Monday, May 28, 2012

REDONDO: SIJAONA PA KWENDA - NABAKI AZAM

Redondo
Midfielder Ramadhani Chombo 'Redondo' anayecheza Azam amesema hana mpango wa kuondoka kwenye klabu hiyo kwa sasa.

Redondo alisema hakuna kitu kigumu kama kuhama katika klabu iliyokuwa na mafanikio na kwenda sehemu nyingine.

"Sina mapango wa kuondoka Azam kwa sababu ni timu nzuri na yenye malengo ya sasa na baadae hivyo kwa kuwa hapa kiwango changu kinakuwa kwani ni timu inayopanda mwaka hadi mwaka tangu kuanzishwa kwake,"alisema Chombo.

Alifafanua kuwa huwezi kucheza kwenye klabu bora ukawa sio mchezaji bora hivyo malengo yake ni kuwa mchezaji bora na anaamini atafanikiwa kwa kuwa nacheza kwenye timu bora.

Alisema mara nyingi wachezaji wanahama kutafuta maslahi, lakini kwa sasa hapa nchini hakuna timu gani yenye maslahi mazuri kwa wachezaji wake kama Azam.

"Tumekuwa washindi wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini tumefanya vizuri kwenye michuano mbalimbali tuliyoshiriki msimu huu.

"Tumetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Mapinduzi kule Visiwani sasa piga mahesabu itakuwaje kwenye msimu ujao wa ligi kama sio kuwa mabingwa wa Ligi Kuu.

"Siondoki hapa ng'o, kwa sababu mwakani tutashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ni nafasi yetu kama wachezaji tutapata fursa ya kuonyesha uwezo wetu kimataifa,"alisema Chombo.

HIVI NDIVYO SIMBA NA YANGA ZINAVYONUFAISHA WENGINE NA ZENYEWE KUBAKI OMBA OMBA KWA MATAJIRI


Wachezaji wa Simba na Yanga katika moja ya mechi zilizozikutanisha timu hizi.
KLABU kongwe za Simba ya Yanga za jijini Dar es Salaam, zinaingiza mamilioni ya pesa kila mwaka kupitia viingilio vya uwanjani, lakini kutokana na mlolongo wa makato toka taasisi mbalimbali, zimejikuta zikiambulia kiasi kidogo kulinganisha na kilichovunwa.
Mbali na makato toka taasisi hizo, likiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambalo huzoa mgao mkubwa, jambo lingine linaloziponza klabu hizo ni kutokuwa na viwanja vyao binafsi ambavyo wangeweza kuvitumia kwa ajili ya mechi zao mbalimbali na hivyo kupunguza makato.

Huu ni watu umati wa mashabikiwa timu hizi mbili kongwe. Mapato yatokanayo na viingilio vya watazamaji hawa yanaenda sehemu nyingine kwa asilimia nyingi kuliko zile wazipatazo Simba na Yanga.

Baadhi ya makato 'yanayonyonya' klabu hizo ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Chama cha Mpira wa Miguu Dar es Salaam (DRFA), gharama za uwanja kama ulinzi, usafi, umeme, tiketi nauli za ndani kwa waamuzi na kamishna, posho za kujikimu kamishna na gharama za kuwalipwa wajenzi wa uwanja, kampuni ya China (Beijing Construction).
Yanga pamoja na kumiliki Uwanja wa Kaunda, lakini haufai na hauna kiwango cha kuchezwa mechi za Ligi Kuu, na Simba haina kabisa uwanja wake binafsi zaidi ya kumiliki eneo wanalotarajia kujenga uwanja.
Azama FC mfano wa kuigwa kwa Simba na Yanga.

Klabu ya Azam FC iliyoanzishwa miaka ya karibuni ndiyo pekee nchini yenye uwanja wa kisasa unaokidhi mahitaji ya mechi za Ligi Kuu, hali ambayo imefanya kukwepa baadhi ya makato.

