwa rahisi kwa Yanga
kupata matokeo kirahisi kwa Tp Mazembe.
Mo Bejaia
Timu kutoka Algeria, iliyoanzishwa mwaka 1954, haina rekodi kubwa
katika michuano ya Afrika, lakini si timu ya kubeza sana sababu
wamefanikiwa kuiondoa moja ya timu bora Afrika, Esperanca ya Tunisia,
baada ya mechi ya kwanza kutoka bila bila na marudiano kule Tunisia
mchezo kuisha kwa goli moja moja hivyo Mo Bejaia kufuzu kwa goli la
ugenini, kutokana na ubora wa nchi ya Algeria katika soka Mo Bejaia
itakuwa moja ya timu itakayo leta upinzani mkubwa katika hatua hio ya
makundi.
Fus Rabat
Mabingwa wa zamani wa kombe la shirikisho mwaka 2010, Fus Rabat
kutoka Morocco, imefanikiwa kuingia hatua ya makundi baada ya kuiondoa
Stade Maliene ya Mali kwa idadi ya magoli 4 kwa bila, moja ya timu bora
kati ya timu zilizomo kwenye 8 bora shirikisho, wanashika nafasi ya pili
kwenye ligi kuu nchini Morocco ambayo ni miongoni mwa ligi bora za
Afrika, Fus Rabat ,Yanga haina budi kuzihofu changamoto za klabu hii
ya Morocco sababu ya uwekezaji wao waliofanya katika klabu kwa nia ya
kufanya vizuri Afrika.
Etoile Du Sahel
Huyu ndo bingwa mtetezi wa kombe la shirikisho, kutokana na Yanga
kutokuwa na matokeo mazuri kwa timu za kiarabu, kwa miaka ya hivi
karibuni si timu sahihi ya kuiombea kupangwa nayo kundi moja, aina ya
wachezaji wenye uzoefu wa michuano mikubwa, ukubwa wa la benchi la
ufundi na ubora wa ligi yao, ambao wanongoza ligi mpaka sasa, Etoile
itakuwa kikwazo kwa Yanga kama wakitupwa kundi moja, itakuwa ngumu
kupata matokeo ugenini kwa Yanga endapo watapangwa katika kundi moja.
CHANZO: GOAL
No comments:
Post a Comment