Sunday, May 1, 2016

Haji Mwinyi arejea Dimbani Yanga Sc

Hajji Mwinyi amepona majeruhi ya misuli aliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri
Kikosi cha Yanga kimezidi kuimarika baada ya kurejea kwa beki wake, Hajji Mwinyi aliyepona majeruhi ya misuli aliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Beki huyo ameiambia Goal, hivi sasa yupo fiti kabisa na yupo tayari kuendelea kuitumikia timu yake katika mechi zilizo salia za mashindano yote ambayo timu yake inashiriki.
“Niliumia misuli ambayo ilinilazimu kukaa nje wiki mbili na kukosa mechi nne za ligi na moja ile ya marudiano na Al Ahly, lakini nafurahi kuona nimepona na nimerejea kwenye kikosi ni kocha tu kuona kama atanitumia kwenye michezo iliyo mbele yetu,”amesema Mwinyi .
Beki huyo wa kushoto mwenye uwezo mubwa wa kupanda mbele na kupiga krosi zenye madhara anakabiliwa na wakati mgumu kurudi kwenye nafasi yake kwani mbadala wake Oscar Joshua amekua akifanya vizuri kwenye mechi zote alizocheza.
CHANZO: Goal

No comments: