Mdachi huyo aliyedumu misimu miwili Old Trafford
ametupiwa virago rasmi leo ikiwa ni siku ya pili tu tangu atwae Kombe la
FA Uingereza
Manchester United wamemtupia virago Louis van Gaal, vyanzo kutoka Old Trafford vimeitaarifu Goal.Mdachi huyo aliiongoza United kutwaa Kombe la kwanza la FA tangu 2004 Jumamosi kwa kuifunga 2-1 Crystal Palace, ingawa sherehe za taji hilo zilifunikwa na tetesi kuwa angeondoka na nafasi yake kutwali wa na Jose Mourinho.
Miaka miwili ya Van Gaal Old Trafford imekuwa na mijadala mingi, midahalo ikiongozwa na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo hali kadhalika mashabiki wasiofurahishwa na aina ya uchezaji wa kikosi chake huki timu ikiwa imefunga magoli 49 tu ya Ligi msimu huu.
Mourinho amekuwa hana kazi tangu alipofukuzwa Chesea Desemba mwaka jana, lakini sasa anasubiri kutangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United. Van Gaal anaondoka Old Trafford baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili, ambapo msimu wa kwanza aliiongoza klabu kumaliza nafasi ya nne msimamo wa Ligi ya Uingereza.
Hata hivyo United wameshindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa - ambayo kwa msimu ulioisha waitolewa katika hatua ya makundi - licha ya kutumia kitita cha paundi milioni 250 kusajili wachezaji wapya kipindi cha Van Gaal.
United sasa wameshindwa kumaliza ndani ya tatu bora tangu kustaafu kwa Sir Alex Ferguson waliposhinda ubingwa wa ligi 2012-12.
Ryan Giggs alikuwa eneo la mazoezi pia Jumatatu asubuhi, lakini aliondoka saa moja baadaye. Mustakabali wa raia huyo wa Wales haujulikani wakati Jose Mourinho akiwa mbioni kutangazwa.
CHANZO: GOAL
No comments:
Post a Comment