Heka heka langoni mwa timu ya Ndanda. |
Kikosi cha Ndanda kilianza katika mechi dhidi ya Yanga Nangwanda Mtwara. Timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0 |
Juma Mohamed, Mtwara.
Klabu ya
soka ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara imeendelea kuwabania Yanga kuweza kuapata
ushindi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona ambapo katika mchezo wa leo wa ligi
kuu ya Vodacom Tanzania Bara wamelazimishwa suluhu ya bila kufungana.
Mchezo huo
ulioamriwa na mwamuzi Hance Mabena kutoka jijini Tanga akisaidiwa na Nicholous
Makaranga na Haji Mwalukuta, ulikuwa ni wa kushambuliana zamu kwa zamu huku
timu zote zikijaribu kufanya madiliko kadhaa ambayo hata hivyo hayakuzaa
matunda.
Kikosi cha Yanga kilianza katika mechi dhidi ya Ndanda. Mechi hiyo iliisha kwa suluhu ya 0-0 |
Yanga
walimbadilisha Deus Kaseke ambaye alionyeshwa kadi ya njano na nafasi yake
kuchukuliwa na Juma Maadhi, huku Ndanda wakimtoa kiungo Salum Minelly ambaye
pia alionywa kwa kadi ya Njano na nafasi yake kuchukuliwa na Nassoro Kapama.
Baada ya
mchezo huo makocha wa timu zote mbili Juma Mwambusi ambaye ni msaidizi wa Hans
Van Pluijm wa Yanga na Hamimu Mawazo wa Ndanda wameeleza maoni yao.
“Hii ni mara
ya pili tunacheza na mara ya kwanza tulifungwa hii tumetoka sare, kwahiyo
siwezi kusema hatuwezi kushinda uwanja wa Nangwanda..lakini kikubwa ni hali ya
hewa na hali ya uwanja kwa tulitegea kutocheza mpira nzuri..” alisema Juma
Mwambusi kocha msaidizi wa Yanga.
Naye Hamimu
Mawazo wa Ndanda FC alisema kutokana na alikitazama kikosi chake katika mchezo
huo amegundua kuwa wameanza kujirekebisha makosa yaliyokuwa yakiwatatiza mwanzo
na kwamba kadiri muda unavyokwenda watazidi kuwa sawa.
Kwa upande
wa mashabiki, Ndanda wameonekana kuyapokea vizui matokeo hayo na kuahidi
kufanya vizuri katika mchezo ujao na Kagera, huku wale wa Yanga wakielekeza
lawama zao kwa mwamuzi.
Hii ni mara ya pili kwa Yanga kushindwa kupata matokeo ya ushindi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara ambapo misimu miwili iliyopita mabingwa hao watetezi wa VPL waliwahi kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho wa ligi
Wachezaji wa timu za Ndanda na Yanga wakisalimia mashabiki muda mfupi kabla ya kuanza mchezo wao. |
No comments:
Post a Comment