HATIMA YA YANGA SASA IPO KWA ALEX MGONGOLWA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania
(TFF) linatafakari mustakabali wa Yanga, kufuatia Wajumbe kadhaa wa Kamati ya
Utendaji ya Yanga akiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga
kujiuzulu.
Ofisa Habari wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY
mchana huu kwamba, Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeliandikia barua shirikisho
hilo, ikitaka mwongozo juu ya hilo.
Wambura amesema kwamba, kwa
kuzingatia hilo, TFF imepeleka suala hilo kwa Kamati yake ya Sheria, Maadili na
Hadhi za Wachezaji ili itoe maoni yake kisheria ya nini kinafanyike kuhakikisha
Yanga inaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Amesema Kamati ya Sheria,
Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa (pichani)
inatarajia kukutana leo jioni kushughulikia suala hilo na baadaye Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga pamoja na Kamati ya Uchaguzi ya TFF zitapewa maelekezo ya
kufanya kwa kuzingatia taratibu zilizopo.
LIGI YA TFF KUANZA MEI 27
MICHUANO ya Ligi ya Taifa
inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inaanza Mei 27 mwaka huu katika vituo vitatu
tofauti huku Ashanti United ya Ilala na Polisi ya Mara zikifungua dimba katika
Kituo cha Musoma.
Ligi hiyo ambayo inatarajia
kumalizika Juni 12 na 13 mwaka huu itashuhudia mechi mbili kwa siku katika kila
kituo, huku ya kwanza ikichezwa saa 8 mchana na kufuatiwa nay a pili 10
jioni.
Mechi za ufunguzi Kituo cha
Musoma ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma
ni Flamingo ya Arusha dhidi ya Forest ya Kilimanjaro (saa 8 mchana) wakati saa
10 jioni ni Ashanti United na Polisi.
Kituo cha Kigoma siku ya
ufunguzi kutakuwa na mechi moja tu itakayoanza saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja
wa Lake Tanganyika kati ya Mwadui ya Shinyanga na JKT Kanembwa ya Kigoma. Siku
inayofuata ni CDA (Dodoma) vs Majimaji ya Tabora (saa 8 mchana) na Bandari ya
Kagera vs Pamba ya Mwanza (saa 10 kamili jioni).
Tenende ya Mbeya na Kurugenzi
ya Iringa ndizo zitakazoanza saa 8 mchana kwenye Kituo cha Mtwara na kufuatia na
mechi kati ya Mpanda Stars ya Rukwa na Ndani ya Mtwara kuanzia saa 10 kamili
jioni. Mechi hizo zitachezwa katika Uwanja wa Umoja.
NYOTA WA ATLETICO MADRID KUIONGOZA MALAWI DHIDI YA TAIFA STARS KESHO
Robin Ngalande |
IKIONGOZWA na mchezaji wa timu ya vijana ya Atletico
Madrid ya Hispania, Robin
Ngalande Malawi The Flames kesho inatarajiwa kuwa mgeni wa
Tanzania, Taifa Stars katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Makocha wa timu zote mbili,
Kim Poulsen wa Taifa Stars na Kinnah Phiri wa The Flames wamezungumzia umuhimu
wa mechi hiyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo (Mei 25
mwaka huu) ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Kim ambaye hiyo itakuwa mechi
yake ya kwanza tangu asaini mkataba wa kuinoa Stars, amesema baada ya mazoezi ya
siku kumi hicho ndicho kipimo chake cha kwanza na cha mwisho kabla ya kucheza na
Ivory Coast kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayofanyika ugenini Juni
2 mwaka huu.
“Wachezaji wangu wamekuwa
wakipokea mafunzo vizuri ingawa Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu hatakuwepo kwa
vile ni majeruhi. Bila shaka baada ya mazoezi ni lazima ujipime, hivyo mechi hii
ni muhimu kwangu ukizingatia kuwa kwenye ubora wa viwango vya FIFA, Malawi wako
juu yetu,” amesema Kim.
Naye Phiri ambaye ni mchezaji
wa zamani wa kimataifa wa Malawi amesema awali aliombwa mechi na Misri, lakini
akaamua kucheza na Taifa Stars kwa vile anaamini kitakuwa kipimo kizuri kwake
kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Kenya itakayofanyika
Juni 2 mwaka huu jijini Nairobi.
“Nimekuja na wachezaji 20
ambapo nusu yao wanacheza mpira wa kulipwa nje ya Malawi, wengi wakiwa Afrika
Kusini lakini wapo pia kutoka Msumbiji na mmoja anacheza Hispania katika timu ya
vijana ya Atletico Madrid. Tumejianda si kwa mechi hii tu, bali pia dhidi ya
Kenya na baadaye Nigeria ambao tutacheza nao numbani Juni 9 mwaka huu,” amesema
Phiri ambaye kwenye benchi lake la ufundi anasaidiwa na Young
Chimodzi.
Viingilio katika mechi hiyo ni
sh. 3,000 kwa viti vya kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh.
15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A inayochukua watazamaji 748 tu itakuwa sh.
20,000.
BLATTER AKATAA MIKWAJU YA PENALTI, ASEMA ITALETA BALAA
RAIS wa FIFA, Sepp
Blatter amesema kwamba soka inaweaza kugeuka janga iwapo mechi itaamuliwa kwa
mikwaju ya penalti.
Licha ya kutawala mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ndoto za Bayern Munich kutwaa taji hilo la Ulaya, zilizimwa na Chelsea kwa bahati nasibu ya mikwaju ya penalti Jumamosi ya wiki iliyopita.
Blatter anaamini uhalisia wa soka unapotea inapofikia mechi inaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, na amesema kwamba ufumbuzi utatafutwa baadaye.
"Soka inaweza kuwa janga unakwenda kwenye mikwaju ya penalti," Blatter alisema kwa mujibu wa BBC. "Soka haiwezi kuwa ya mmoja kwa mmoja, inapofikia kwenye mikwaju ya penalti soka inapoteza uhalisi wake.
"Natumai Franz Beckenbauer na Kamati yake ya [FIFA Task Force] 2014 watatuonyesha njia, hata isiwe leo, lakini baadaye."
Katika jitihada za kurekebisha zaidi mchezo huo, FIFA imetangaza kwamba mechi ya kirafiki kati ya England na Ubelgiji Juni 2, itatumika kufanyia majaribio sheria ya teknolojia kwenye mstari wa lango, ili kujua kama mpira umevuka, au haujavuka mstari.
Licha ya kutawala mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ndoto za Bayern Munich kutwaa taji hilo la Ulaya, zilizimwa na Chelsea kwa bahati nasibu ya mikwaju ya penalti Jumamosi ya wiki iliyopita.
Blatter anaamini uhalisia wa soka unapotea inapofikia mechi inaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, na amesema kwamba ufumbuzi utatafutwa baadaye.
"Soka inaweza kuwa janga unakwenda kwenye mikwaju ya penalti," Blatter alisema kwa mujibu wa BBC. "Soka haiwezi kuwa ya mmoja kwa mmoja, inapofikia kwenye mikwaju ya penalti soka inapoteza uhalisi wake.
"Natumai Franz Beckenbauer na Kamati yake ya [FIFA Task Force] 2014 watatuonyesha njia, hata isiwe leo, lakini baadaye."
Katika jitihada za kurekebisha zaidi mchezo huo, FIFA imetangaza kwamba mechi ya kirafiki kati ya England na Ubelgiji Juni 2, itatumika kufanyia majaribio sheria ya teknolojia kwenye mstari wa lango, ili kujua kama mpira umevuka, au haujavuka mstari.
TASWA YAMPA 'BRAVO' MHARIRI TANZANIA DAIMA KUINGIA RT
CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pongezi kwa Mhariri
wa Habari za Michezo wa gazeti la Tanzania Daima, Tullo Chambo (pichani kushoto)
kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania
(RT).
Katibu
Mkuu wa TASWA, Amiri Mhando ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu
kwamba, Chambo alitwaa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa RT uliofanyika
Jumapili mjini Morogoro, ambapo ni miongoni mwa wajumbe wapya walioingia kwenye
chama hicho.
Wengine
walioshinda ni Anthony
Mtaka ambaye anakuwa Rais mpya wa RT, wakati Makamu wa Rais Utawala ni William
Kallaghe, Makamu wa Rais Ufundi, Dk. Ahmed Ndee, Katibu Mkuu, Suleiman Nyambui,
Katibu Msaidizi, Ombeni Zavalla, Mhazini, Is-Haq Suleiman.
Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji ni Mwinga Mwanjala, Meta Petro, Peter Mwita, Rehema Killo,
Lwiza John, Zakaria Barrie, Zakaria Gwanda, Robert Kalyahe na Christian
Matembo.
TASWA
inatambua Chambo ni mwanahabari mzoefu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mhariri wa
habari za michezo na ni mtu mwenye kujua mambo mengi yanayohusu riadha, hivyo
atakuwa kiungo muhimu kwa watu wa riadha, pia atakuwa kiongo kizuri kwa
waandishi wa habari za michezo kuhusiana na mambo ya riadha.
TASWA
inaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kadri itakavyoweza na inamtakia kila la
heri, huku ikiamini hatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa RT waliomuamini
wakamchagua kushika wadhifa huo.
Pia
Taswa inawapongeza viongozi wote wa RT walioingia madarakani Jumapili, ikiamini
watakuwa chachu ya mafanikio ya riadha hapa nchini.
HALI BADO TETE YANGA LICHA YA NCHUNGA KUJIUZULU
KIKAO cha Kamati ya Utendaji
ya Yanga kujadili barua ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd Baharagu
Nchunga kujiuzulu kimeshindwa kufanyika leo, kutokana na safu
kutotimia.
Katibu Mkuu wa Yanga,
Celestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba,
Mbaraka Igangula yupo Afrika Kusini wakati Khalifa Mgonja yupo Arusha,
Mwesigwa alisema kwa sababu
hiyo, wanasubiri Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji wafike Dar es Salaam ndipo
kikao kifanyike. Wakati huo huo, Wazee wa klabu hiyo walikutana na waandishi wa
Habari leo mchana makao makuu ya klabu na kusema kwamba, hawamtambui Mjumbe
yeyote wa Kamati ya Utendaji, kwani Nchunga ameondoka na watu wake
wote.
Aidha, baadhi ya Wajumbe
waliotangaza kujiuzulu wameanza kuzikana barua zao, wakidai walilazimika
kuandika kutokana na vitisho walivyokuwa wakipewa. BIN ZUBEIRY iliwasiliana na
Mwanasheria wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alex Mgongolwa kutaka
ufafanuzi zaidi juu ya sakata la klabu hiyo, lakini akasema yuko kwenye
kikao.
Wakati BIN ZUBEIRY ikiwa
imetega rada zake kwa Mgongolwa hadi hapo atakapomaliza kikao, taarifa zaidi
zinasema kikao hicho kinahnusu syala hilo hilo la Yanga na atalitolea tamko
leo.
Jana, Nchunga alitangaza
kujiuzulu Uenyekiti wa Yanga, akisema timu anaikabidhi kwa Baraza la Wadhamini,
ambalo kwa sasa linaundwa na wajumbe watatu, Mama Fatuma Karume, Deo
Filikunjombe na Francis Kifukwe.
COLE AANDALIWA MKATABA MPYA MNONO CHELSEA SAWA NA WA TORRES
EXCLUSIVE
By Wayne Veysey | Chief Correspondent
By Wayne Veysey | Chief Correspondent
KLABU ya Chelsea, iko tayari kumpa ofa ya mkataba mpya
Ashley Cole ambao utamuweka Stamford Bridge kwa kipindi chote kilchobaki cha
maisha yake ya soka.
Beki huyo amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa
sasa na klabu hiyo inataka kumfunga kwa mkataba mpya mwanzoni mwa msimu ujao,
kwa mazungumzo ambayo yataanza hivi karibuni, baada ya beki huyo wa kushoto
kuonyesha soka ya nguvu msimu huu, akitoa mchango mkubwa kwa timu kutwaa taji la
Ligi ya Mabingwa.
Chanzo cha habari, kimeiambia Goal.com, ambako BIN
ZUBEIRY imeipata habari hii, kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 31
atapewa mkataba wa makia mitatu na kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa
vizuri katika klabu hiyo, sambamba na akina John Terry, Frank Lampard na
Fernando Torres.
Mshahara wake wa sasa inasemekana ni kiasi cha pauni
120,000 kwa wiki, wakati Barcelona ni miongoni mwa klabu ambazo zinamtaka sana
Cole na kwa sasa inasikilizia tu kama Chelsea itashindwana naye, iingie msituni
kusaka saini ya mchezaji huyo, aliyesajiliwa Stamford Bridge katika mazingira ya
utatanishi kutoka Arsenal mwaka 2006.
Hadi sasa hakuna dalili kwamba Cole anataka kuondoka London
na baada ya kumaliza msimu na mataji mawili, kwa sasa yuko likizo Los Angeles,
Marekani kabla ya kujiunga na timu ya taifa ya England wiki ijayo kujiandaa na
mchezo wa kirafiki dhidi ya Ubelgiji Juni 2, mwaka huu.
Pamoja na kurefusha maisha ya Cole, Stamford Bridge, pia
Chelsea inataka kuwaongezea mikataba Michael Essien, Florent Malouda na Frank
Lampard, ambao wanamaliza 2013.
Kama BIN ZUBEIRY ilivyoinukuu Goal.com Jumatano kwamba
Salomon Kalou anaweza kutemwa, sasa suala lake litatatuliwa wiki ijayo, wakati
Jose Bosingwa anajiandaa kutemwa licha ya kuwa beki chaguo la kwanza kulia
katika kikosi kilichomaliza msimu na mataji mawili.
WANAUME FAMILY KUMPA TAFU DOGO ASLAY DODOMA
Wanaume Family |
KUNDI
zima la TMK Wanaume Family la Temeke jijini Dar es Salaam, litasindikiza
utambulisho wa msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini Aslahi Isihaka
‘Dogo Aslay’ litakalofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma na ukumbi wa Royal
Village mjini humo.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi jijini Dar es Salaam jana mratibu wa onesho hilo Jackline Masano wa
Kampuni ya Ruhazi Promotion ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa TMK Family
watafanya vituo vyao kwenye onesho hilo litakalofanyika Jumamosi Juni 9,2012
kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Alisema TMK Family wanaungana
na wasanii kutoka kituo cha Mkubwa na Wanawe cha Temeke Sandali jijini katika
kumsindikiza msanii huyo aliye gumzo hivi sasa kutona na wimbo wake ‘Naenda
Kusema’.
“Tunapenda kuwaambia wapenzi
wa muziki wa mjini Dodoma na maeneo jirani kwamba Kampuni ya Ruhazi Promotion
imekubaliana na TMK Family hivyo mchana wa Jumamosi Juni 09, 2012 kuanzia saa
6:00 mpaka saa 12:00 jioni itakuwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma na litaanza
saa 2:00 usiku hadi saa 6:30 usiku kwenye ukumbi wa Royal Village,” alisema
Jackline Masano.
Alisema pamoja na kwamba
onesho hilo litapambwa na wasanii wengi lakini kiingilio kitakuwa shilingi 5,000
tu kwa wakubwa na shilingi 1,000 kwa watoto ili kuwawezesha wapenzi wengi zaidi
kukimudu ambapo watapata burudani ya uhakika.
Aliongeza kwamba hivi sasa,
wanaendeelea kufanya mazungumzo na wasanii wengine watakaopamba maonesho hayo
yote na kwamba pindi mazungumzo yatakapokamilika watawaweka
hadharani.
KILIMANJARO PREMIUM LAGER KUENDELEA KUDHAMINI KOMBE LA TAIFA
George Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Beer |
Gaudence Mwaikimba, mfungaji
bora wa taifa Cup msimu uliopita akiwa na mabingwa watetezi Mbeya |
Akizungumza na BIN
ZUBEIRY jana usiku katika mahojiano maalum, Nyumbani Lounge, Oysterbay,
Dar es Salaam, Kavishe alisema kwamba Kilimanjaro Premium Lager bado ni
wadhamini wa Taifa Cup na mwaka huu itafanyika kama kawaida.
Hata hivyo, alipoulizwa juu ya
ukimya wa maandalizi hadi sasa, Kavishe alisema; “Sisi tunawasubiri TFF
(Shirikisho la Soka Tanzania), wao ndio wanatakiwa kutupa mwongozo, sisi ni
wadhamini tu, tunawezesha, ila mipango yote na nini, ni TFF wao wenyewe,”alisema
Kavishe ambaye jana bia yake ilifanya pati la uzinduzi wa kampeni ya Kilimanjaro
Premium Lager 100% TZ Flava kwenye ukumni wa Nyumbani Lounge.
Kumekuwa na wasiwasi wa Kombe
la Taifa ama kutofanyika kabisa mwaka huu, au kufanyika bila ya udhamini, baada
ya Kilimanjaro Premium Lager ambao pia ni wadhamini wa klabu za Simba na Yanga,
kuingia mkataba wa kuidhamini Taifa Stars, ambayo awali ilikuwa inadhamini na
bia ya Serengeti Premium Lager.
Lakini kauli hii ya Kavishe
inakuja kuondoa wasiwasi huo na mikoa sasa inaweza kuendelea na maandalizi yake
kama kawaida.
Thursday, May 24, 2012
MAN CITY WATAKA KUNG'OA KIFAA KINGINE BARCA
Martinez |
Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
MAN CITY WAIPA FEDHA NA MCHEZAJI BARCELONA ILI WAMTWAE DANI ALVES
KLABU ya Manchester City
inajiandaa kuchukua mchezaji mwingine Barcelona, beki nyota Dani Alves, mwenye
umri wa miaka 29. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, City wametoa ofa ya
pauni Milioni 12 na kuwapa Aleksandar Kolarov pia.
MSHAMBULIAJI
wa Manchester City, Mario Balotelli ameonyesha nia yake ya kubaki katika klabu
hiyo, akikanusha uvumi kwamba anataka kurejea Italia kujiunga na AC
Milan.
KLABU
ya Manchester United inajiandaa kuboresha ofa yake ya ya pauni Milioni 13
kumnasa kiungo Shinji Kagawa mwenye umri wa miaka 23, kutoka Borussia
Dortmund.
KLABU
ya Tottenham ipo karibu kumsaini beki wa kati Jan Vertonghen, mwenye umri wa
miaka 25, kutoka Ajax kwa dau la pauni Milioni 9.6.
KLABU
ya Arsenal iko tayari kwa mazungumzo ya kumchukua mshambuliaji wa Montpellier,
Olivier Giroud kwa ofa ya dau la pauni Milioni 6.4, pamoja na kuwapa Marouane
Chamakh, ili wamnase mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
MWENYEKITI WIGAN AMUONYA MARTINEZ
MWENYEKITI
wa Wigan, Dave Whelan amemtaka kocha wake, Roberto Martinez kufikiria kwa
umakini juu ya kujiunga na Liverpool kufanya kazi chini ya Mkurugenzi wa
Soka.
KOCHA
wa zamani wa England, Fabio Capello anakuwa kocha wa mwingine kusitisha mpango
wa kwenda Liverpool, lakini bado ana matumaini ya kupata kazi Chelsea.
KOCHA
Steve Bruce anatakiwa na Hull City akachukue nafasi ya Nick Barmby, lakini
hawezi kuchukua uamuzi wowote kwa sasa, akiwa anavizia kurejea kwa mara ya tatu
Wigan, iwapo Martinez ataondoka.
KOCHA
wa Muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo anatakiwa na klabu ya nyumbani kwao,
Italia, Napoli baada ya mazungumzo yake na klabu yake ya sasa, Chelsea kuwa bado
hayajafanyika.
No comments:
Post a Comment