Monday, June 27, 2016

ATUPELE: Ndanda walichelewa kufanya maamuzi.






Atupele Green akiwa mazoezini msimu uliopta na timu ya Ndanda Fc






Na Juma Mohamed, Mtwara

MSHAMBULIAJI Atupele Green ambaye msimu uliopita wa alikipiga kwa mafanikio na klabu ya Ndanda Fc, amejiunga rasmi na klabu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mshambuliaji huyo ameiambia Juma News kuwa, sababu ya yeye kuamua kuachana na Ndanda ni kutokana na viongozi wa timu hiyo kuchelewa kufanya naye mazungumzo na kwamba walipoamua kufanya hivyo alikuwa tayari amesha ingia mkataba na Ruvu.
"Wao kutokuwa kwao haraka kufanya maamuzi ndio imepelekea mimi kusaini JKT Ruvu..lakini nawashukuru mashabiki wa Ndanda najua walikua pamoja na mimi kwa kipindi chote lakini ni kawaida kwa mchezaji kuhama nikitolea mfano hata Christiano Ronaldo aliondoka Machester United akaenda Real Madrid." alisema.
Alisema uamuzi huo pia ameangalia mustakabali wa baadae wa maisha yake huku akikiri kwamba alikuwa akiwindwa pia na vilabu vya Simba na Yanga lakini aliamua kujiunga na Ruvu kwasababu aliona wanaendana na matarajio yake ya baadae.
"Najua kuna vitu vingi vitasemwa na maneno mengi yatasemwa, lakini baada ya kushauriana na watu wangu wa karibu tukakubaliana na kufikia hatua ya mimi kusaini JKT Ruvu.."alisema.


Atupele ambaye msimu uliopita aliichezea kwa mafanikio Ndanda Fc na kuweza kuifungia magoli 10 amekiri kuwa na mipango ya kwenda kucheza kwa majaribio nje ya nchi ambao alianza nayo kablaya kumalizika ligi kuu msimu uliopita.
Aidha, alisema atawakumbuka kwa kheri wachezaji wenzake wote ambao alikipiga nao pamoja katika klabu ya Ndanda pamoja na mashabiki ambao walionesha upendo wa dhati kwake kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupachika mabao.
Mashabiki wa Ndanda walisema kuondoka kwa mchezaji huyo ni kutokana na viongozi wa timu hiyo kutokuwa makini katika harakati za kuwabakisha wachezaji wao kwasababu walitakiwa kuanza kuzungumza nae kabla ligi haijamalizika.

Atupele Green katika moja ya mechi za Ndanda



Kwa upande wake, afisa habari wa Ndanda Fc, Idrissa Bandari, alisema waliwahi kufanya naye mazungumzo mchezaji huyo lakini hawakuweza kufikia makubaliano na kudai kuwa inawezekana mazungumzo yao hayakuwa na tija kwake.
"Tulijiandaa kama timu kwa mchezaji kama yeye ambaye alifanya vizuri katika kikosi chetu mambo mawili yangeweza kutokea, kuendelea kumshawishi abaki au aende kwenye timu nyingine kwahiyo tulijiandaa kwa mambo hayo ingawa kitu cha kwanza hakikuwa kwa yeye kuondoka.." alisema Bandari.
Aliongeza kuwa mwalimu Malale Hamsini tayari ameshapata mbadala wa Atupele (hakumuweka wazi) ambaye wanatarajia atakuwa na uwezo kama au zaidi ya Atupele na wakati ukifika wataweka wazi.

No comments: