Mwaibambe na Madereva Bodaboda |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mtwara, Kamishina Msaidizi wa Polisi Henry Mwaibambe amewataka
madereva Bodaboda mkoani humo kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika
kutokomeza uhalifu ikiwa ni pamoja na wizi wa pikipiki.
Akizungumza
katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Nchini (PPF) kwa
madereva Bodaboda wa manispaa ya Mtwara Mikindani, alisema uhalifu wa wizi wa
pikipiki umefanikiwa kutokomezwa katika wilaya zote mkoani humo lakini bado
changamoto imebaki katika wilaya ya Mtwara.
“Tushirikiane
naomba sana, vinginevyo hapo ‘trend’ itaendelea..nyie ndio wenye Mtwara sisi
tunapita tu mnajuana vizuri, kitu hicho mimi ndio kinaniekera kidogo yani
ukikaa wiki mbili Pikipiki moja inanisumbua, lakini Masasi tulishawaweza vizuri
wale vijana..” alisem.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP-Henry Mwaibambe, akiwa katika picha ya pamoja na madereva Bodaboda na watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Nchini (PPF). |
Kwa upande
wao madereva Bodaboda, walikiri kuwapo kwa vitendo vya uhalifu ambapo wameahidi
kushirikiana vyema na jeshi hilo kuutokomeza huku meneja wa PPF kanda ya kusini
Kwame Temu akieleza lengo la semina hiyo pamoja na manufaa watakayopata
madereva hao kupitia mfumo mpya wa Wote Scheme.
Khamisi
Abdallah, alisema anaungana na Kamanda huyo kwa kulikemea suala hilo na
kuwataka wenzake kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa mapema mara
baada ya kubaini kutokea kwa uhalifu huku akiliomba jeshi hilo kutopuuzia
taarifa pindi watakapopatiwa.
Aidha,
wengine waliupongeza mfuko wa PPF kwa kuwapatia semina ambayo wanaamini
kutokana na shughuli zao kuwa miongoni mwa vipaumbele vilivyopo katika mfumo wa
Wote Scheme, wameona itakuwa ni msaada mkubwa sana kwao.
“Kutokana na
shughuli zetu hizi kwasababu hatuna bima ambayo inaweza kutuongoza katika
mazingira haya ya matizo yanapokuwa yametukuta, kwahiyo mimi kwanza napongeza
PPF kwa kuweza kuliangalia hili kwa kuliangalia kwa mapana na kuweza
kutuunganisha sisi madereva bodaboda ili watupe elimu kwa maana ya sisi wenyewe
tukishapokea basi tutakuwa rasmi kujiunga na mfuko huu..” alisema Omary Mbonde.
Meneja wa PPF kanda ya Kusini, Kwameh Temu, akiongea na wanabarai (hawapo pichani) baada ya ufunguzi wa semina kwa madereva Bodaboda. |
Naye, meneja
wa PPF kanda ya Kusini, Kwameh Temu, aliezea lengo la semina hiyo kuwa ni
pamoja na manufaa watakayopata madereva hao kupitia mfumo mpya wa Wote Scheme.
“Tumeandaa
semina hii kwa ajili ya vijana wa Bodaboda mkoa wa Mtwara ili kuweza kuwapa
elimu juu ya mfumo wetu mpya wa Wote Scheme ambao tuliunzisha mwaka jana..kupitia
mfumo huu tunaweza kuandikisha watu ambao wapo katika sekta isiyo rasmi Wavuvi,
Wakulima, Mamalishe..kwahiyo tuliona ni muhimu kuanza na kundi hili la
waendesha Bodaboda kwasababu ni watu ambao wanazalisha kipato na kupata faida
nyingi mbalimbali..” alisema Temu.
No comments:
Post a Comment