Friday, March 4, 2016

PICHAZ..Mazishi ya aliyekua mwandishi wa Pride Fm-Hassan Lingundula.

Safari ya kwenda kuupumzisha mwili wa aliyekuwa mwandishi wa kituo cha redio cha Pride Fm cha mkoani Mtwara, Hassan Lingundula, katika makaburi ya kijijini kwao Dinyecha, halmashauri ya mji wa Nanyamba.



Wazee na wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mtwara wakisoma dua kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa marehemu Hassan Lingundula, kijijini kwao Dinyecha, Nanyamba.


Dua ya kuuombea mwili wa marehemu Hassan Lingundula.



Dua kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa Hassan Lingundula


Mwili wa Hassan Lingundula ukiwa katika jeneza ukisomewa kabla ya kwenda kuupumzisha katika makaburi ya katani Dinyecha, halmashauri ya mji wa Nanyamba ambako ndio nyumbani kwao marehemu.



Safari ya mazishini..


Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Hassan lingundula..Aaamen.


No comments: