MAFISANGO KUAGWA ASUBUHI KESHO LEADERS
MWILI wa kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango wa Simba, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari maeneo ya Tazara, Dar es Salaam unatarajiwa kuagwa kesho saa 2 asubuhi katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
Meneja wa Simba SC, Nicodemus Menard Nyagawa ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, baada ya zoezi la kuagwa kukamilika, mwili huo utasafirishwa kwa ndege ya shirika la ndege ya kenya, KQ kwenda Kigali, Rwanda kwa shughuli za mazishi.
Nyagawa ametoaq wito kwa wapenzi wote wa Simba kujitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa marehemu Mafisango, aliyekuwa kiungo tegemeo wa klabu hiyo katika msimu wake mmoja tu wa kuichezea tangu ajiunge nayo, akitokea Azam FC.
Mafisango alifariki kwa ajali ya gari akiwa anarejea nyumbani kwake, kutoka disko na kwa sasa mwili wake upo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Nyagawa alisema Mafisango aliyekuwa anaendesha mwenyewe gari lake, alikuwa anajaribu kumkwepa dereva wa pikipiki na kwa bahati mbaya akaingia mtaroni na kuumia kabla ya kufariki dunia.
Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 mjini Kinshasa, DRC alikoanzia soka kabla ya kuhamia Rwanda, ambako baadaye alichukua uraia wa nchi hiyo.
Kabla ya kuja Tanzania alichezea APR ya Rwanda. Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea Simba ilikuwa dhidi ya Al Ahly Shandy nchini Sudan Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.
Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo Simba katika safu ya kiungo na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange 'Kaburu' alisema kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao.
Pamoja na kucheza kama kiungo, Mafisango pia anamudu kucheza nafasi ya beki wa kushoto na beki wa kati.
Japokuwa alikuwa kiungo, lakini pia alikuwa hodari wa kufunga mabao na msimu huu imeshuhudiwa akiifungia Simba mabao 11 katika Ligi Kuu na manne kwenye Kombe la Shirikisho.
Wakati Simba ikijiandaa kwenda kurudiana na ES Setif katika mechi ya hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho, ilitaka kumuacha kiungo huyo baada ya kumsimamisha kwa utovu wa nidhamu- ingawa baadaye busara ilitumika akasafiri na timu baada ya kuomba radhi.
Tuhuma aza utovu wa nidhamu kwa Mafisango zilianza kumuandama tangu akiwa Azam FC na ndiyo sababu kubwa ya klabu hiyo kumuacha aende Simba licha ya kwamba ilimsajili kwa gharama kubwa kutoka APR ya Rwanda.
Pamoja na yote, ndani ya Uwanja Mafisango alikuwa suala jingine- anajituma mno na alikuwa ana msaada mkubwa timu. Kwa sababu ya nidhamu aliachwa hadi timu ya taifa, Amavubi- lakini kwa soka yake maridadi akiwa Simba, kocha mpya wa timu hiyo Milutin Sredojevic 'Micho' safari hii alimuita kikosini, ingawa kabla ya kupanda ndege kurejea nyumbani kuitikia wito huo, umauti umemkuta.
Poleni wana Simba wote, pole kwa ndugu, jamaa na familia ya Mafisango. Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele. Amin. Mungu aiweke pema peponi Roho ya Marehemu.
TEVEZ AMUAMBIA FERGUSON; "USIJIONE RAIS WA ENGLAND"
Published: 16th May 2012
CARLOS TEVEZ ameanzisha rasmi vita ya maneno na kocha wake wa zamani, Alex Ferguson — akimuambia: “Unafikiri wewe ni rais wa England.”
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Manchester City alibeba bangto lililoandikwa ‘RIP Fergie’
wakati sherehe za klabu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England Jumatatu wiki
hii.
City
iliomba radhi kwa kitendo hicho cha Tevez, lakini Muargentina huyo amegoma
kusema samahani.
Alisema:
“Inaonekana kama Ferguson ni rais wa England.
“Wakati
wote anazungumza mambo yasiyo na maama juu yangu na sijawahi kumuambia aniombe
msamaha.
“Wakati
mtu mmoja anapomtania mwingine pia, unaweza kuomba radhi. Lakini siwezi kusema
swamahani.”
Bango
alilobeba Tevez kwa mashabiki, ilikuwa ni kukumbushia kauli ya Ferguson kabla ya
mechi ya wapinzani hao wa jiji la Manchester mwaka 2009.
Aliulizwa
kama itafikia Man United watakuwa vibonde wa City, Ferguson akasema: “Siyo
nikiwa hai,".
Wednesday, May 16, 2012
MAN CITY YAFANYA KUFURU KWA IBRAHIMOVIC
Last Updated: 17th May 2012
MANCHESTER CITY imetenga dau la pauni Milioni 25 kwa ajili ya mshambuliaji wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic.
Kocha
Roberto Mancini atampa Msweden huyo mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki.
Hiyo
dhahiri itamfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika Ligi Kuu
ya England, akimpiku kiungo wa City, Yaya Toure anayelipwa pauni250,000 kwa
wikki.
Lakini
huwezi kuamini eti Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 30, ameomba muda kuifikiria
ofa hiyo.
Hii
ni mara ya pili kwa Mancini kujaribu kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa
Barcelona, Juventus na Inter Milan atue Eithad na safari hii anatarajia
kufanikiwa.
Mancini
alimsajili Ibrahimovic wakati akiwa Inter Milan kwa pauni Milioni 22 mwaka
2006.
Na
sasa yuko tayari kubomoa beki kumnasa ngongoti huyo mwenye urefu wa futi 6 na
inchi 5 kwa dau tamu la usajili, posho kibwenana marupurupu mengine kibao —
sambamba na mshahara mkubwa kwa wiki.
MAN UNITED WAMTAKA VAN PERSIE
KLABU ya Manchester United
imeamua kuungana na mahasimu wao, Manchester City katika kuwania saini ya
Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka
28-mkataba wake Emirates unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.
KLABU
ya Juventus imejitoa kwenye mbio za kuwania saini ya Van Persie, ikihofia
haitaweza kushindana kwa dau na Manchester City na sasa wanahamishia mawindo
yake kwa mshambuliaji wa Napoli, Edison Cavani.
Manchester
City inajiandaa kubomoa benki na kutumia kiasi cha pauni Milioni 28.7 ili
kumnasa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 27 kutoka Athletic Bilbao, Fernando Llorente.
MCHEZAJI
anayewani na Chelsea na Everton, Oscar Cardozo ameambiwa anaweza kuondoka
Benfica. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, pia anazivutia klabu za CSKA
Moscow na Rubin Kazan.
KIUNGO
wa Montpellier na Morocco, Younes Belhanda mwenye umri wa miaka 22, amepuuza
tetesi za kutakiwa na Arsenal na Liverpool kwa kusema kwamba anataka kubaki kwa
vinara hao wa Ligi Kuu ya Ufaransa msimu ujao.
KIUNGO
wa Borussia Dortmund, Shinji Kagawa amesema alifanya mazungumzo na kocha wa
Manchester United, Sir Alex Ferguson. "Alikuwa ana vitu vizuri vya kuniambia,"
alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan, mwenye umri wa miaka 23.
KLABU
ya Fulham imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Huddersfield na Scotland, Jordan Rhodes, ikimpata kwa dau la pauni Milioni
3.5 nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, ikizipiku Norwich, Aston Villa na West
Ham.
DESCHAMPS, AVB, KLOPP KUMRITHI DALGLISH LIVERPOOL...
KOCHA
wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas, kocha wa Borussia Dortmund, Juergen
Klopp na wa Marseille, Didier Deschamps ni miongoni mwa walimu waliomo kwenye
orodha ya makocha wanaotakiwa kurithi mikoba ya Kenny Dalglish
Liverpool.
BEKI
Rio Ferdinand hamemtupia lawama kocha wake wa Manchester United, Alex Ferguson
kwa amechangia kutemwa kwake katika kikosi cha timu ya taifa ya England
kitakachocheza fainali za Euros, baadfa ya Mscotland huyo kuulizwa kama beki
huyo mwenye umri wa miaka 33 kama anaweza kucheza mechi za kimataifa.
MSHAMBULIAJI
wa Manchester City, Emmanuel Adebayor amesema chaguo lake la kwanza msimu ujao
ni kuendelea kuichezea Tottenham, ambako amekuwa akicheza kwa mkopo msimu mzima.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, pia ana ofa ya kwenda kukipiga Marekani
na Urusi.
VAN PERSIE AWAKATALIA MAN CITY, ETI WALIMPA PAUNI 130,000 KWA WIKI
Published: 16th May 2012
ROBIN VAN PERSIE sasa yuko mguu nje, mguu ndani Arsenal- baada ya mazungumzo ya jana kati yake na kocha Arsene Wenger kumalizika bila kufikia mwafaka.
The
Gunners walitumaini kumtuliza kwa mkataba mpya wa mika mitatu ambao ndani yake
walimuandalia mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki ambao walidhani ungemfanya
apuuze ofa mabingwa wapya wa Ligi Kuu, Manchester City na kubaki Emirates.
Lakini
mazungumzo ya jana, yalivunjika bila makubaliano.
Shaka
imetawala sasa kwamba Van Persie anaweza kuondoka Arsenal na kuhamishia cheche
zake Etihad, huku ikielezea kiu yake ya wazi wazi ya kumnasa mfungaji huyo bora
wa Ligi Kuu.