Kwa mfano, msimu wa 20l0/2011 na 2011/2012, mechi nne za Ligi Kuu zilizozikutanisha timu hizo, zilipatikana kiasi cha Sh979.5 milioni lakini baada ya makato kila mmoja akaambulia Sh227.7 milioni tu.
Kiasi hiki walichopata ni kidogo kulinganisha na pesa zilizoingizwa na klabu hizo katika mechi hizo nne baina yao, achilia mbali mechi nyingine za ligi hiyo na michuano mingine ya kimataifa.
Hawa ndio viongozi wa Simba na Yanga

Hii ina maana kwamba, klabu hizo zimekuwa ziingiza kiasi kikubwa cha pesa, lakini zimejikutaka zikiambulia kiasi kidogo kutokana na orodha ndefu ya makato.
Katika misimu miwili, Simba na Yanga zilikutana mara nne, mara tatu kwenye Taifa, Dar es Salaam na mara moja Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo Yanga ilishinda michezo miwili, sare moja na Simba kushinda mmoja.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, mchezo wa kwanza wa timu hizo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Oktoba 18, 2010, ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, zilipatikana Sh138 milioni.
Mapato hayo yalivunja rekodi ya yale ya awali yaliyosomeka Sh105 milioni katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Taifa Stars na Senegal mwaka juzi.
Jumla ya watazamaji 25,000 waliingia uwanjani kwenye mchezo huo kwa kiingilio cha juu Sh30,000 na cha chini 5,000, ambapo kila timu uliambulia Sh33.4 milioni.
Machi 5, 2011 katika mzunguko wa pili, ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, ziliingiza Sh243 milioni baada ya kuingia watazamaji 46,539, ambapo kiingilio cha juu kilikuwa Sh30,000 na cha chini Sh3,000. Katika mgao huo kila timu iliambulia Sh51.1 milioni.
Aidha, katika mchezo namba 78 uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Oktoba 29 mwaka jana, timu hizo zilivuna kiasi cha Sh337.5 milioni.
Pesa hizo zilipatikana baada ya kuingia uwanjani watazamaji 53,366 kwa kiingilio cha chini Sh5,000 na kila cha juu zaidi Sh20,000 kwa siti za VIP A. Yanga ilishinda bao 1-0.
Baada ya makato, kila timu iliweka mfukoni kiasi cha Sh77milioni, na mchezo wa mwisho ya Ligi Kuu msimu huu ulikuwa Mei 6, ambapo watazamaji 41,733 waliingia uwanjani.
Kiasi cha Sh260.9 zilipatikana na kila timu ikaweka mfukoni kiasi cha Sh62.6milioni, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga.
Katika misimu hiyo miwili, msimu wa mwaka 2011/2012 ndiyo uliokuwa na mavuno mengi kwa timu hizo kulinganisha na msimu uliotangulia kwa tofauti ya Sh61 milioni.
Akiongelea hali hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwasigwa alisema mfumo wa makato wa unaziumiza kwa kiasi kikubwa klabu ambazo msingi mkubwa wa kuziendesha utegemea mapato ya milangoni.
"Kweli makato ni makubwa sana, kuna mlolongo mrefu wa gharama ambazo zinalipwa toka kwenye viingilio. Kwa hali hii, klabu zetu haziwezi kusonga mbele," alisema Mwasigwa.
Mwasigwa alisema wamezungumza mara kwa mara na TFF kuhusu makato hayo, lakini hakuna ambalo limeweza kufikiwa mpaka sasa. "Tunahitaji mabadiliko yenye kuzinufaisha klabu na siyo kuzinyonya."
source: www.mwananchi.co.tz

KALI YA LEO: BAADA YA KUDUNDWA NA KOCHA WAKE - ADAM LJAJIC AFUNGIWA KWA KUSHINDWA KUIMBA WIMBO WA TAIFA

Chama cha soka cha Serbia kimesema kiungo Adam Ljajic amesimamishwa kuichezea timu ya Taifa kwa kushindwa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya mechi dhidi ya Spain.

Ni adhabu kubwa kwa mchezaji ukilinganisha na kosa, lakini ukiwa na kocha aina ya mtu kichaa kama Sinisa Mihajlovic - then adhabu kama hizi inabidi uzizoee tu.

