Wahamiaji haramu waliokamatwa Mtwara wakijaribu kuvuka mpaka wa Tanzania na Msumbiji, katika kijiji cha Kilambo, halmashauri ya wilaya ya Mtwara. |
Wanahudumiwa Chai na Mkate |
Juma Mohamed, Mtwara.
Idara ya
uhamiaji mkoa wa Mtwara imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu Kumi na wanane
raia wa nchini Ethiopia wakiwa katika harakati za kuvuka katika mpaka wa
Kilambo, halmashauri ya wilaya ya Mtwara kuelekea nchini Msumbiji.
Akizungumza
mkoani hapa, naibu kamishina wa Uhamiaji, afisa uhamiaji mkoa wa Mtwara, Rose
Mhagama, alisema wahamiaji hao wamekamatwa huku ikiwa haijafahamika aliyehusika
katika kuwasafirisha, na kwamba leo wanafikishwa mahakamani baada ya
kujiridhisha kuwa wameingia nchini visivyo halali.
“Sisi kama
Uhamiaji ambao ndio jukumu letu kuwashughulikia watu wa aina hii, tuko nao hapa
na baada ya muda mfupi tutawafikisha mahakamani baada ya kujiridhisha kwamba
wameingia nchini visivyo halali, wamekiuka sheria ya uhamiaji ya kuwapo nchini
bila vibali..lakini kama haitoshi waliweza kupita njia zisizo rasmi..” alisema.
Naibu kamishina wa Uhamiaji, afisa uhamiaji mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama. |
Aidha, alikiri
kuwa mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya kutumika kama njia kwa wahamiaji,
kutokana na kupakana na nchi ya Msumbiji, nakuwataka wananchi kushirikiana na
maafisa uhamiaji katika kutoa taarifa za raia hao, ili kukabiliana na
changamoto hiyo.
Wanarejeshewa Passport zao |
Hatua
imekuja ikiwa ni wiki mbili baada yawaziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mhe. Kassim Majaliwa, kutoa msisitizo kwa Idara hiyo kuhakikisha
inaimarisha ulinzi katika mipaka yote inayopakana na nchi jirani ili kudhibiti
raia hao.
Mkoa huo
umefanikiwa kuwakamata jumla ya wahamiaji haramu 123 kuanzia mwezi Januari
mpaka Juni mwaka huu, kutoka katika mataifa Kumi na Mbili na kati ya hao, raia
Hamsini na sita ni kutoka nchini Ethiopia.
No comments:
Post a Comment