Habari
zilizopatikana jana zimesema kwamba, Arsenal iko tayari kucheza ngoma ngumu
iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, Van Persie hataki kubaki ba
watamlazimisha amalizie mwaka wake mmoja uliobaki katika mkataba wake wa
sasa.
Mholanzi
huyo aliyeifungia mabao 37 The Gunners msimu huu katika Ligi Kuu, ameshinda tuzo
za Mwanasoka Bora wa Mwaka ya PFA na Waandishi wa Soka.
GYAN, DEDE AYEW WATEMWA KIKOSI CHA GHANA
Mshambulizi matata Asamoah Gyan hayuko kwenye kikosi cha timu ya
taifa ya Ghana kilichotajwa na Kocha Kwesi Appia.
Wengine
waliotemwa ni mwamba wa Chelsea Michael Essien na Andre 'Dede' Ayew ambaye ana
jeraha.Gyan ameachwa nje hata baada ya shinikizo kwamba ajumuishwe kwenye kikosi
cha Ghana.
John
Paintsil na aliyekuwa nahodha wa Ghana John Mensah nao pia hawamo.
katiuka
kikosi chake kipya kocha Appiah amewajumuisha wachezaji sita wapya wengi wakiwa
wanachezea soka la kulipwa ulaya. hata hivyo amejumuisha wachezaji tisa toka
ligi ya nyumbani.
Asamoah
Gyan aliamua kujiondoa toka timu ya taifa baada ya kushambuliwa na mashabiki
baada ya uchezaji wake duni katika michuano ya kombe la bara afrika la hivi
majuzi.
ilikuwa
inatarajiwa kwamba angelirejea katika timu kabla ya mwezi ya Juni.
kwa
upande wa Ayew , alifanyiwa upasuaji hivi majuzi nae Essien alisema
atashughulika zaidi na timu yake ya Chelsea.
KIKOSI
KAMILI: Makipa
Adam Kwarasey (Stromsgodset, Norway), Robert Dabuo (Wa All Stars), Daniel Adjei
(Liberty Professionals), Ernest Sowah (Berekum Chelsea)
Mabeki:
Samuel Inkoom (Dnipro, Ukraine), Daniel Opare (Standard Liege, Belgium),
Harrison Afful (Esperance, Tunisia), Richard Kissi Boateng (Berekum Cheslea),
Masawudu Alhassan (Genoa, Italy), John Boye (Rennes, France), Lee Addy (Dalian
Aerbin, China), Daniel Addo (Arsenal Kyiv, Ukraine) Rashid Sumaila (Dwarfs),
Jerry Akaminko (Manisaspor, Turkey), Isaac Vorsah (Hoffenheim, Germany)
Viungo:
Anthony Annan (Vitesse Arnhem, Netherlands), Derek Boateng (Dnipro, Ukraine),
Emmanuel Agyemang Badu (Udinese ,Italy), Rabiu Mohammed (Evian, France) Richard
Mpong (Medema) Albert Adomah (Bristol City, England), Christian Atsu (Rio Ave,
Portugal), Ishamel Yartey, (Servette, Switzerland), Sulley Muntari (AC Milan,
Italy), Kwadwo Asamoah (Udinese, Italy).
Washambuliaji:
Jordan Ayew (Marseille, France), Dominic Adiyiah (Arsenal Kyiv, Ukraine), Ben
Acheampong (Kotoko), Emmanuel Baffour (New Edubiase), Emmanuel Clottey (Berekum
Chelsea)
MAESTRO WA SIMBA MAFISANGO AFARIKI DUNIA
KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango wa Simba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tazara, Dar es Salaam.
Mafisango amefariki kwa ajali ya gari akiwa anarejea nyumbani kwake, kutoka disko na kwa sasa mwili wake upo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Meneja wa Simba SC, Nicodemus Menard Nyagawa amethibitisha kifo cha mchezaji huyo na amesema hilo ni pigo kubwa kwa klabu hiyo.
Nyagawa alisema Mafisango aliyekuwa anaendesha mwenyewe gari lake, alikuwa anajribu kumkwepa dereva wa pikipiki na kwa bahati mbaya akaingia mtaroni na kuumia kabla ya kufariki dunia.
Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 mjini Kinshasa, DRC alikoanzia soka kabla ya kuhamia Rwanda, ambako baadaye alichukua uraia wa nchi hiyo.
Kabla ya kuja Tanzania alichezea APR ya Rwanda. Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea Simba ilikuwa dhidi ya Al Ahly Shandy nchini Sudan Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.
Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange Kaburu alisema kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao. Poleni wana Simba wote, pole kwa ndugu, jamaa na familia ya Mafisango. Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele. Amin. Mungu iweke pema peponi Roho ya Marehemu.
No comments:
Post a Comment