Chama cha soka kimesema Mihajlovic aliamua kumrudisha nyumbani Ljajic kwa sababu alishindwa kufuata masharti na sheria alizoweka kocha wake kwa wachezaji kuimba wimbo wa taifa kabla ya mechi.

Kweli huu sio mwezi mzuri kwa Adam, baada ya kupigwa mangumi na kocha wake wa Fiorentina sasa hivi ametemwa kuichezea timu ta taifa.

GOLI LA SIKU: MAREKANI ILIPOWAUA SCOTLAND 5-1


OFFICIAL: EDEN HAZARD ATHIBITISHA KUJIUNGA NA CHELSEA

Kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa Twitter Eden Hazard amethibitisha atajiunga na Chelsea.

Ameandika "Najiunga na mabingwa wa ulaya,"

BREAKING NEWS: HIKI NDIO KIKOSI CHA WAJERUMANI KWA AJILI YA EURO



Squad:
Goalkeepers: Manuel Neuer (Bayern Munich), Tim Wiese (Werder Bremen), Ron-Robert Zieler (Hanover)

Defenders: Holger Badstuber (Bayern Munich), Jerome Boateng (Bayern Munich), Benedikt Hoewedes (Schalke 04), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Philipp Lahm (Bayern Munich), Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund), Per Mertesacker (Arsenal/ENG)

Midfielders: Lars Bender (Bayer Leverkusen), Toni Kroos (Bayern Munich), Thomas Mueller (Bayern Munich), Mesut Ozil (Real Madrid/ESP), Andre Schuerrle (Bayer Leverkusen), Sami Khedira (Real Madrid/ESP), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Mario Goetze (Borussia Dortmund), Ilkay Guendogan (Borussia Dortmund)

Forwards: Mario Gomez (Bayern Munich), Miroslav Klose (Lazio/ITA), Lukas Podolski (Arsenal/ENG), Marco Reus (Borussia Moenchengladbach)

EXCLUSIVE INTERVIEW: DORTMUND INAVYOTISHIA UTAWALA WA BAYERN MUNICH KWENYE SOKA LA UJERUMANI








Sunday, May 27, 2012

RIPOTI KAMILI: OKWI AZIKOSA SHEREHE UBINGWA - KABURU ATANGAZA KAGO NA WALULYA WAMETEMWA RASMI

Gervas Kago

MAMIA ya mashabiki wa soka walijitokeza kwenye mitaa mbalimbali Dar es Salaam jana wakati wachezaji wa Simba wakipita na Kombe lao la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Msafara wa wachezaji wa Simba pamoja na baadhi ya viongozi wao wa benchi la ufundi ulianzia mchana makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi na kupita mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam na kisha kuelekea ukumbi wa Dar Live, Mbagala ambako umati mkubwa ulijitokeza.


Simba jana iliandaa sherehe ya kujipongeza kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2011/2012.


Hata hivyo baadhi ya wachezaji nyota wa Simba hawakuwepo katika msafara huo kutokana na wengine kuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzanai ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast Jumamosi.


Wakati huohuo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema klabu yake haina mpango na wachezaji Ferick Walulya wa Uganda na Gervais Kago wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.


Alisema wachezaji hao mikataba yao imeisha, hivyo Simba haitahitaji kuwaongezea na kwamba watakuwa huru kujiunga na timu nyingine.


Akizungumzia vipaumbele katika usajili wa mwaka huu, alisema ina mkakati wa kuboresha
zaidi usajili katika safu ya beki wa kati.

Pia alisema wanahitaji kupata mrithi wa kiungo mahiri wa timu hiyo aliyefariki hivi karibuni
kwa ajali ya gari, Patrick Mafisango.

Aliongeza kuwa klabu yake imejipanga kuhakikisha kuwa usajili wa mwaka huu unafanyika
kiumakini zaidi huku akisisitiza kuwa nguvu pia itawekwa katika kuwasajili wachezaji wa kikosi cha vijana cha timu hiyo

No comments: