Monday, August 1, 2016

‘UKUTA’ wa Chadema kanda ya kusini kufanya maandamano na mikutano ya hadhara 8,762


Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya kusini, Philbert Ngatunga, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa maazimio ya kamati kuu ya chama hicho juu ya kufanya maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.

Mwenyekiti wa Chademakanda ya kusini, Khamisi Namangaya (kulia) akiwa na katibu wake Philbert Ngatunga na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Lindi, Latifa Chande.



Juma Mohamed, Mtwara.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya kusini kimesema kinatarajia kufanya maandamano na mikutano ya hadhara 8,762 katika mikoa Mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma inayounda kanda hiyo, kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.
AKitangaza maazimio hayo, katibu wa chama hicho kanda ya kusini, Philbert Ngatunga, alisema hatua hiyo ni kuunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya chama hicho ambayo yametangaza kuanza kufanya maandamano na mikutano ya hadhara ifikapo Septemba Mosi mwaka huu katika oparesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA), yenye lengo la kupinga kile ilichokiita ukandamizaji wa demokrasia
“Kila ngazi ya chama ndani ya kanda ya kusini itafanya hilo jambo na tunalisimamia lazima lifanyike, kwahiyo kwa ujmla wake kuanzia ngazi ya msingi mpaka ngazi ya kanda pekeyake, kila ngazi itafanya na kwa ujumla kutokana na hesabu ambazo nimewaambia kutakuwa na jumla ya maandamano na mikutano ya adhara 8,762 kwa hii mikoa mitatu ya kanda ya kusini..” alisema.

Viongzi wa Chadema kanda ya kusini wakiwa na wabunge wa viti maalumu wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.



Aidha, chama hicho kimepingana na kauli za msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi, kwamba wamekiuka misingi ya sheria ya vyama vya siasa na kumtaka azipime kauli zake hizo.
“Tunamshangaa na tunampinga kauli iliyotolewa na msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi..Francis Mutungi, kwakusema kwamba baada ya mwenyekiti (Freeman Mbowe) kutoa maazimio yale mbele ya waandishi wa habari ameonesha kwamba Chadema inataka kuleta vurugu, Chadema inakiuka misingi ya sheria za vyama vya siasa..kwahiyo sisi ile kauli aliyoitoa July 27 Jaji Mutungi msajili wa vyama vya siasa anatakiwa aipime upya..” aliongeza Ngatunga.
Chama hicho kimepanga kuanza kuendesha maandamamo pamoja na mikutano ya hadhara nchi nzima katika kutekeleza oparesheni yake ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA), yenye lengo la kupinga kile ilichokiita ukandamizaji wa demokrasia.




No comments: