Tuesday, January 31, 2017

Dar yaburuza mkia Matokeo ya Kidato cha Nne Kitaifa.



PICHA KWA HISANI YA MWANANCHI COMMUNICATIONS



Baraza la Mitihani la Taifa NECTA leo limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne, ambapo katika matokeo hayo, mkoa wa Dar es Salaam umejikuta ukishika mkia Kitaifa baada ya kutoa shule Sita kati ya Kumi zilizoshika mkia.
Katibu mkuu wa NECTA Dkt. Charles Msonde akitangaza matokeo hayo amezitaja shule hizo kuwa ni Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole, Somangila Day na Kidete.
Shule nyingine Nne zinazokamilisha idadi ya shule Kumi za mwisho na mikoa yake kwenye mabano ni Masasi (Pwani), Dahani (Kilimanjaro), Ruponda (Lindi) na Makiba ( Arusha)

No comments: