Mmoja wa Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia katika ajali |
Juma Mohamed, Mtwara.
Wasaidizi
wanne wa ofisi ya makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata ajali
likiwa katika msafara kuelekea wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara.
Akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo
iliyohusisha gari lenye namba za usajili ST. 244A, kamanda wa Polisi mkoa wa
Mtwara, Thobias Sedoyeka, alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa Nne na nusu
asubuhi ambapo majeruhi wote wamekimbizwa katika ospitali ya rufaa ya Ligula
kwa taratibu za kiuchunguzi.
“Katika kijiji
cha Malanje majira ya saa Nne na Nusu katika msafara wa makamu wa Rais kuelekea
wilayani Tandahimba kulitokea ajali, gari ST 244 A hata hivyo gari limeharibika
na majeruhi tumewapeleka hospitali ya serikali kwa ajili ya taratibu nyingine
za kiuchunguzi..” alisema kamanda.
Mganga mkuu
wa mkoa wa Mtwara, Dkt. Wedson Sichawe, alisema katika majeruhi hao hakuna
aliyeumia vibaya sana isipokuwa dereva wa gari hilo ambaye hakumtaja jina kuwa
alikuwa akilalamika maumivu ya shingo.
Mkuu wa mkoa
wa Mtwara, Halima Dendego, aliwaondoa hofu Watanzania na kusema kuwa waliopata
ajali wote ni wazima huku msafara wa makamu wa Rais ukiendelea na ziara yake
wilayani Tandahimba.
Gari lililopata ajali katika msafara wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-Samia Suluhu Hassan ukielekea wilayani Tandahimba mkoani Mtwara. Toyota Land Cruiser- ST 244 A |
“Gari
limepata madhara na ndugu zetu wameumia kidogo niwaondoe hofu ni wazima wote na
tumewachukua tumewakimbiza hospitali yetu ya mkoa ya rufaa ya Ligula kwa ajili
ya uwangaliazi zaidi..lakini ni jambo ambalo ni bahati mbaya kwakweli lakini
msafara wote ukiacha hao waliopata ajali uko salama na tunaendelea na ziara
kama
Mkamu wa
Rais leo ametembelea kiwanda cha kubangua korosho cha AMAMA Farms Ltd katika
mwendelezo wa ziara yake mkoani humo pamoja na kuzungumza na wakazi wa wilaya
ya Tandahimba.
No comments:
Post a Comment