Friday, November 25, 2016

Wanaume Mtwara wanakumbwa na ukatili wa kijinsia.


Baadhi ya wageni waalikwa na wanachama wa Kituo cha Ushauri na Msaada wa Kisheria Mtwara PARALEAGEL wakiwa katika ufunguzi wa maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani.



Juma Mohamed, Mtwara

Ikiwa Jamii inaelekea kuadhimisha siku ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia Desemba 10 mwaka huu, huko mkoani Mtwara matukio ya aina hiyo yanawakumba wanaume lakini wanashindwa kuyaripoti kutokana na sababu mbalimbali.
Wakizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na kituo cha ushauri msaada wa kisheria PARALIGO mkoani humo, baadhi ya wanaume walitoa ushuhuda wa matukio hayo licha ya jamii kuamini kuwa wanaofanyiwa vitendo hivyo ni wanawake na watoto.
“Kwa mfano kuna jirani yetu mmoja hivi akirudi nyumbani mkeo anamfungia ndani anampiga hata kama akitimiza mahitaji yote..alafu tena anamsachi mfukoni anamchukulia chochote ambacho anacho asubuhi Yule mwanaume anadharau anaenda kufanya kazi zake kama kaiwaida..” alisema Shaibu Salum mkazi wa Mtwara.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dokta Khatibu Kazungu, akizungumza jambo katika ufunguzi wa maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani, yaliyoandaliwa na kituo cha Ushauri na Msaada wa Kisheria Mtwara PARALEAGEL.



Naye mwenyekiti wa dawati la jinsia mkoa wa Mtwara Bahati Sembela, anaeleza kukithiri kwa malalamiko juu ya vitendo hivyo huku akidai kuwa waathirika wakubwa ni wanawake na watoto
Maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yamezinduliwa leo mkoani Mtwara ambapo yanafikia mwaka wa 9 sasa toka kuanza kuadhimishwa kwake mwaka 2007.

 

No comments: