Mwandishi wa habari ya Juma News, Juma Mohamed, akiwa na wadau wa maendeleo wilayani Masasi katika shughuli za usafi wa mazingira. |
Juma Mohamed, Mtwara
Waandishi wa
habari mkoani Mtwara wanatarajiwa kuungana na wadau wao pamoja na viongozi wa
mkoa kesho septemba 17 kuendesha zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya
rufaa ya mkoa huo, Ligula.
Katibu
mtendaji wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mtwara MTPC, Bryson Mshana,
alisema lengo la zoezi hilo ambalo limepangwa kutekelezwa mwezi septemba ya
kila mwaka ni kukutana na wanajamii ambao ni wadau wakubwa katika tasnia ya
habari.
“lengo letu
hasa ni kukutana na wanajamii ambao tunafanya nao kazi na kufanya nao shughuli
mbalimbali na siku ya kesho tumeamua kufanya usafi katika hospitali yetu ya
Ligula..kwa maana ya kufanya usafi, kutazama wagonjwa lakini pia kupanda miti..”
alisema Mshana.
Frank Fue,
nimiongoni mwa wanahabari watakaofanya usafi huo utakaoambatana na zoezi la
upandaji miti kuanzia saa 2 mpaka saa 4 asubuhi, alieleza umuhimu wake na kutoa
rai kwa jamii.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiwa katika moja ya shughuli za usafi katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. |
Zoezi hilo
litaongozwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego, atakaeambatana na mkuu wa
wilaya hiyo Dokta Khatibu Kazungu, ambaye aliwataka wakazi wa mkoa wake
kujitokeza kwa wingi katika kuwaunga mkono wanahabari.
“jambo hili
hufanywa kila mwaka na ndugu zetu hawa wadau wa maendeleo,kwahiyo niwaombe
wanamtwara wote kwa utamaduni wetu tuliouzoea tujitokeze, kwasababu
wanalolifanya ni kwa ajili ya jamii yetu, najua tukiunga mkono kazi hii kubwa
wanayoenda kuifanya kesho basi matokeo yake yatatugusa sisi sote.” Alisema Dendego
Zoezi la
usafi kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara linafanyika kila ifikapo
Jumamosi ya kwanza ya mwezi Septemba ya kila mwaka.
No comments:
Post a Comment