Saturday, December 31, 2016

Wazazi na walezi watakaotelekeza watoto sikukuu ya Mwaka Mpya Mtwara kutiwa nguvuni.

Image result for thobias sedoyeka

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Thobias Sedoyeka.


Juma Mohamed,Mtwara

Wazazi na walezi mkoani Mtwara wametakiwa kuwachunga watoto wao katika sherehe za sikukuu ya mwaka Mpya, na kwamba atakaepotelewa na mtoto kwa uzembe atachukuliwa hatua za kisheria.
Wito huo umetolewa mkoani hapa na kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Thobiasi Sedoyeka na kuongeza kuwa jeshi hilo halitokua na huruma kwa mzazi yeyote atakaetelekeza mtoto wake.
Jeshi hilo limeendelea kutoa tahadhari za kiusalama kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanakuwa waangalifu na kuhepuka kuendesha vyombo vyao wakiwa wamelewa, pamoja na kuwataka wafanya biashara wa Baa kuhakikisha wanafunga biashara zao katika muda uliopangwa.

No comments: