Mmoja wa waumin wa Kiisilam akichangia damu baada ya swala ya Eid |
Akina mama, watoto na wasichana waliojitokeza katika swala ya Eid jana katika viwanja vya shule ya Kiisilam ya Amana. |
Waumin wakitekeleza ibada ya swala ya Eid |
Swala ya Eid |
Juma Mohamed, Mtwara.
Waumin wa
dini ya kiislamu mkoani Mtwara wamehamasika na kushiriki katika kutoa sadaka ya
sikukuu ya Eid El- Fitr kwa kuchangia damu kwa hiyari katika zoezi lililoendeshwa
na mpango wa Taifa wa damu salama kanda ya kusini mara baada ya kuswali swala
ya Eid katika viwanja vya shule ya sekondari ya Amana Islamic.
Wakizungumza
na Juma News, walisema kuchangia damu ni sehemu ya ibada muhimu kwa waumin wa
kiislam kwasababu mahitaji ya damu ni makubwa, na husaidia kuokoa maisha ya
watu, na kuwataka wananchi wengine kuona umuhimu wa kufanya hivyo.
Walisema
suala la kutoa sadaka ya Eid linaweza kufanyika kwa njia nyingi ambazo Mungu
huzikubali kama hauna uwezo wa kutoa pesa au chakula basi ni kheri kujitolea
damu ambayo itasaidia kuokoa maisha ya Watanzania wengine wenye mahitaji ya
damu.
Uchangiaji wa damu salama. |
“Nimeamua
kutolea sadaka damu yangu mimi, kwamaana hiyo sikuwa na uwezo wa kutoa sadaka
ya Fitir, sikuwa na uwezo wa kuchangia Majanvi nikachangia damu salama..na
naomba wanawake wenzangu tujihamasishe kuchangia damu tuwachangie wagonjwa,
kuna wengine wagonjwa hawajiwezi..” alisema Niya Ahmad.
Naye, Said
Hassan, aliwataka wananchi wengine kuacha kuwa na woga katika kutekeleza zoezi
hilo na kwamba kuchagia damu ni moja ya ibada muhimu kwa Waisilam ambayo
inaokoa uhai wa wengine walio katika Hospitali mbalimbali.
Afisa uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama kanda ya kusini, Maary Meshy, akieleza namna wanavyoendsha zoezi la uchangiaji damu baada ya swala ya Eid. |
Kwa upande
wake, afisa uhamasishaji wa benki ya damu kanda ya kusini, Marry Meshy,
alibainisha kuwa sasa katika benki ya damu kuna upungufu mkubwa wa kutokana na
watu walikuwa katika mfungo wa Ramadhan hivyo kushindwa kuchangia.
“Benki ya
damu kwa sasa tuna upungufu na uhitaji mkubwa kutokana na tumetoka katika
kipindi cha mfungo..na watu tunatambua kipindi cha mfungo kuna baadhi ya
taratibu au vigezo hawakidhi na wanahisi labda wataharibu funga yao kwahiyo
kipindi hicho upatikanaji wa damu unakuwa ni mdogo..kwa sasa hivi tumekuja
katika sikukuu ya Eid hii kwakuwa tunatambua mchango wa ndugu zetu Waisilam
huwa hawatuangushi miaka yote hua wanachangia damu ya kutosha..” alisema Meshy.
Damu salama |
Jumla ya
wakazi 115 walifanikiwa kuchangia damu hapo jana kupitia zoezi hilo ambalo
liliendeshwa katika vituo viwili vya Shule ya msingi Magomeni ambako
walifanikiwa kukusanya Units 35 za damu pamoja na shule ya Kiisilam ya Amana na
kupata Units 80.
Awali akitoa
mawaidha kwa waumin baada ya swala ya Eid, Ustaadh Idrissa Bakari, aliwahusia
waisilam kushikamana na kuwa wamoja pamoja na kuachana na kuingia katika
makundi ambayo yatawaondoa katika kumcha Mwenyezimungu.
Ustadh huyo
amewataka waisilam kuacha kujiita majina ya Kitaasisi ambayo yanaweza kuwafanya
wamsahahu Mungu na kufanya maasi.
Ustaadh Idrssa Bakar, akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid el Fitir. |
No comments:
Post a Comment